Hali Ngumu: Njooni tujuzane bei za mahindi/unga kwenye mkoa uliopo

Swizzy

JF-Expert Member
Nov 4, 2016
773
514
habari wanaJF!!!!

kama kichwa cha habari kinavyo jieleza na tunajua chakula kikuu kwa watanzania wengi ni ugali wa mahindi.

mimi niko mkoa wa mbeya huku bei ya mahindi imepanda sana tena kwa asilimia 100+ hapo mwanzo tulikuwa tuna nunua Plastic moja(ndoo ya lita ishirini) kwa Tsh7000 - 8000/= lakini leo hii plastic moja (ndoo ya lita20) tuna nunua kwa Tsh18,000/= hadi Tsh 20,000/=

kwa hizo bei kuna wanambeya saizi kula ugali imekuwa adimu sana kwa sababu ya hizo bei za mahindi kupanda kwa kiasi kikubwa. Na kama tunavyojua kwa hali ya kawaida Mtanzania kula vyakula vingine kwa mda mrefu pasipo kula ugali inafikia kipindi anakuwa na hamu na ugali.

Na Mbeya ni miongoni mwa mikoa inayo zalisha mahindi kwa wingi hapa Tz, sasa kama bei za mbeya zipo juu hivi je mikoa mingine bei zipoje?.

TUSAIDIANE KUJUZANA HAPA bei za Mahindi na Unga kwa huo mkoa uliopo wewe.

............NAWASILISHA..........
 
Bora hata Mbeya hapo kuna namna ya kubadili chakula wali, ndizi, majimbi, viazi nk. maeneo mengine hicho kitu hakipo
 
Tanga hali sio mbaya saana, kilo ya unga ni 1700 na mchele ni 2700 tuu bila kuxahau nyanya kilo ni 2500 mpaka 3000 yaani mukideeeee
 
Unga kilo sh 1700 na mchele 2700 halafu hali sio mbaya sanaa du! Wewe utakuwa sio mwananchi wa kawaida.
 
habari wanaJF!!!!

kama kichwa cha habari kinavyo jieleza na tunajua chakula kikuu kwa watanzania wengi ni ugali wa mahindi.

mimi niko mkoa wa mbeya huku bei ya mahindi imepanda sana tena kwa asilimia 100+ hapo mwanzo tulikuwa tuna nunua Plastic moja(ndoo ya lita ishirini) kwa Tsh7000 - 8000/= lakini leo hii plastic moja (ndoo ya lita20) tuna nunua kwa Tsh18,000/= hadi Tsh 20,000/=

kwa hizo bei kuna wanambeya saizi kula ugali imekuwa adimu sana kwa sababu ya hizo bei za mahindi kupanda kwa kiasi kikubwa. Na kama tunavyojua kwa hali ya kawaida Mtanzania kula vyakula vingine kwa mda mrefu pasipo kula ugali inafikia kipindi anakuwa na hamu na ugali.

Na Mbeya ni miongoni mwa mikoa inayo zalisha mahindi kwa wingi hapa Tz, sasa kama bei za mbeya zipo juu hivi je mikoa mingine bei zipoje?.

TUSAIDIANE KUJUZANA HAPA bei za Mahindi na Unga kwa huo mkoa uliopo wewe.

............NAWASILISHA..........
 
Hiyo ndiyo nchi ya viwanda iliyokuwa inasubiriwa. Tujiandae kwa uongezeko jipya. Mpaka ifike 2020 bei ya sukari itakuwa 5,000
 
Tumeshaambiwa tulie tugaragare hakuna kitachobadilika kwangu mimi nimeshakubaliana na hali yenyewe utafanyaje sasa kulalamika haisaidii kitu
 
Back
Top Bottom