Hali ya Kisiasa: Ridhiwan Kikwete anapumulia mashine Jimboni

Mbunge wa Jimbo la Chalinze Ridhiwan Kikwete anapumulia mashine Jimboni kutokana na hali mbaya ya kisiasa uchaguzi mkuu 2020 hali inayomfanya ashindwe kuhudhuria bunge la bajeti na kuweka kambi Jimboni kufanya kampeni .

Ridhiwan Kikwete amekosa uungwaji mkono kutokana na utendaji wake dhaifu na kushindwa kutelekeza ahadi alizotoa kwa wananchi wakati anachaguliwa mwaka 2015 . Utekelezaji wa ahadi zake ni sawa na asilimia 0.00000 , wakati anachaguliwa alitoa ahadi kumi zilizowavutia wananchi wakiamini huyu ni mtoto wa Rais hakuna kinachoshindikana , ahadi hizo ni ;
1. Kuifanya Chalinze kuwa Dubai
2. Kujenga soko la kimataifa
3. Kujenga stendi ya kisasa
4. Kugawa trekta moja kila kijiji
5. Kujenga uwanja wa mpira wa kisasa
6. Kutoa Ambulance moja kila kata
7. Kuwawezesha vijana wa bodaboda
8. Kuwawezesha wanawake
9. Kuwapa studio ya kisasa wasanii
10. Tatizo la maji kuwa historia

Mbunge huyo kwa Sasa ameacha vikao vya bunge na kujichimbia kuzunguka Jimboni kukutana na wajumbe wa mkutano mkuu akiwafuata na kufanya vikao , amenukuliwa akiwaomba msamaha ili aungwe mkono tena wakati wa kura za maoni . Kila anakopita wajumbe wamemhoji kwa ujasiri MWENZETU UMEKUJA KUAGA ? ULIKUWA WAPI MIAKA YOTE ? KWANINI HUPOKEI SIMU ZA WANANCHI ? OFISI YAKO IKO WAPI ?UMEFANYA NINI MIAKA MITANO ? KWANINI HAUKO BUNGENI NA BADALA YAKE UNAZURURA HUKU ?

Kwa hali ya kisiasa ilivyo Ridhiwan Kikwete hawezi kutetea nafasi yake kwakuwa hakuna alichokifanya , alitelekeza Jimbo kwa muda mrefu , pia anaponzwa kwa dharau na kiburi chake .

WANAOMNYIMA USINGIZI

kwa mujibu wa duru za siasa za Chalinze Kuna watia nia wawili wanaomfanya Ridhiwan Kikwete akose usingizi na kuhaha kama faru aliyejeruhiwa , watia nia hao ni pamoja na ;

1. SAIDI ZIKATIMU, huyu ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Chalinze anayetajwa kufanya kazi nzuri ya kusimamia Halmashauri kukusanya mapato ya kutosha na kutelekeza miradi mingi ya maendeleo kwa kutumia mapato ya ndani ikiwemo sekta ya Elimu , Afya na kutoa mikopo kwa wanawake na vijana .

ZIKATIMU anatajwa kufanya kazi nzuri mithili ya mbunge ikiwemo kusikiliza kero za wananchi na kuzitatua na amekuwa kimbilio la wananchi wengi hivyo kuonekana anafaa kuinuliwa kuwa mbunge wa Jimbo la Chalinze ili aweze kuwatumikia wananchi.

2. RAMADHANI MANENO ; huyu ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Pwani na mbunge wa zamani wa Jimbo la Chalinze 2005-2010 . Maneno anatajwa kutia nia kugombea Ubunge kurejea kwenye kiti chake baada ya miaka kumi aliposhindwa kwenye uchaguzi wa kura za maoni ndani ya chama mwaka 2010 .

Jimbo limewaka moto !!!



Sent using Jamii Forums mobile app
Alitegemea kutekeleza hayo yote ikiwa bamdogo angepokea kijiti kutoka kwa baba yake (kaka mtu) lakini bahati haikuwa hivyo!
 
Sio mbele ya Vasco Dagama pengine mbele ya JIWE; kumbuka Vasco Dagama ndio aliyemuumba huyu Makonda!! Makonda alikuwa anafunga gidamu za Ridhwani!!!
Maisha yanabadilika sasa hivi Riziwani ndiye mfunga viatu wa Makonda kwasasa Makonda ndiye kiongozi mkuu (kama alivyo zitto act) wa Ccm Tanzania analolisema linakuwa la taifa hakuna wa kumpinga.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Riz-1 hawezi kurudi wala mama yake, yaani mama Salma ambaye hajawahi kutoa mchango zaidi ya mara mbili kwa bunge zima hawarudi, mama salma alipewa tu ili kuficha ile kitu yake nanii
 
Jamaa aliahidi vitu vikubwa mno! Kwani wananchi waliamini kwamba atatekeleza? Yaani mbunge afanye mkoa uwe kama Dubai? Heheheheheee....!
 
Sio rahisi kihivyo. Baba yake sio Rais tena, akikosa na ubunge atabaki na nini? Ni mwanasheria lakini sijui kama amewahi kuingia hata mahakama ya mwanzo kutetea mwizi wa kuku. Biashara zenyewe wakati huu ni changamoto, tena bila msaada wa cheo chake na cha baba yake, atapata tabu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hivi kabisa unamaanisha na akili yako inakubali kua Ridhiwani hata akikosa ubunge ataadhirika au kupata tabu? Hv unajua Rais mstaafu analipwa 80% ya mshahara wa Rais aliye madarakani,kwani unafikiri kikwete anashindwa kumlipa mwanae Ridhiwani mshahara sawa na wa ubunge akiamua ni Basi tu dogo anataka status tu
 
Sio rahisi kihivyo. Baba yake sio Rais tena, akikosa na ubunge atabaki na nini? Ni mwanasheria lakini sijui kama amewahi kuingia hata mahakama ya mwanzo kutetea mwizi wa kuku. Biashara zenyewe wakati huu ni changamoto, tena bila msaada wa cheo chake na cha baba yake, atapata tabu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hakuna kitu kama hicho. Hizo njaa za kiwango hicho hawezi kuzifikia. Huyu ni mtoto wa Jk. Raisi mstaafu wa JMT. Hiyo title tu inamlisha yeye na familia mpaka afe. Labda apigane na serikali.
 
Hakuna kitu kama hicho. Hizo njaa za kiwango hicho hawezi kuzifikia. Huyu ni mtoto wa Jk. Raisi mstaafu wa JMT. Hiyo title tu inamlisha yeye na familia mpaka afe. Labda apigane na serikali.

Au Serikali iamue kupigana na yeye.

My point ni, kama huna nguvu za kisiasa Afrika, uko kwenye hatari. Angalia yanayoikuta familia ya Dos Santos huko Angola.
 
Hivi kabisa unamaanisha na akili yako inakubali kua Ridhiwani hata akikosa ubunge ataadhirika au kupata tabu? Hv unajua Rais mstaafu analipwa 80% ya mshahara wa Rais aliye madarakani,kwani unafikiri kikwete anashindwa kumlipa mwanae Ridhiwani mshahara sawa na wa ubunge akiamua ni Basi tu dogo anataka status tu
Hujanielewa.

Ubunge wako si kwa ajili ya mshahara, kwanza mshahara wa wabunge hapa Tanzania ukilinganisha na "majukumu" wanayopewa na wananchi, familia na ndugu sio mshahara wa maana. Wanachogombania ni political influence inayokuja na huo ubunge. Hilo ndio la muhimu, na wengi wakikosa mambo yao hayaendi sawa. Wewe unadhani Shabiby au Abood kwenye siasa wamefuata mshahara? Ni influence, kuna milango inafunguka kwa sababu ya ubunge wake
 
5 Reactions
Reply
Back
Top Bottom