Hali ya mchungaji Gwajima mahututi ICU

Hali ya mchungaji Gwajima mahututi ICU

Status
Not open for further replies.
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
JESHI LA POLISI TANZANIA

PRESS RELEASE
29/03/2015

WATU 15 WAKAMATWA NA JESHI LA POLISI KWA TUHUMA ZA KULA NJAMA NA KUJARIBU KUMTOROSHA ASKOFU GWAJIMA AKIWA HOSPITALINI.
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linawashikilia na kuwahoji watu 15 ambao wanatuhumiwa kwa makosa ya kula njama pamoja na kujaribu kumtorosha Askofu Josephat Mathias Gwajima ambaye amelazwa katika Hospitali ya TMJ kwa matibabu.
Mnamo tarehe 29/03/2015 majira ya saa tisa na dakika thelathini usiku watu hao 15 katika hali isiyo ya kawaida walifika hospitalini hapo wakidai kwamba walikuwa wanataka kwenda kumuona mgonjwa huyo. Askari ambao wapo katika lindo hilo waliwatilia mashaka watu hao hivyo waliwakatalia kuingia. Kundi hilo la watu 15 lilijaribu kutumia nguvu kuingia katika chumba alicholazwa askofu Gwajima lakini walikamatwa na kikosi maalum cha Polisi ambacho kabla ya tukio hilo walikuwa wanafuatilia mwenendo wa kundi hilo.
Baada ya kukamatwa watuhumiwa hao walipekuliwa hapo hapo TMJ na kukutwa na Begi ambalo lilikuwa na vitu mbalimbali kama ifuatavyo:
Silaha ambayo ni Bastola aina ya BERRETA yenye namba CAT5802 ikiwa na risasi tatu.
Risasi 17 za Shortgun.
Vitabu viwili vya Hundi (Cheque Books)
Hati ya kusafiria yenye jina la GWAJIMA JOSEPHAT MATHIAS yenye namba AB 544809.
Kitabu cha Hundi cha EQUITY Bank.
Nyaraka mbalimbali za kampuni ya PUMA
Chaja ya Simu na Tablets
Suti mbili na nguo za ndani.
Orodha ya watuhumiwa waliokamatwa ni kama ifuatavyo:
CHITAMA S/O MWAKIBAMBO, Miaka 32, Fundi Selemala, Mkazi wa Gongolamboto.
EDWIN S/O AUDEX, Miaka 24, Mchungaji, Mkazi wa Kawe Maringo.
ADAM S/O MWASELELE, Miaka 29, Mhandisi, Mkazi wa Kawe Maringo.
FREDERICK S/O FUSI, Miaka 25, Mkazi wa Mbezi Beach.
FRANK S/O JOHN MINJA, Miaka 24, Mwanafunzi IMTU, Mkazi wa Mbezi Beach.
EMMANUEL S/O NGWELA, Miaka 28, Mlinzi Shirikishi, Mkazi wa Keko Juu.
GEOFREY S/O WILLIAM, Miaka 30, Mhadhiri UDSM, Mkazi wa Survey Chuo Kikuu.
MATHEW S/O NYANGUSI, Miaka 62, Mchungaji, Mkazi wa Mtoni Kijichi.
BONIPHACE S/O NYAKYOMA, Miaka 30, Mchungaji, Mkazi wa Kitunda.
GEOFREY S/O ANDREW, Miaka 31, Dereva, Mkazi wa Kimara Baruti.
DAVID S/O MGONGOLO, Miaka 24, Mchungaji, Mkazi wa Ubungo Makoka.
GEORGE S/O MSAVA, Miaka 45, Mfanyabiashara, Mkazi wa Ilala Boma.
NICHOLAUS S/O PATRICK, Miaka 60, Mchungaji, Mkazi wa Mbagala Mission.
GEORGE S/O KIWIA, Miaka 37, Dalali wa magari, Mkazi wa Tandale Uzuri.
YEKONIA S/O BIHAGAZE, Miaka 39, Mchungaji, Mkazi wa Kimara Stop Over.
Baada ya upekuzi kukamilika watuhumiwa walifikishwa kituo cha Polisi cha Oysterbay kwa mahojiano zaidi ikiwa ni pamoja na kupata uhalali wa wao kumiliki silaha hizo na risasi mpaka walipokamatwa.
Upelelezi wa shauri hilo unaendelea kwa madhumuni ya kubaini sababu za njama hizo sambamba na kujua mbinu zote zilizotumika kutaka kufanikisha jaribio la kumtorosha Askofu Josephat Mathias Gwajima.

S. H. KOVA
KAMISHNA WA POLISI KANDA MAALUM
DAR ES SALAAM
 
Pamoja na kuwa mkatoriki, Gwajima amesimamia ukweli na tutamkumbuka daima

Ni shujaa wa Jeshi LA Bwana na ndiyo sababu Mungu amehifadhi uhai wake!
Wiki ijayo tutakuwa bondeni tena na kiongozi wetu tukibomoa falme za giza kama kawaida!
 
Na bado, dhambi ya kumtukana mpakwa mafuta itaendelea kuwatafuna.

Tunaomba mzee wetu Kova utusaidie na huo mkusanyiko wao wa packers uondoshwe mara moja, tumechoshwa na makelele ya zile spika zao.
Tangu huyu gwajima ahamie kawe ni kerooo!
 
Uhuru wa kuongea upo ila Uhuru baada ya kuongea hakuna..
 
Na bado, dhambi ya kumtukana mpakwa mafuta itaendelea kuwatafuna.

Tunaomba mzee wetu Kova utusaidie na huo mkusanyiko wao wa packers uondoshwe mara moja, tumechoshwa na makelele ya zile spika zao.
Tangu huyu gwajima ahamie kawe ni kerooo!

Waondoe nalile hekalu LA mashetani opposite na uwanja lenye vipaza sauti linatupigia kelele kwa lugha isoyoeleweka tukiwa club triple 7!
 
yani kuhojiwa tu na polisi pressure imempanda, siku akihijiwa na Mungu kwa yale matusi itakuwaje,mbwebwe kibao kumbe ndina tu.
wale waandishi wa habari waliompa kipaza sauti ndio wahojiwe, unajua asilimia 50 ya waandishi wa habari huwa wanatumiwa na serikali. isije kuwa walichomoa kipaza sauti chao wakaweka bandia chenye dawa.
 
POSTED SUNDAY, MARCH 29, 2015
Gwajima chini ya uangalizi maalumu TMJ
Hali ya Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima inaendelea vizuri, ingawa

> Askofu wa Kanisa la Ufufuo na uzima ,Josephat Gwajima akihudumiwa na muuguzi wa hospitali ya TMJ, Dar es Salaam jana.Askofu Gwajima amelazwa katika hospitali hiyo baada ya kuzimia wakati akihojiwa na polisi juzi.Picha na Salim Shao.

ADVERTISEMENT
Dar es Salaam. Hali ya Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima inaendelea vizuri, ingawa haijabainika anasumbuliwa na tatizo gani kiafya hadi hapo vipimo vitakapopatikana.

Gwajima aliyelazwa katika chumba cha wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalumu kwenye Hospitali ya TMJ, Mikocheni, Dar es Salaam alifikishwa hospitali hapo juzi usiku baada ya hali yake kubadilika ghafla alipokuwa akihojiwa Kituo Kikuu cha Polisi, Kanda Maalumu ya Dar es Salaam.

Askofu huyo alijisalimisha kituoni hapo juzi mchana akiitikia wito wa polisi uliomtaka kufanya hivyo kutokana na tuhuma za kutoa lugha chafu dhidi ya Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki, Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo.

Akizungumza na gazeti hili hospitalini hapo jana, Dk Fortunatus Mazigo anayemtibu kiongozi huyo wa kiroho alisema kuwa hali yake haijabadilika tangu afikishwe hospitalini hapo jana (juzi) usiku.

Alisema hadi sasa bado hawajafahamu ana tatizo gani kutokana na kutokamilika kwa baadhi ya vipimo, ingawa kuna matumaini kutokana na kuwa na hali nzuri katika mfumo mzima wa damu, mapigo ya moyo na viungo vyote vinafanya kazi.

“Sina cha kusema kuhusu ugonjwa wake kwa sababu hiyo ni siri ya anayeumwa na daktari, ninachoweza kusema hali yake aliyokuja nayo jana usiku haijabadilika, ingawa kuna matumaini kwa sababu vitu muhimu vipo sawa,” alisema Dk Mazigo.

Hali ilivyo hospitalini hapo

Waumini kutoka katika Kanisa na Ufufuo na Uzima walikuwa wakipishana hospitalini hapo jana ili kumwangalia kiongozi wao ambaye amelala kitandani, akiwa hawezi kuzungumza.

Mchungaji Yekonia Biyagaze ndiye anafanya kazi ya ziada kuhakikisha waumini wanaoshindwa kupata nafasi ya kuingia wodini kumwona kiongozi wao wanapata maelezo ya kina kutoka kwake kuhusiana na kinachoendelea kwa mgonjwa huyo.

Baadhi ya waumini waliozungumza na gazeti hili hospitalini hapo, walieleza kushtushwa kwao.

Muumini aliyejitambulisha kwa jina la Masinde alisema kuwa anachofahamu kiongozi wake alikuwa Arusha na alirudi ili kutii amri ya polisi ya kutakiwa kufika kituoni hapo kwa ajili ya mahojiano.

“Nimeshtuka, natamani ufanyike uchunguzi wa kina tubaini nini kinaendelea ni kiongozi mkubwa na ni muhimu kwetu kama waumini wake, sitarajii kama litatokea jambo baya, kwani inaweza kuwa hatari,” alisema muumini huyo.

Masinde alisema walikuja wengi, lakini baada ya kupewa maelezo na Mchungaji Biyagaze wakaamua kuondoka ili kupisha na wengine wapate nafasi ya kumjulia hali kwa sababu kila mmoja anataka kusikia au kuona kwa macho badala ya kuambiwa akiwa mbali.

Awali, kabla ya kufika katika wodi hiyo kulikuwa na askari kadhaa waliovaa kiraia waliozunguka eneo hilo kwa kupanda juu ghorofani alipo Askofu Gwajima na kushuka, ambapo baada ya muda walipungua na kubaki wachache.

Kabla ya kuingia chumba cha mgonjwa

Tofauti na ilivyozoeleka kuwa unapotaka kuingia chumba cha mgonjwa mnapewa maelekezo na daktari, katika kile kinachoonekana kuhakikisha usalama unakuwapo.

Aliyekuwa na jukumu la kutoa maelekezo kwa watu wote wanaokwenda kumwona mgonjwa, wakiwamo wanahabari ni Mchungaji Biyakaze, ambaye aliwataka wakiingia ndani wasishike kitanda, wala shuka kwa usalama wao.

Hata baada ya kuingia, kundi la watu Askofu Gwajima hakufumbua macho wala kupepesa, hali inayoonyesha kuwa bado yupo katika hali isiyoridhisha.

Akiwa amelala chali, huku amefungwa mashine ya kupimia mapigo ya moyo mkononi, chumbani humo kulikuwa na muuguzi aliyekuwa anaratibu kila kinachoendelea, ikiwamo kuwazuia watu wasiguse kitu chochote.

Kabla ya kuingia ndani na kumwona mgonjwa, Mchungaji Biyakaze alizungumzia hali ya mgonjwa alisema anaendelea vizuri, ingawa alishindwa kumalizia na kubaki akisema...lakini na kumalizia kusema kuwa kinachonipa moyo wa kuwa atapona kwa sababu ni mtumishi wa Mungu sina jingine.

Mlangoni mwa wodi alimolazwa Askofu Gwajima kulikuwa na watu ambao hawatoki muda wote, mmojawao alipopewa pole alisema kuwa asipewe pole kwani huo ni ushindi na hakuna mapambano yasiyokuwa na vikwazo.

“Usinipe pole, nipongeze huu ni ushindi na ndiyo mapambano yalivyo lazima kuwe na vigingi, ambavyo ukivivuka unakuwa umeshinda na sisi tumeshinda,” alisema kijana huyo.

Slaa, Baregu wafika hospitalini

Saa sita mchana, Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk Willibroad Slaa alifika hospitalini hapo akiongozana na Mjumbe wa Kamati Kuu, Profesa Mwesiga Baregu kumwona Gwajima.

Baada ya kumwona mgonjwa, Dk Slaa alizungumzia utata unaowapata watu wanaohojiwa na polisi, huku akisisitiza kuna vitu vinatakiwa kufanyiwa kazi, ikiwamo kubaini kuna nini.

Alisema sheria za kuhojiwa zipo wazi kuwa mtu asihojiwe zaidi ya saa nane, vitu kama hivyo vinatakiwa kuzingatiwa katika mahojiano.

“Nyinyi kama waandishi ndiyo kazi yenu kuangalia kwa undani kuna nini kinaendelea katika haya mahojiano hadi mtu anapoteza fahamu, siyo huyu hata kama kuna mwingine ilimtokea hali hiyo,” alisema Dk Slaa.

Akizungumza hali ya mgonjwa kwa mtizamo wake, alisema kuwa daktari anayemtibu hawajawafahamisha nini kimempata, lakini kwa bahati mbaya hata mgonjwa mwenyewe hawezi kuzungumza na wao hawakuweza kumuuliza chochote, hivyo hana la kusema.

“Angekuwa anazungumza, labda angeniambia ilikuwaje, lakini hawezi hivyo sijapata lolote kutoka kwake wala daktari,” alisema Dk Slaa.

Souse :- mwananchi
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom