Hali ya kiredio si shwari, Kiredio akutwa na nini

Hali ya kiredio si shwari, Kiredio akutwa na nini

Jannatul Firdaus

JF-Expert Member
Joined
Aug 4, 2026
Posts
442
Reaction score
1,083
Habari kuhusu kusambaa kwa taarifa za mtangazaji na mwanamtandao maarufu nchini Tanzania, Kiredio, imeshika kasi kwenye mitandao ya kijamii kufuatia tukio la kutapeliwa kiasi cha shilingi milioni 60 za Kitanzania akiwa nchini China.

Inaarifiwa kuwa Kiredio alisafiri kuelekea China kwa ajili ya kufanya shughuli zake za kibiashara, lakini safari hiyo iligeuka kuwa msiba wa kifedha baada ya kuingizwa mkenge na kutapeliwa fedha hizo zote shilingi milion 60, jambo lililomfanya apate mshtuko mkubwa wa kisaikolojia na msongo wa mawazo.

Pigo hilo kubwa la kifedha likiwa ugenini lilisababisha afya ya Kiredio kuanza kudhoofu kwa kasi muda mfupi baada ya tukio hilo. Kudhoofika huko kwa mwili kulipelekea kukutwa na matatizo ya kiafya ambayo vipimo vya awali vimeshindwa kubaini mara moja chanzo chake, jambo linalotajwa na wengi kama ugonjwa usiojulikana unaotokana na mshtuko wa ghafla.

Hivi sasa, mashabiki, marafiki, na wadau mbalimbali kwenye mitandao ya kijamii wanaendelea kutuma jumbe za kumfariji, kumuombea dua, na kumtakia afueni ya haraka ili aweze kuvuka kipindi hiki kigumu cha afya na maumivu ya kupoteza mtaji wake.
 
Attention ua 🦟

Nyumba nyingine bhana🦟🦟🦟


Ma influencer wa dar jau. Sana
 
Kama hela zote ni zake sawa ila kama ni hela za kikundi abanwe pumbu atasema ukweli
 
60m si pesa nyingi kihivyoo ikufanye u paralyze. Labda utuambie Kuna shida nyingine.
 
Back
Top Bottom