Hali ya Kamanda Nassari

Hali ya Kamanda Nassari

mbona umekuwa kimya tena please updates!!!!!!! tunasubiri kwa hamu kujua kinachoendelea
 
Mbona morani waliompiga hawajakamatwa! Kwani hawajulikani? Laigwenan Mkuu Lowassa anapoendelea na kampeni zake za ukuu nchini adhihirishie umma kuhusu utashi wake kwa utawala wa sheria kwa kusaidia kukamatwa hao morani wahalifu.
Nilisikia kuwa katika kundi hilo kulikuwa na vijana wa kisomali walioshiriki kumpiga Nasari. Mtu anayetaka kuwa Rais kwa udi na uvumba anatumia vikundi vya kupiga watu tena vikishirikisha hata Wasomali? Kweli Lowasa hapo umebugi,huna tofauti na Mchemba na sasa watu wamekuelewa.
jambo la ajabu ni kuwa kila anayesifiwa na mwenyekiti kuwa huyu ni jembe basi anaanza kufanya vitendo viovu bila woga.
Alianza Mwigulu kusifiwa pale Dodoma na tumeona matendo yake,majuzi akasifiwa Lowasa kuwa Makuyuni anaiweza sasa tumeona aliyofanya. Nadhani sifa toka kwa mwenyekiti maana yake fanya lolote usihofu una kinga yangu.
 
Nassari amepigwa na nani? au alikuwepo kwenye mlipuko?

Mbona sielewi?
Nassari



  • Nassari alivamiwa, kupigwa na kujeruhiwa sehemu mbalimbali mwilini na watu wanaodaiwa kuwa viongozi na wafuasi wa CCM.



Chaguzi ndogo za udiwani zilizofanyika sehemu mbalimbali ziligubikwa na vurugu wakati hali ilikuwa mbaya zaidi huko Makuyuni mkoani Arusha ambako Mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari alipigwa na wafuasia wa CCM na kulazimika kulazwa hospitalini. Pamoja na vurugu hizo, CCM iliendelea kudhihirisha umwamba wake katika ulingo wa siasa baada ya kujizolea viti vingi vya udiwani wakati wa chaguzi ndogo zilizofanyika sehemu mbalimbali nchini.

Wafuatiliaji wa mambo ya kisiasa walikuwa wanafuatilia kwa kina chaguzi hizo ili kupima joto la kisiasa nchini.
Uchaguzi uliokuwa unasubiriwa kwa hamu ni ule wa Makuyuni wilayani Monduli ambako Mbunge wake ni mwanasiasa maarufu Edward Lowassa.

CCM iliibuka kidedea huko Makuyuni na kufanya maneno ya Rais Jakaya Kikwete kuwa Lowassa ana misuli ya kuifanya CCM ishinde huko Monduli. Lowassa alikuwa na kibarua cha kukabiliana na Chadema waliokuwa wanataka kujipenyeza Monduli ambako hawajahi kuwa na kata tangu mfumo wa vyama vingi uanzishwe.

Hata hivyo, bado CCM haijapata dawa ya ushindi Pemba kwani kilishindwa vibaya na CUF kwenye uchaguzi wa ubunge wa Chambani. Chadema kwa upande wake kilitoa changamoto kwa CCM katika chaguzi hizo za kata na hata kujizolea kata mbili za Iyela huko Mbeya na wilayani Hanan’g huko mkoani Manyara.

Nassari apata kichapo Makuyuni

Nassari alivamiwa, kupigwa na kujeruhiwa sehemu mbalimbali mwilini na watu wanaodaiwa kuwa viongozi na wafuasi wa CCM, akiwa katika harakati za uratibu wa shughuli za upigaji kura za udiwani katika Kata ya Makuyuni, wilayani Monduli.
Nassari aliyekuwa wakala mkuu wa Chadema katika kata hiyo alivamiwa na kundi la watu zaidi ya 30 waliomshambulia kwa fimbo na

Tukio hilo lilitokea jana kati ya Saa 3:00 na 4:00 katika kituo cha kupigia kura cha Kwa Zaburi wakati mbunge huyo alipofika kuangalia maendeleo ya zoezi la kura.

“Mara nilipofika kwenye kituo kile nilikutana na kundi kubwa la vijana wa CCM waliokuwa wamejifunika mashuka ya Kimaasai wakiwa na fimbo mikanoni ambao walinizuia kuingia kituo cha kura, lakini askari na wasimamizi wakaniruhusu baada ya kuwaonyesha kitambulisho cha wakala mkuu,” alisema Nassari
Akizungumza kwa njia ya simu akiwa hospitali ya Seliani Jijini Arusha alikokimbizwa kwa matibabu, Nassari alisema vijana hao wa CCM walimsubiri nje ya kituo na kumvamia mara alipotoka nje na kuanza kumshambulia kwa fimbo na marungu kila sehemu ya mwili.

“Kama siyo kukabiliana nao na kupata upenyo wa kukimbilia bastola yangu niliyoiacha kwenye gari, nadhani ningekuwa marehemu sasa. Nimetokwa na damu nyingi puani na mdomoni. Pia nasikia maumivu makali ya kichwa na kifua,” alisema Nassari
Pamoja na Nassari, kiongozi mwingine wa Chadema aliyeshambuliwa na vijana wa CCM hadi kuokolewa na polisi ni katibu wa chama hicho Wilaya ya Monduli aliyejulikana kwa jina la Thomas Kipese.

Makuyuni (Arusha)
Mgombea wa CCM, Goodluck Lekurunya alipata kura 1547 wakati Josephat Sironga wa Chadema alipata kura 302.

Iyela (Mbeya)
Mgombea wa Chadema, Charles Mkela naye aling’ara kwenye uchaguzi wa kata ya Iyela baada ya kujizolea kura 1918, Richard Shangwi wa CCM alifuatia baada ya kupata kura 1163, Kapaga Mwakibete (NCCR) kura 17, Amosi Mwambagi (DP) kura 20

Dongobesh (Manyara)
Mgombea wa Chadema, Ernest Jorojik aliibuka mshindi baada ya kujizolea kura 1,500 akifuatiwa na Josep Barabojika wa CCM (900), Amon Akonaay wa CUF(123). Walikuwa wawania kuchukua nafasi ya Daniel Siasi aliyefariki dunia.

Bashneti (Manyara)
Msimamizi wa uchaguzi, Julius Lawi alitangaza mgombea wa Chadema, Lawrence Surumbu Tara, alipata kura 2008, Nicodemus Gwandu wa CCM alipata 1,130 na Alloyce Gwandu wa NCCR (253).

Ibugugile (Dodoma)
Leonard Eliya Kagoa (CCM) alichaguliwa kuwa diwani mpya wa katia ya Ibubugile baada ya kupata kura 733 akifuatiwa na Julius Francis Chawenda (Chadema) kura 170 na Aman Madagadi (APPT-Maendeleo) kura sita.

Stesheni (Mtwara)
Msimamizi msaidizi wa uchaguzi, Hassan Masoud alitangaza kuwa CCM imetetea kiti hiki cha Stesheni kilicho wilayani Nachingwea baada ya kura 806 na waliomfuatia ni Ally Luhundu (Chadema) kura 327, Athumani Msauna (CUF) kura 480 na Zawadi Ligawa (ADC) kura 48.

Genge (Tanga)
Steven Mlaguzi wa CCM ameshinda baada ya kupata kura 347, Joseph Komba (Chadema) kura 326, Oledi Abdulrahman (CUF) kura saba.

Tingeni (Tanga)
Aisha Mohamed wa CCM aliibuka kidedea baada ya kupata kura 362, Omar Salim (Chadema) kura 244 na Ramadhan Yahya wa CUF kura nne.

Mimeta (Morogoro)
Athumani Kapati (CCM) alishinda udiwani baada ya kupata kura 1154 na kumshindi wa Michael Madili wa Chadema alipata kura 1004.

Mbalamaziwa (Iringa)
CCM iliibuka kidedea baada ya kupata 1642 na yule wa Chadema aliambulia kura 185.

Iseke (Singida)
Emmanuel Jingu wa Chadema aliibuka kidedea kwenye uchaguzi wa kata hiyo.
 
Anaendelea vizuri.................... mleta mada kaongeza chumvi nyingi.
thanx kaka. taarifa kama hizi zinazotia moyo na zenye ukweli ndio tunazozihitaji.
mungu ni mwema na tunamuombea ahueni ya haraka ndugu nasari
 
Mungu atafanya maajabu na kamanda atapona.nassari tupo pamoja nawe usihofu.
 
Asafirishwe kwenda India

Ndo mnachokijua tu,ina maana nyie magamba mlimpiga ili asafirishwe kwenda India?shame on you mnaotenda matendo maovu na kuvaa miwani ya mbao kwasababu ya vijisenti kdogo, muogope Mungu wako na jua kuna kaburi, I dare say wewe ni mnyama usiyefaa kusimama kati ya wastaarabu, mtu akipigwa regardless of his political affiliation cyo ishu kuandika upuuzi huu, unless umevurugwa.
 
Hilo si jukumu la makamanda tena!! Yupo hospital, is it? Sasa what does makamanda has to do with the medical issues? Tumwombee apone,kisha apone haraka.

Kwani we hujui kuna madaktari makamanda?shame on you
 
Kwa Mungu kila kitu kitahesabiwa kamanda Nassari atpona na atongea hila waliofanya unyama naapa watalipwa tu.!
 
Ndo mnachokijua tu,ina maana nyie magamba mlimpiga ili asafirishwe kwenda India?shame on you mnaotenda matendo maovu na kuvaa miwani ya mbao kwasababu ya vijisenti kdogo, muogope Mungu wako na jua kuna kaburi, I dare say wewe ni mnyama usiyefaa kusimama kati ya wastaarabu, mtu akipigwa regardless of his political affiliation cyo ishu kuandika upuuzi huu, unless umevurugwa.
Nyie si mnasema yuko na hali mbaya, sasa kuna ubaya gani wa mimi kusema apelekwe India kufanyiwa uchunguzi. Au chama kina ogopa gharama?
 
Back
Top Bottom