PISTO LERO
JF-Expert Member
- Mar 8, 2011
- 2,819
- 1,454
HALI si shwari ndani ya Jumuiya ya Wazazi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), baada ya Diwani wa Kata ya Magomeni, Julian Bujugo kufungua kesi Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam akiitaka Jumuiya hiyo kumlipa Sh3 bilioni kama gharama alizotumia kukarabati majengo ya Shule ya Sekondari Kaole iliyopo Bagamoyo mkoani Pwani.
Sekondari hiyo awali ilikuwa chini ya jumuiya hiyo lakini baada ya kushindwa kujiendesha, ilichukuliwa na Bujugo ambaye aliikarabati na kuibadilisha kuwa Chuo cha Kilimo Kaole, ambapo huchukua asilimia 75 ya mapato huku asilimia 25 zikienda katika mfuko wa Jumuiya hiyo.
Hatua hiyo imekuja siku tatu baada ya Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo Taifa, Abdallah Bulembo kumtaka Bujugo aikabidhi shule hiyo kwa jumuiya kabla hajachukuliwa hatua za kisheria.
Katika maelezo yake, Bulembo alisema Bujugo hana haki ya kuendelea na ujenzi wowote katika majengo ya chuo hicho kwa kuwa mikataba aliyoingia na jumuiya ni feki na haina baraka za Baraza Kuu wa Wadhamini la Wazazi, huku akifafanua kuwa diwani huyo alikabidhiwa shule ili awe meneja lakini alikiuka makubaliano na kuifanya kuwa chuo.
Akizungumza na waandishi wa habari jana Dar es Salaam, Bujugo alisema kesi hizo namba 16 na 20 amezifungua juzi, ikiwa ni wiki mbili tangu kupewa barua na jumuiya hiyo akitakiwa kusimamisha ujenzi wa chuo hicho.
"Nimefungua kesi namba 16 ambayo inalenga kuizuia jumuiya kutowasumbua wanachuo na kesi ya pili ni namba 20 ambayo inawataka wanilipe gharama nilizotumia kukarabati chuo" alisema.
Alifafanua, "Niliingia nao mkataba ambao tuliusaini mwaka 2010 kati yangu mimi, aliyekuwa mwenyekiti wa jumuiya ambaye kwa sasa ni marehemu, Athumani Mhina pamoja na katibu ambaye mpaka sasa yupo katika jumuiya, Khamis Dady" alisema Bujugo huku akionyesha mkataba huo.
Akifafanua fedha anazoidai jumuiya hiyo alisema ili kuyaachia majengo ya chuo hicho, ameitaka jumuiya hiyo ya wazazi kumlipa Sh3 bilioni kama gharama alizotumia kufanya ukarabati.
"Wakati wananikabidhi shule hii niliwakuta walimu wanadai fedha na nikawalipa Sh45 milioni.
Nimelipa madeni ya Mamlaka ya Mapato (TRA)Sh65 milioni, umeme nilikuta wanadaiwa Sh15 milioni, nilitumia zaidi ya Sh1.8 bilioni kufanya ukarabati wa majengo, ukiweka na gharama nyingine inafikia Sh3 bilioni," alisema Bujugo na kuongeza; "Ninachotaka ni wao kunilipa gharama zinizotumia, sina kinyongo na mtu na wala sitaki kuking'ang'ania chuo.
Kwanza pale chuoni kuna wanafunzi 300 wanashindwa kusoma kwa sababu ya mvutano huu." Akizungumzia kauli hiyo Bulembo aliliambia gazeti hili jana kwa njia ya simu kwamba, msimamo wake uko palepale na chuo hicho ni lazima kirudi mikononi mwa jumuiya hiyo. "Nilishasema hata nilipokuwa wilayani Bagamoyo, mikataba ile aliyoingia ni feki na lazima chuo kirudi mikononi mwa jumuiya" alisema Bulembo