"Hali ya BABA WA TAIFA mbaya, Uingereza"

Kivumah

JF-Expert Member
Jan 7, 2008
2,428
1,050
wana jamvi, mwezi huu unatimiza Mwaka wa 11 sasa tangu Mwalimu atutoke. forever we will miss u MWALIMU
 

Attachments

  • nyerere.jpg
    nyerere.jpg
    18.3 KB · Views: 80
  • nyerere2EY.jpg
    nyerere2EY.jpg
    7.6 KB · Views: 94
Aliona balaa lililokuwa mbele yetu ndo maana alitulilia mpaka dakika ya mwisho ya uhai wake.
Aliona kuwa tangu vijana wake waamue kwenda Zenji kurekebisha azimio la arusha baas watanzania watateseka mno.
Lakini kwa umoja, udugu na ujasiri aliotupatia tutautumia kuamua hapo oktoba 31 kwamba tuendelee kuteseka au tubadili uongozi na kuweka wanaotujali zaidi.
Sio kazi rahisi kuuondoa mbuyu njia panda. lakini ukishaondoka njia inakuwa nyeupee kupitika
 
...alituambia ili Nchi iendelee inahitaji vitu vinne, WATU, ARDHI, SIASA SAFI na UTAWALA BORA.
..alisema kipindi cha Utawala wake adhabu waliopewa Mafisadi na Wala Rushwa ilikuwa ni mbali ya kwenda Jela lkn pia mtuhumiwa atachapwa viboko 12, 6 wakati anaingia Jela na 6 wakati anatoka akamuonyeshe Mkewe...
...alisema Mtu ambaye anajiandikisha kupiga kura halafu siku ya uchaguzi haendi kupiga kura ni MPUMBAVU.!!!
 
Alisema bila ya CCM....nchi itayumba watu watu mpaka leo wanaogopa kufanya mabadiliko...to hell with mwalimu!
 
Najua kutokana na kiwango kibaya cha masomo Bongo, watu hata wale unaodhania kidogo wameelimika , kama wale wanaochangia humu, huonesha dhahiri kiwango kibovu cha elimu. Mfano nimesoma mchango wa mtu anayeandika laisi (rahisi au rais),hatali, aluki (haruki), lizika (ridhika), galama (gharama) n.k. Ajabu ni kuwa mara nyingi hawafanyi makosa hayo wanapoandika Kiingreza! Nataka kumsahihisha Kivumah juu ya kauli mbiyu ya zamani ya TANU. Ili tuendelee....' ya mwisho ni UONGOZI BORA na si UTAWALA BORA. Katika Kiswahili, tofauti ya utawala na uongozi ni kubwa. Utawala ni ule unaofanywa na mgeni juu ya wazalendo. Iwapo mtawala ni mzalendo, yeye huitwa kiongozi na 'utawala wake' huitwa uongozi. Vijana wa siku hizi hawapambanui kati ya haya. Utawakuta wanasema, utawala wa Kikwete!
 
Atuombee kwa Mola ili tuwe na uchaguzi wa amani na tupate RAISI anaekelwa na umaskini,ujing na maladhi yetu
 
Back
Top Bottom