Hali ya balozi zetu ni mbaya | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hali ya balozi zetu ni mbaya

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by EMT, Apr 14, 2012.

 1. EMT

  EMT JF-Expert Member

  #1
  Apr 14, 2012
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 14,464
  Likes Received: 865
  Trophy Points: 280
  Yamekuwa yakisemwa hapa kwa muda mrefu lakini baadhi ya watu wakawa wanapinga. Katika ripoti yake CAG amedhibitisha kuwa kutolewa kwa fedha pungufu ya bajeti iliyoidhinishwa kumesababisha matatizo makubwa kwa balozi zetu katika kumudu gharama za uendeshaji ikiwa ni pamoja na kushindwa kutekeleza majukumu ya kufanikisha shughuli za diplomasia ya uchumi.

  CAG ametoa mfano kuwa wakati wa ukaguzi walikuta baadhi ya maofisa wa balozi za Tanzania katika nchi za China na Italia ambao hawajarejea nchini kutokana na ukosefu wa fedha, licha ya kumalizika kwa muda wao wa kazi vituoni.

  Pia CAG amesema baadhi ya balozi zimeshindwa kuendeleza viwanja kutokana na uhaba wa fedha. “Tatizo hili limekuwepo kwa muda mrefu sasa licha ya kulitolea taarifa kwenye ripoti yangu ya mwaka jana,” alisema na kutaja baadhi ya vituo hivyo kuwa ni London, Dubai, Kigali na Msumbiji.

  Aidha, amesema matumizi ya ziada kupitia maduhuli yaliyokusanywa na ofisi za balozi zinazokusanywa katika balozi za Tanzania hazisimamiwi kwa ufanisi. Amesema mlipaji mkuu wa serikali anatakiwa kusimamia fedha hizo ambazo zinasababisha kuwepo kwa matumizi ya ziada na yasiyoridhisha.

  Kutokana na kasoro hizo, Sh. 3,013,732,776 zimetumika nje ya bajeti iliyoidhinishwa na Bunge.
   
 2. Nzowa Godat

  Nzowa Godat JF-Expert Member

  #2
  Apr 14, 2012
  Joined: Jun 15, 2011
  Messages: 2,630
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  Sio balozi tu zenye hali mbaya hata halmashauri nyingi ziko hoi kwa sababu zilipewa 35% tu ya badget ya fedha iliyoombwa. Baba aweza kudokoa mboga asijue kumbe mama kaubajeti kwa familia yake. Wakati wa chakula baba asiye muungwana atataka apate share kubwa tena na hivyo watoto kuishia kuramba mchuzi tu. Ndio situation iliopo hapa nchini leo hii. Sijui hata zahanati za huko kwa ma.ga.bach.oli kama tumemaliza madeni ya gharama za matibabu ya politicians.
   
 3. Kobello

  Kobello JF-Expert Member

  #3
  Apr 14, 2012
  Joined: Feb 20, 2011
  Messages: 5,689
  Likes Received: 656
  Trophy Points: 280
  Sikubaliani na hili. Ma-attachee huwa wanaminya kurudi nyumbani.
   
 4. EMT

  EMT JF-Expert Member

  #4
  Apr 14, 2012
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 14,464
  Likes Received: 865
  Trophy Points: 280
  Hata wakipelekewa fedha za kurudi nyumbani bado wanaminya kurudi?
   
 5. Albedo

  Albedo JF-Expert Member

  #5
  Apr 14, 2012
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Wengi wanaishia kuwa walowezi
   
 6. UmkhontoweSizwe

  UmkhontoweSizwe JF-Expert Member

  #6
  Apr 14, 2012
  Joined: Dec 19, 2008
  Messages: 2,971
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Eti tunaongozwa na msomi wa uchumi!
   
 7. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #7
  Apr 14, 2012
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  What a joke!
   
 8. k

  komredi ngosha JF-Expert Member

  #8
  Apr 14, 2012
  Joined: Jan 11, 2011
  Messages: 381
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Simple plan, revolt....you love peace then you will die stupid and unhappy
   
 9. KOMBAJR

  KOMBAJR JF-Expert Member

  #9
  Apr 14, 2012
  Joined: Nov 15, 2011
  Messages: 5,848
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Kazi za balozi zote zinafanywa na Raisi
   
 10. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #10
  Apr 14, 2012
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,474
  Likes Received: 4,134
  Trophy Points: 280
  ni wakati sasa wa Serikali kukiri kuwa imefilisika.
   
 11. Kobello

  Kobello JF-Expert Member

  #11
  Apr 14, 2012
  Joined: Feb 20, 2011
  Messages: 5,689
  Likes Received: 656
  Trophy Points: 280
  YEP, Pesa za kurudi ni dola efu tano tu! ambazo ni sawa na mchango wa Nchimbi kwa marehemu Kanumba.
   
 12. EMT

  EMT JF-Expert Member

  #12
  Apr 14, 2012
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 14,464
  Likes Received: 865
  Trophy Points: 280
  Kama wanapelekewa hizo fedha halafu wanaminya, mpira unarudi kule kule kwa serikali.
   
 13. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #13
  Apr 14, 2012
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,275
  Trophy Points: 280
  Kwani familia zao hawaruhusiwi kupiga box wakiwa huko ughaibuni? Wamarekani ni wabunifu sana kwenye swala hili na sidhani kama mishahara ya ubalozi wa Marekani kama inatoka Marekani maana zile pesa za viza fee za Watanzaia wanavyoibiwa kimachomacho na viza zenyewe hawawapi mpaka roho inauma.
   
 14. Return Of Undertaker

  Return Of Undertaker JF-Expert Member

  #14
  Aug 22, 2012
  Joined: Jun 12, 2012
  Messages: 2,376
  Likes Received: 8,524
  Trophy Points: 280
  Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, Edward Lowassa, amesema balozi zote za Tanzania nje ya nchi zinakabiliwa na hali ngumu ya kifedha, hali inayosababisha morali ya kazi kwa watumishi wake kushuka.

  Amesema hali hiyo inasababishwa na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa kuchelewa kufanya maamuzi, ikiwa ni pamoja na kuwa nzito kujibu barua na simu za watumishi wa balozi hizo wanapohitaji msaada wa kutatua matatizo ya kiuchumi na kifedha.

  Lowassa, ambaye ni Mbunge wa Monduli (CCM), alisema hayo alipokuwa akihojiwa katika kipindi cha Dakika 45 kilichorushwa na kituo cha televisheni cha ITV juzi, kuhusu mambo mbalimbali, ikiwamo hali za balozi za Tanzania kufuatia ziara iliyofanywa na kamati yake kukagua hali za balozi hizo zilizoko katika nchi mbalimbali duniani, hivi karibuni.

  “Wimbo ni mmoja. Liturijia inayoimbwa ni ya aina moja. Hapa watakueleza tatizo la fedha, Canada watakueleza tatizo la fedha, South Afrika watakueleza tatizo la fedha. Kila mahali Liturijia inayoimbwa ni moja. Kwamba kuna matatizo makubwa sana ya fedha kwenye balozi zetu, makubwa sana ya kibajeti, ambayo yametokana na uwezo wa nchi. Lakini ni makubwa kabisa,” alisema Lowassa.

  Alisema kwa mfano, kamati ilifika katika baadhi ya nchi na kushuhudia mishahara ikiwa imechelewa kupelekwa katika baadhi ya balozi kwa miezi sita na nyingine miezi mitatu na kuhoji: “Hivi mtu yuko kule nje, hana mjomba, hana shangazi, anafanyaje?”

  Lowassa alisema hata fedha za kulipia pango ya nyumba za watumishi wa balozi huchelewa kiasi cha kutishiwa kutimuliwa na wenye nyumba na kuhoji: “Aende wapi huyu mtumishi?”

  Alisema wizara imekuwa ikiacha pia kupeleka fedha za gesi kwenye balozi wakati wa baridi, hali ambayo imekuwa ikiwafanya watumishi wa balozi hizo kushindwa kuwasha kipasha joto ili kukabiliana na baridi.

  “Hakuna fedha. Ni matatizo makubwa sana, sana, sana ya fedha. Kwa hiyo, athari zake ziko katika maeneo mengi nje ya nchi. Kuna morali ya watumishi wetu nje ya nchi ni ndogo sana. Na hili linaharibiwa zaidi kwa sababu Wizara ya Mambo ya Nje imekuwa nzito kidogo kujibu barua zao, kujibu simu zao na kuwasaidia wanapokuwa na matatizo hayo ya kiuchumi. Kwa hiyo, ni matatizo makubwa ya kiuchumi,” alisema Lowassa.

  Hata hivyo, alisema kufunga balozi kutokana na hali hiyo, si suluhu, kwani Tanzania bado inahitaji kufungua balozi zaidi na zile zilizopo kufanya kazi kikamilifu kwa vile bado kuna mahitaji makubwa ya kuwapo na balozi katika nchi mbalimbali duniani.

  Kuhusu hali ya uchumi nchini, alisema serikali imefanya mambo makubwa, hasa katika ujenzi wa miundombinu, ambapo barabara nyingi zimejengwa.

  Alishauri mafuta kununuliwa kwa wingi ili kama bei yake itashuka katika soko la dunia, yawepo kwa wingi nchini, pia ulazima wa serikali kupunguza matumizi, mikopo ya nyumba na kusimamia kilimo cha mashamba makubwa na cha umwagiliaji ili kupata chakula cha kutosha ili kukabiliana na mfumuko wa bei.

  Pia alisisitiza ulazima wa kuondokana na matumizi ya jembe la mkono, akisema kamwe haliwezi kusaidia kuimarisha kilimo, badala yake akataka kwenda kwenye matumizi ya nguvu za wanyama kazi na kisha matrekta na kusisitiza umuhimu wa kuingiza kwa wingi matrekta kwa ajili ya kilimo nchini.
   
 15. mtotowamjini

  mtotowamjini JF-Expert Member

  #15
  Aug 22, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 4,540
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Alivyokua Waziri Mkuu hakujua hili swala? maana hili tatizo ni la mda mrefu...Hizo balozi zinapangiwaga bajeti zake na wizara sasa hizo hela hua zinaendaga wapi kwani wizara haijui budget za balozi zote huko nje na kuzipangilia vizuri...msiseme hela hakuna hela zipo sema matumizi ndio ovyo
   
 16. Maundumula

  Maundumula JF-Expert Member

  #16
  Aug 22, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 7,055
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Alipokuwa waziri mkuu alikuwa na mambo mengi sasa hivi mkuu wa kamati concentration yake kwenye maswala haya tu.
   
 17. Lu-ma-ga

  Lu-ma-ga JF-Expert Member

  #17
  Aug 22, 2012
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 2,843
  Likes Received: 472
  Trophy Points: 180
  Sasa naanza kuamini ccm HAITAFIKA 2015 ikiwa na nguvu za kukiwezesha kupigania kubaki madarakani.Ule utabiri uliosema kuwa vingozi wa ccm ni sawa na Wajenga mnara wa BABEL,kwa sasa tunasikia lugha zao zinagongana kana kwamba hawana dira.
  Juzi nilikutana na jamaa yangu mhasibu wa ccm alinitaarifu kuwa ccm hawafiki salama 2015 maana sasa makundi ni hazalani, amenidokeza anataka kuacha kazi kwani anaogopa garika la cdm kumkuta mwajiriwa kwa ni aibu
   
 18. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #18
  Aug 22, 2012
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,326
  Likes Received: 1,793
  Trophy Points: 280
  na ya kugombea uraisi pia nayo yanampa pressure nyingine ndogo ndogo
   
 19. Tungaraza Jr

  Tungaraza Jr Senior Member

  #19
  Aug 22, 2012
  Joined: Feb 3, 2012
  Messages: 196
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Playing SMART to 2015???.............Who knows!
   
 20. N

  Nikupateje JF-Expert Member

  #20
  Aug 22, 2012
  Joined: Dec 22, 2009
  Messages: 1,314
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Niliwahi kuingia kwenye residence ya ubalozi wa Sudan kule karibu na Golden Tulip Hotel. Aisee nilidhani nimeingia nyumba ya mtaani yenye vurugu ya miaka mingi. Ndipo nikajua kwamba kumbe hiyo nyumba walipewa miaka ya zamani enzi za Nyerere na haijafanyiwa matengenezo huwezi amini.

  Binafsi ninaposafiri nje huwa sipiti kwenye balozi zetu. Lakini kama nako hali ni kama nilivyoona ubalozi wa Sudan basi ni watu wa kuhurumia na tusijidanganye kwamba kila anayekaa Masaki, Msasani au Oysterbay basi yuko kama tulivyozoea kufikiri.
   
Loading...