Hali ya Kisiasa: Ridhiwan Kikwete anapumulia mashine Jimboni

Kama kuna watu waliamini ahadi namba 1 basi tatizo la ujinga nchi hii ni kubwa kuliko tunavyofikiri
 
Huyu riz1 alitumia pesa kupata ubunge wala hakuwa anakubalika na kiukweli Hana alichofanya hapa Chalinze si yeye wala Baba yake poor them wameshindwa kuijenga Kwao hawana maana


Sent using Jamii Forums mobile app

Ridhiwan hana mpinzani hapo Chalinze kwani kura za ushindi hazitoki Chalinze mjini bali zipo vijijini ambako bwana Riz kajichimbia na ukitaka kujua moto huo tembelea vijijini
 
Kwenda bungeni sio wote walikubaliwa, hata unao waona pale wamechaguliwa hivyo swali kuwa mbona hayuko bungeni sio swali. Pili, we ungejua kuwa mama kachaguliwa mbunge wa kuteuliwa ungenyamaza tu kimya. Toka lini First Lady aliyepita akachaguliwa mbunge wa kuteuliwa?? Jua kwamba kuna kitu inaundwa hapo. Iko siku Hliary wetu naye atatokea TZ. Akitokea nadhani hata baba naye atarudi kuja kula bata. Hivyo Rizi kuukosa ubunge labda atake mwenyewe lakini si kuondolewa na mtu baki
 
Hakuna wa kumtoa ridhiwani Chalinze hilo haliwezekani na halitawezekana

Ukweli ni kwamba kama wakwere wanaweza kumtoa Jakaya huko Msoga basi wataweza kumtoa Ridhwani kama mbunge Chalinze!!! Kampeni ya Ridhwani ni kampeni ya Jakaya Kikwete!!
 
Ukweli ni kwamba kama wakwere wanaweza kumtoa Jakaya huko Msoga basi wataweza kumtoa Ridhwani kama mbunge Chalinze!!! Kampeni ya Ridhwani ni kampeni ya Jakaya Kikwete!!
Wakumtoa Riziwani labda Kikwete mwenyewe au Makonda angombee ila hakuna mwingine sijui nani hilo haliwezekani kabisa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wakumtoa Riziwani labda Kikwete mwenyewe au Makonda angombee ila hakuna mwingine sijui nani hilo haliwezekani kabisa

Wewe ni mtu wa ajabu sana; yaani Jakaya Rais Mstaafu arudi kuwa mbunge badala ya mwanae? Makonda hata kwa ndumba za kisukuma hawezi kumshinda Ridhwani kwao Chalinze hata awe boya namna gani!!
 
Fisi wameanza kulana wao kwa wao...:D

Everyday is Saturday...................... :cool:
 
Wewe ni mtu wa ajabu sana; yaani Jakaya Rais Mstaafu arudi kuwa mbunge badala ya mwanae? Makonda hata kwa ndumba za kisukuma hawezi kumshinda Ridhwani kwao Chalinze hata awe boya namna gani!!
Makonda hawawezi shindwa kokote maana ushindi wake ni wa bao la mkono iwe mvua liwe jua Makonda atashinda.
Kuhusu Kikwete ninamna ya kuwasilisha wewe itakuwa umri mdogo au elimu haijakusaidia kulinganisha mtu haina maana ya kwamba iwe kweli.
Nikimshindanisha Magufuli kwa Vladimir Putin haina maana kuwa Magufuli atakwenda kugombea Russia au Putin aje Tanzania
Ni ulinganifu tu wa kuweka ukubwa wa jambo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Makonda hawawezi shindwa kokote maana ushindi wake ni wa bao la mkono iwe mvua liwe jua Makonda atashinda

Sio mbele ya Vasco Dagama pengine mbele ya JIWE; kumbuka Vasco Dagama ndio aliyemuumba huyu Makonda!! Makonda alikuwa anafunga gidamu za Ridhwani!!!
 
Mbunge wa Jimbo la Chalinze Ridhiwan Kikwete anapumulia mashine Jimboni kutokana na hali mbaya ya kisiasa uchaguzi mkuu 2020 hali inayomfanya ashindwe kuhudhuria bunge la bajeti na kuweka kambi Jimboni kufanya kampeni .

Ridhiwan Kikwete amekosa uungwaji mkono kutokana na utendaji wake dhaifu na kushindwa kutelekeza ahadi alizotoa kwa wananchi wakati anachaguliwa mwaka 2015 . Utekelezaji wa ahadi zake ni sawa na asilimia 0.00000 , wakati anachaguliwa alitoa ahadi kumi zilizowavutia wananchi wakiamini huyu ni mtoto wa Rais hakuna kinachoshindikana , ahadi hizo ni ;
1. Kuifanya Chalinze kuwa Dubai
2. Kujenga soko la kimataifa
3. Kujenga stendi ya kisasa
4. Kugawa trekta moja kila kijiji
5. Kujenga uwanja wa mpira wa kisasa
6. Kutoa Ambulance moja kila kata
7. Kuwawezesha vijana wa bodaboda
8. Kuwawezesha wanawake
9. Kuwapa studio ya kisasa wasanii
10. Tatizo la maji kuwa historia

Mbunge huyo kwa Sasa ameacha vikao vya bunge na kujichimbia kuzunguka Jimboni kukutana na wajumbe wa mkutano mkuu akiwafuata na kufanya vikao , amenukuliwa akiwaomba msamaha ili aungwe mkono tena wakati wa kura za maoni . Kila anakopita wajumbe wamemhoji kwa ujasiri MWENZETU UMEKUJA KUAGA ? ULIKUWA WAPI MIAKA YOTE ? KWANINI HUPOKEI SIMU ZA WANANCHI ? OFISI YAKO IKO WAPI ?UMEFANYA NINI MIAKA MITANO ? KWANINI HAUKO BUNGENI NA BADALA YAKE UNAZURURA HUKU ?

Kwa hali ya kisiasa ilivyo Ridhiwan Kikwete hawezi kutetea nafasi yake kwakuwa hakuna alichokifanya , alitelekeza Jimbo kwa muda mrefu , pia anaponzwa kwa dharau na kiburi chake .

WANAOMNYIMA USINGIZI

kwa mujibu wa duru za siasa za Chalinze Kuna watia nia wawili wanaomfanya Ridhiwan Kikwete akose usingizi na kuhaha kama faru aliyejeruhiwa , watia nia hao ni pamoja na ;

1. SAIDI ZIKATIMU, huyu ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Chalinze anayetajwa kufanya kazi nzuri ya kusimamia Halmashauri kukusanya mapato ya kutosha na kutelekeza miradi mingi ya maendeleo kwa kutumia mapato ya ndani ikiwemo sekta ya Elimu , Afya na kutoa mikopo kwa wanawake na vijana .

ZIKATIMU anatajwa kufanya kazi nzuri mithili ya mbunge ikiwemo kusikiliza kero za wananchi na kuzitatua na amekuwa kimbilio la wananchi wengi hivyo kuonekana anafaa kuinuliwa kuwa mbunge wa Jimbo la Chalinze ili aweze kuwatumikia wananchi.

2. RAMADHANI MANENO ; huyu ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Pwani na mbunge wa zamani wa Jimbo la Chalinze 2005-2010 . Maneno anatajwa kutia nia kugombea Ubunge kurejea kwenye kiti chake baada ya miaka kumi aliposhindwa kwenye uchaguzi wa kura za maoni ndani ya chama mwaka 2010 .

Jimbo limewaka moto !!!



Sent using Jamii Forums mobile app

Taaraifa yako umeandika kwa panic sana. Jifunze kuadika mambo aya kwa utulivu.
 
Naamini Ridhiwani bado anahitaji nafasi ingawa kwa utawala huu wabunge wengi majimboni kilio ni hiko hiko hakuna cha maana kilichofanyika.

Baba yake Mzee Jakaya alijenga nchi,akasahau mkoa Pwani alipozaliwa. Hakuna barabara inayounganisha Wilaya zote za mkoa na makao makuu ya mkoa Kibaha, Rufiji,Kisarawe (hakuna lami),Mkuranga,Chalinze,Bagamoyo,Kibiti na Mafia lazima upitie Dar.

Umeme aliacha maeneo mengi hayajaunganishwa,maji mpaka Leo bado shida.

Hata mradi wa Bandari Bagamoyo alitarajia mrithi wake ndio autekeleze ili kuepuka lawama. Anyway tunashukuru aliijenga Dar es Salaam,ambapo hapo awali ilijuwa makao makuu ya mkoa wa Pwani.
 
Back
Top Bottom