Hali si shwari Jumuiya ya Wazazi CCM

Hali si shwari Jumuiya ya Wazazi CCM

bujugo huyu jamaa wa home kabisa ila hovyo sana,si bora hizo asset akawasaidia anakotoka badala ya kutapeli mjini
 
Mbona swala dogo tu hili. Mama diwani alete vithibitisho vya gharama aliyotumia, then utaratibu wa kumrudishia ufanyike.


BUJUGO ni mwanaume jamii ya MACCM!.. Anaishi ki CCM .. CCM, Kifisadi fisadi tu!.. Dili kacheza na MaCCM wenzie, leo wanamruka!.
 
Japo ni kweli hali si shwari kule 'Wazazi CCM',

lakini nako nao Ma-Kada kibao CCM nao hivi sasa wanamchukia Kinana hakuna fanania yake; madai yakiwa ni kwamba huyo mwakilishi rasmi wa MASLAHI YA MAFISADI chamani na katika biashara mbalimbali nchini hivi sasa anasomwa kama MHARIBIFU MKUBWA aliyetumwa na Lowassa kuja kukiua kabisa chama chao hata kabla ya 2015.

Habari ndio hiyo!!!

Kuhusu Lowasa kumtumia Kinana ni kweli na haina ubishi.
Last month katika vikao vya siri vya lowasa vinavyofanyika nyumbani kwake, yeye lowasa alisema kwa kinywa chake kuwa Kinana ni tegemeo lake la pekee ktk kusimama kama mgombea wa ubunge Arusha mjini 2015, wapambe wa lowassa walimsihi kuwa Kinana hakubaliki Arusha ila Lowasa alijibu kuwa anajua kuwa arusha ni ngome ya chadema na ni pagumu kweli ila mpaka sasa mtu pekee anayemwamini ni Kinana.
Nilihamaki sana nilipojua kuwa Kinana ni mteule mtiifu wa Lowasa.
 
Nini maana ya neno KINANA kwa luga ya kwenu
 
Uhai una sehemu kuu 3:- KUZALIWA, KUKUA & HATIMAYE KUFA. Hawa sasa ni wa KUANIKA JUANI mazishi ni 2015. Wananchi tusirudie tena kosa
 
What goes around comes around, walifadhili uasi ndani ya CDM sasa dhambi hiyo imewarudia acha wafe nayo.
 
Safi sana wabuluze mahakamani ili washike adabu maccm wezi sana!
 
Bujugo tapeli mali ya jumuiya atajimilikishaje kienyeji!!! Kama kweli alitumia bilioni 3 si angejenga na kuanzisha chuo chake mwenyewe kikubwa chenye hadhi totauti na chuo cha Kaole ambacho kiko hohehahe!!!
 
Baada ya Kinana kuteuliwa na Rais ( Mwenyekiti wa CCM) jina lake lilirudishwa kwa wanaCCM kwa ajili ya kuthibitishwa kukubali au kumkataa, kama walikuwa hawamtaki kwa nini hawakumkataa?

Unamuuliza nani "kwa nini"
 
HALI si shwari ndani ya Jumuiya ya Wazazi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), baada ya Diwani wa Kata ya Magomeni, Julian Bujugo kufungua kesi Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam akiitaka Jumuiya hiyo kumlipa Sh3 bilioni kama gharama alizotumia kukarabati majengo ya Shule ya Sekondari Kaole iliyopo Bagamoyo mkoani Pwani.

Sekondari hiyo awali ilikuwa chini ya jumuiya hiyo lakini baada ya kushindwa kujiendesha, ilichukuliwa na Bujugo ambaye aliikarabati na kuibadilisha kuwa Chuo cha Kilimo Kaole, ambapo huchukua asilimia 75 ya mapato huku asilimia 25 zikienda katika mfuko wa Jumuiya hiyo.

Hatua hiyo imekuja siku tatu baada ya Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo Taifa, Abdallah Bulembo kumtaka Bujugo aikabidhi shule hiyo kwa jumuiya kabla hajachukuliwa hatua za kisheria.

Katika maelezo yake, Bulembo alisema Bujugo hana haki ya kuendelea na ujenzi wowote katika majengo ya chuo hicho kwa kuwa mikataba aliyoingia na jumuiya ni feki na haina baraka za Baraza Kuu wa Wadhamini la Wazazi, huku akifafanua kuwa diwani huyo alikabidhiwa shule ili awe meneja lakini alikiuka makubaliano na kuifanya kuwa chuo.

Akizungumza na waandishi wa habari jana Dar es Salaam, Bujugo alisema kesi hizo namba 16 na 20 amezifungua juzi, ikiwa ni wiki mbili tangu kupewa barua na jumuiya hiyo akitakiwa kusimamisha ujenzi wa chuo hicho.

"Nimefungua kesi namba 16 ambayo inalenga kuizuia jumuiya kutowasumbua wanachuo na kesi ya pili ni namba 20 ambayo inawataka wanilipe gharama nilizotumia kukarabati chuo" alisema.

Alifafanua, "Niliingia nao mkataba ambao tuliusaini mwaka 2010 kati yangu mimi, aliyekuwa mwenyekiti wa jumuiya ambaye kwa sasa ni marehemu, Athumani Mhina pamoja na katibu ambaye mpaka sasa yupo katika jumuiya, Khamis Dady" alisema Bujugo huku akionyesha mkataba huo.

Akifafanua fedha anazoidai jumuiya hiyo alisema ili kuyaachia majengo ya chuo hicho, ameitaka jumuiya hiyo ya wazazi kumlipa Sh3 bilioni kama gharama alizotumia kufanya ukarabati.

"Wakati wananikabidhi shule hii niliwakuta walimu wanadai fedha na nikawalipa Sh45 milioni.

Nimelipa madeni ya Mamlaka ya Mapato (TRA)Sh65 milioni, umeme nilikuta wanadaiwa Sh15 milioni, nilitumia zaidi ya Sh1.8 bilioni kufanya ukarabati wa majengo, ukiweka na gharama nyingine inafikia Sh3 bilioni," alisema Bujugo na kuongeza; "Ninachotaka ni wao kunilipa gharama zinizotumia, sina kinyongo na mtu na wala sitaki kuking'ang'ania chuo.

Kwanza pale chuoni kuna wanafunzi 300 wanashindwa kusoma kwa sababu ya mvutano huu." Akizungumzia kauli hiyo Bulembo aliliambia gazeti hili jana kwa njia ya simu kwamba, msimamo wake uko palepale na chuo hicho ni lazima kirudi mikononi mwa jumuiya hiyo. "Nilishasema hata nilipokuwa wilayani Bagamoyo, mikataba ile aliyoingia ni feki na lazima chuo kirudi mikononi mwa jumuiya" alisema Bulembo
well done bulembo. nilifikiri wewe ni kopo kumbe ni jembe. fukuza wezi wote wa mali za umma jumuiya ya wazazi. watu watu wanasema etu hujasoma. wao waliosoma wamefanya nini. again well done mkuu.
 
Bulembo mpenda kesi!
Huyu si ndo anamiliki kampuni ya uwakala wa kukusanya kodi za halmashauri husika ktk mikoa mbali mbali? (Metro merchandise)
Jumuiya ya wazazi wakae mkao wa kwenda mahakamani kila kukicha. jamaa shule hakuna ila anapenda kesi balaa.
Hapo alipo ananuka kesi kibao na nyingi tu ameshapigwa chini na anatakiwa alipe fidia za mamilioni ya pesa.
hiyo jumuiya kwisha habari yake!
tusubiri tuone.
 
Baada ya Kinana kuteuliwa na Rais ( Mwenyekiti wa CCM) jina lake lilirudishwa kwa wanaCCM kwa ajili ya kuthibitishwa kukubali au kumkataa, kama walikuwa hawamtaki kwa nini hawakumkataa?

Umesahau kura za maruhani? ulitegemea wangemkataaje wakati washaambiwa ukipiga kura ya hapana kwa chaguo la raisi hiyo kura ni ya maruhani
 
Back
Top Bottom