Hali ya mtaani kwako baada ya Matokeo ya NEC

marine 1

Member
Jul 29, 2015
60
67
Poleni kwa Mihangaiko ya kutafuta riziki Wakuu,

Huku nilipo Kumepoa sana, yaani kila mtu hana hamu ya chochote baada ya NEC kumtangaza mshindi wa uchaguzi mkuu hapo jana.

Ningependa kujua mtaani kwako hali ikoje?
 
Arusha ni kimya sana, wahindi wengi wamefunga maduka ila waswahili wanapiga kazi. Ulinzi umeimarishwa na amani inatawala
 
Chaguo langu hajashinda na tulimchagua kwa wingi nashangaa wachache kushinda
 
Poleni kwa Mihangaiko ya kutafuta riziki Wakuu,

Huku nilipo Kumepoa sana, yaani kila mtu hana hamu ya chochote baada ya NEC kumtangaza mshindi wa uchaguzi mkuu hapo jana.

Ningependa kujua mtaani kwako hali ikoje?

Huku mpaka mtoto wa primary kanuna!!! Hatuna furaha na hii mvhi tena
 
kila mtu kazini kwangu amejiinamia! n huzuni na simanzi! binafsi sijalala kwa siku mbili pamoja na wadogo zangu; tena kuna mmoja yupo shulen alinipigia simu analia ikaniongezea uchungu! machozi ya watanzania yataenda bure! Mungu atalipa! sisi tumefundshwa kuushinda ubaya kwa wema!
 
Huku kwetu kumepokea kama siku ileeee ya tarehe 14 October 1999 alipofariki Nyerere. Yaani mji umezizima kwa huzuni...
 
Mimi huku nilipo niliweka dau na mtu na tukaandikishiana kabisa kuwa magufuli akishinda ninampa elfu 50.Lakini cha kushangaza hata kunidai au kukumbushia tu hakuna.Nahisi hata yeye anajua kuwa magufuli hajashinda bado.
 
Back
Top Bottom