Mohammed Hamad
JF-Expert Member
- Jan 17, 2011
- 3,988
- 1,308
Hali nchini Côte d'Ivoire baada ya upatanishi kushindwa
Großansicht des Bildes mit der Bildunterschrift: Rais Laurent Gbagbo
Viongozi wa bara la afrika wameingia mbioni kumshinikiza Laurent Gbagbo akubali kuondoka kwa khiari madarakani.Rais anaetambuliwa kimataifa anahimiza hata nguvu zitumike ikilazimika.
Rais wa Côte d`Ivoire anaetambuliwa kimataifa Alassane Dramane Ouattara amesisitiza umuhimu wa kutumiwa nguvu ikilazimika,kumng'owa madarakani rais aliyemaliza wadhifa wake Laurent Gbagb😵uattara amesema hayo wakati wa mahojiano pamoja na ripota wa DW mjini Abidjan,
Mbali na ripota wa DW mjini Abidjan,Alassane Outtara alizungumza pia na maripota wa shirika la habari la Reuters na kudai hatua kali zichukuliwe.Amefahamisha hata hivyo vikwazo vya kiuchumi pindi vikichukuliwa basi vimlenge Gbagbo tuu na na washirika wake na sio raia wa kawaida wa nchi hiyo inayozalisha kakao kwa wingi kabisa ulimwenguni.
Bildunterschrift: Großansicht des Bildes mit der Bildunterschrift: Alassane Ouattara na mjumbe wa Umoja wa Afrika Raila Odinga
Akiulizwa kwa muda gani mgogoro huu utaendelea,na kama ukiselelea ataendelea kusalia katika Hoteli Golf,rais huyo anaetambuliwa kimataifa Alassane Dramane Ouattara amesema:
"Hasha,mgogoro hautadumu muda mrefu.Nimeshasema na nnasema tena,lengo letu ni kuona hali inarejea kuwa ya kawaida kabla ya mwisho wa mwezi huu.Na nnaamini hivyo ndivyo itakavyokuwa.Jumuia ya maendeleo ya kiuchumi Afrika Magharibi ECOWAS imesema wazi kabisa,kwamba Laurent Gbagbo lazma ang'oke madarakani.Hayo yamesemwa tangu december 7 iliyopita-Wiki sita zimeshapita sasa.Ni sawa kwamba ECOWAS ina muongozo wake na hivi sasa pia viongozi wa kijeshi wanakutana mjini Bamako.Baadae watakuja Bouake kutuarifu.Lakini na sisi pia tunajitahidi upande wetu katika sekta ya kidiplomasia na fedha ili kuhakikisha Laurent Gbagbo anaondoka madarakani.Hawezi peke yake kushindana na ulimwengu mzima."
Bildunterschrift: Großansicht des Bildes mit der Bildunterschrift: Vikosi vya Umoja wa mataifa vinapiga doria mjini Abidjan
Waziri mkuu mteule wa Côte d'Ivoire Guillaume Sorro alikwenda Togo na Burkina faso jana,katika juhudi za kuwatanabahisha viongozi wa nchi hizo wazidi kumtia kishindo Laurent Gbagbo.
Wakuu wa kijeshi wa jumuia ya uashirikiano wa kiuchumi ya Afrika Magharibi walisema baada ya mkutano wao mjini Bamako Mali wamesema wako tayari,hata kama wanaendelea na maandalizi.
Mjumbe maalum wa Umoja wa Afrika ,waziri mkuu wa Kenya Raila Odinga yuko Afrika kusini kwa mazungumzo pamoja na rais Jacob Zuma baada ya kushindwa juhudi zake mjini Abidjan.
Wakati huo huo tume ya Umoja wa mataifa nchini Côte d'Ivoire imesema wa-Côte d'Ivoire wapatao 29 elfu wamekimbilia Liberia na mkuyapa kisogo machafuko yaliyozuka baada ya uchaguzi kati kati ya mwezi uliopita.Watu 260 wameuwawa kufuatia machafuko hayo.
Mwandishi:Hamidou Oummilkheir/afp,reuters
Mpitiaji:Abdul-Rahman
Großansicht des Bildes mit der Bildunterschrift: Rais Laurent GbagboViongozi wa bara la afrika wameingia mbioni kumshinikiza Laurent Gbagbo akubali kuondoka kwa khiari madarakani.Rais anaetambuliwa kimataifa anahimiza hata nguvu zitumike ikilazimika.
Rais wa Côte d`Ivoire anaetambuliwa kimataifa Alassane Dramane Ouattara amesisitiza umuhimu wa kutumiwa nguvu ikilazimika,kumng'owa madarakani rais aliyemaliza wadhifa wake Laurent Gbagb😵uattara amesema hayo wakati wa mahojiano pamoja na ripota wa DW mjini Abidjan,
Mbali na ripota wa DW mjini Abidjan,Alassane Outtara alizungumza pia na maripota wa shirika la habari la Reuters na kudai hatua kali zichukuliwe.Amefahamisha hata hivyo vikwazo vya kiuchumi pindi vikichukuliwa basi vimlenge Gbagbo tuu na na washirika wake na sio raia wa kawaida wa nchi hiyo inayozalisha kakao kwa wingi kabisa ulimwenguni.
Bildunterschrift: Großansicht des Bildes mit der Bildunterschrift: Alassane Ouattara na mjumbe wa Umoja wa Afrika Raila OdingaAkiulizwa kwa muda gani mgogoro huu utaendelea,na kama ukiselelea ataendelea kusalia katika Hoteli Golf,rais huyo anaetambuliwa kimataifa Alassane Dramane Ouattara amesema:
"Hasha,mgogoro hautadumu muda mrefu.Nimeshasema na nnasema tena,lengo letu ni kuona hali inarejea kuwa ya kawaida kabla ya mwisho wa mwezi huu.Na nnaamini hivyo ndivyo itakavyokuwa.Jumuia ya maendeleo ya kiuchumi Afrika Magharibi ECOWAS imesema wazi kabisa,kwamba Laurent Gbagbo lazma ang'oke madarakani.Hayo yamesemwa tangu december 7 iliyopita-Wiki sita zimeshapita sasa.Ni sawa kwamba ECOWAS ina muongozo wake na hivi sasa pia viongozi wa kijeshi wanakutana mjini Bamako.Baadae watakuja Bouake kutuarifu.Lakini na sisi pia tunajitahidi upande wetu katika sekta ya kidiplomasia na fedha ili kuhakikisha Laurent Gbagbo anaondoka madarakani.Hawezi peke yake kushindana na ulimwengu mzima."
Bildunterschrift: Großansicht des Bildes mit der Bildunterschrift: Vikosi vya Umoja wa mataifa vinapiga doria mjini AbidjanWaziri mkuu mteule wa Côte d'Ivoire Guillaume Sorro alikwenda Togo na Burkina faso jana,katika juhudi za kuwatanabahisha viongozi wa nchi hizo wazidi kumtia kishindo Laurent Gbagbo.