Hali mbaya SANA.... sikitiko

Hali mbaya SANA.... sikitiko

wana parallel supply yao... Hata hao wa upanga huwa wanaenda kwenye madanguro yao kawe na msasani

mkuu wafanyabiashara wanne au kumi
yasituganye tuchukie wahindi wote
wapo wahindi malofa vile vile na ni waathirika wa tatizo hili pia
 
Ushauri wa Zitto ni mzuri sana, ikifika deadline hakuna kilichofanyika, basi Jk akiwa amiri jeshi mkuu aamuru jeshi kuisimamia utekelezaji wa amri ya ewura na wizara. Ila nina wasiwasi na uwezo wa jk katika hili.

Ila hii nshu ni zaidi ya inavyoonekana, wenye mafuta ndo wadhamini wa ccm, tena yawezekana kabisa wenye uhusiano mkubwa na gamba lililokwanguliwa, sasa hii ishu imegeuka kuwa kitanzi kwa serikali, jamaa wamegrab hii chance kulipiza kisasi, kulipuana hadharani. Inaturudisha kwenye vita ya kuvuana magamba.
 
mkuu wafanyabiashara wanne au kumi
yasituganye tuchukie wahindi wote
wapo wahindi malofa vile vile na ni waathirika wa tatizo hili pia
nasema hivi... wahindi hawako affected mkuu

acha ubishi, wana parallel supply yao....

chunguza useme

Sichukii wahindi wala waarab bali naweka wazi kwamba they have the upper hand kwenye hili
 
nasema hivi... Wahindi hawako affected mkuu

acha ubishi, wana parallel supply yao....

Chunguza useme

sichukii wahindi wala waarab bali naweka wazi kwamba they have the upper hand kwenye hili

nina familly member wahindi na waarabu
na wao wengine wamepanga foleni za mafuta na wengine wamenunua kwa
bei za kulanguliwa
sihitaji kuchunguza hapo
 
kwa kweli kinachotakiwa kufanyika sasa ni maandamano makubwa sana kwa kila mwananchi tupilia mbali chama chako, hao Chadema mbona hawasikiki sasa hivi???? nilikuwa nawategemea wataitisha mandamano ya nchi nzima. hadi kufikia leo hakuna dalili tunaendelea kuvumilia watu wanatuamulia kwenye nchi yetu hadi lini????? wananchi tuamkeni jamani tuingie mitaani, tuache porojo za akina jk
 
watanzania wenzangu tukubali au tukatae ila ukweli ni kwamba hii miaka 10 yaani toka 2005 - 2015 tumeingia mkenge in other words badala ya kusonga step forward sisi tunarudi nyuma at the same time raslimali zinaporwa na watanzania wanaoingia mikataba ya ulaghai na wageni. Ni yale yele tuliyosoma those days wakati mababu zetu walipewa shanga kubadilishana na almasi / dhahabu.

Tutaijutia sana hii miaka 10 tuliyoipoteza as a nation, na kizazi kijacho hakitatuelwa kabisa kwamba je tulitumia ubongo kufikiria au masaburi? nina majonzi sana na nchi yangu yaani mambo yahaendi kabisa kuna nini? ni nuksi nini?
 
Ole wao wanaotunga sheria zisizo za haki,watu wanaopitisha sheria za kukandamiza.Huwanyima maskini haki zao,na kuwaibia maskini wa watu wangu
maslahi yao.
Wajane wamekuwa nyara kwao;Yatima wamekuwa mawindo yao.
Je mtafanya nini siku ya adhabu,siku dhoruba itakapowajieni kutoka mbali?Mtamkimbilia nani kuomba msaada?Mtakwenda wapi kuweka mali yenu?
Litakalowabakia ni kujikunyata kati ya wafungwa na kuangamia pamoja na wanaouawa vitani.
Hata hivyo,hasira ya Mwenyezi Mungu haijatulia bado ameunyosha mkono wake.ISAYA 10:1-4
 
nina familly member wahindi na waarabu
na wao wengine wamepanga foleni za mafuta na wengine wamenunua kwa
bei za kulanguliwa
sihitaji kuchunguza hapo
good....
one down many to go
 
Kwa kweli there is no better way to explain shida za mafuta, umeme, nk.

Upande wa wafanyabiashara, wana hoja na zina mantiki... hasa kuhusu ulaghai!!
Upande wa serikali... tunasikia kujadili, kutoa notice etc.
upande wetu, hali mbaya sana... wapo wanaojifungulia njiani, wanakosa elimu, wanaokosa vipato nk

kinachoniudhi ni jinsi wahindi na waarabu ambavyo hadi sasa hawajaathirika... this just confirm kwamba wana mitandao na serikali zao ndani ya hii nhci na hawaathiriki kwa namna yoyote na janga hili.... THEY HAVE ESTABLISHED THEIR OWN FUEL SUPPLY SYSTEMS

SAD!!

Eeeeeeeeeeeh uwezi amini mvunja Nchi ni mwananchi mwenyewe,uwezi amini kuwa nilileta thread hapa siku kadha kabla ya issue ya mafuta haijawa kubwa.kuna wanaJF waliwatetea wahindi na waarabu hafadhari mdau umeliona hilo,nilisema Mataifa Matatu ndani ya Tanzania.Yanaani wamatumi,Wahindi na Waarbu.Mataifa mawali yaani Wahindi na Waarabu wako pamoja lakini Watanzania Wamatumi imekula kwao.

Niliwaambia wadau waangalie jambo hili kwa jicho la ndani kuna tatizo hapa kubwa sana na limechangiwa na Serikali yetu.Pia wano uwezo wa kulikomesha[Bofya Hapa]

Leo tena nimeandika thread wanaJF wajiulize kwani wale vijana wanaondesha uvunjaji wa maduka uingereza [Yob] ambao wana asili ya Wazungu na Waafrika ndio wanaondesha mtafaruku [Anarchy] mbona wanavamia maduka na makazi ya Wahindi.Imefikia hatua angalieni BBC mtawaona vijana wakihindi wakiwa kwenye vikundi kama ndio waathirika wa kipigo cha umma.Tafuteni kwenye google mtaona kuna mhinid kala kipondo toka kwa yob hao.Tujiukize kuna nini ndani ya matendo haya ya Vijana hawa wa kizungu na Kiafrika kuvamia Wahindi na shughuri zao.[Bofya Hapa].

Sipendi matendo ya hawa jamaa Wahindi na Waarabu kama tusipokuwa makini si muda mlefu Tanzania itakuwa kama Wingereza.Na kwa unafiki wa Waingereza hawataki kusema ukweli kuhusu vijana wa kiingereza wanafanya nini.Wameendesha propaganda kuwa ni wahuni.Wahuni gani wanao hama majiji kwa majiji na wanaopata kipondo hicho ni Wahindi pekee.

Tafakarini wana JF,Sio chuki lakini ndio ukweli,tuufike sehemu tuseme Wahindi na Waarabu basi.

Sooooooooooooooon and Very Soooooooooooooooon tena Sasa ni Very Sooooooooooooooon imeanzia tabata leo
 
Hebu elezea hiyo fuel supply system ya wahindi.
<br />
<br />
Nilikuwa mount meru filling station tabata, kuna foleni ya kufa mtu. Kitu cha ajabu ni kwamba wamesitisha zoezi la kuuza mafuta, wamesema hadi saa nane mchana lakini akija mdosi anapelekwa chemba anapata mafuta na kuondoka. Almanusura raia wameze mtu baada ya kugundua janja ya kuhudumia wadosi. Kwahiyo hawa wahindi na waarabu sio wenzetu!
 
Mbona huo ni mwanzo tu.bdo miaka4.
<br />
<br />
Biblia inajibu hivi, kwa maana siku hizo kutakuwa dhiki, jinsi isivyokuwa tangu mwanzo wa kuumba alipoumba Mungu hata sasa, wala haitakuwa kamwe. Soma Marko 13:19
 
Lazima turudi nyuma na kulaumu mfumo mzima wa kiutendaji, hasa kwa serikali kujitoa kabisa katika biashara, ingawa na ubinafsi wa watz wachache ulichangia sana!
 
vijana na watu wa makamo wote tumelala , tunashindwa hata wazee wa East Afrika angalau wamethubutu kufunga njia, hata police wanaweza kutuachia kidogo maana nao wengi wamo , kwani wale wenye daladala mbovu ni nani? au wenye vibajaj vya mikopo ni wakina nani si hawa mapolisi, tunakosa ushirikiana haya hayahusu CCM peke yake hata wa CCM wana hasira sana , mie kama mpanda basi mashuuri nchini kila si ukipanda wanaongelea wa kulianzisha, muhimu ni kuwaondoa wahindi na waarababu kwenye nyumba za NHC nao wakae mbali na Mji wajionee adha ya usafiri au wahamie USA, hawa ndio wanaotutesa. Angalia kama kuna mmiliki yoyote anakaa gongo la mboto, sana sana wanaishia upanga na Ocean Road , hawavuki mto wowote
 
Narudia tena na tena. Tanzania hiko ICU. Sasa na mitandao ya bank imegoma. CRDB hakuna internet banking tangu last week na wanasema hawajui itarudi lini. Nchi goodbye na bado miaka 4 na kitu.
 
CCM are stuck between a rock and a hard place. Most of oil business magnates are purpoted major party sponsors, and they played a great deal of contribution to put CCM into power. So how could CCM act senselessly and cut the hand that feeds them?

Once you are currupted, it is very difficult to make any rational decision
 
Habari za hali ngumu ya maisha..
Leo nimeenda dukani wadau nimeuziwa soda mia saba!juzi nimeinunua mia tano tu..eti achumi umepanda??mi sielewi kinachoendelea kabisa-elfu 10 siku hizi haisaidii chochote!mkate buku,sukari mmh-hata kiberiti jamani kimeguswa!
Nawaza-tangu jk aingie madarakani vitu vinazidi kupanda bei!hivi-ni macho yangu machanga ambayo hayaoni vizuri au JK anutupeleka kusiko??bado miaka minne amalize muda wake huyu mtaalamu wetu wa uchumi-si yatatukuta ya Zimbabwe??God help us ol..we have seen better dayz!
 
Kwakweli tumekuwa watumwa ndani ya nchi yetu. Matatizo kama haya sio mageni hapa duniani. Kuna mwanajursiprudensia mmoja alipata kunena kwamBa " Serikali ni mkataba kati ya watawala na watawaliwa" Hii inamaanisha kuwa uhusiano tulionao kati yetu na viongozi wetu ni mkataba kama mikataba mingine, Kama upande mmoja kati ya waliongia mkataba hautaridhishwa na mwenendo mbovu juu ya mkataba unaotendwa na upande wa pili wa aliyeingia mkataba, ni dhahiri kuwa upande uwo ambao hujaridhishwa na mkataba husika unaweza kuamua kuvunja mkataba uwo.
Kwa mwenendo wa serikali hii iliyopo madarakani imefikia hatua wananchi tunapaswa kuvunja nayo mkataba. Kwa tukio hili la janga la mafuta hapa nchini lililosababishwa na serikali dhidi ya wananchi wake, sisi wananchi tulitakiwa tushike mabango tuingie barabarani tukionyesha nia yakutaka kuvunja mkataba huu na serikali iliyopo madarakani.Hili janga la mafuta ni golden chance ambayo inatuwezesha wananchi kuamasisha serikali ijiengue kwa makosa inayofanya.
Watanzania tunahisia ya kumtoa mkoloni mweusi madarakani ila tunakuwa wanafki tunaishia kuongelea ili swala vyumbani mwetu. Swala la maandamano ya kuipinga serikali tusiwaachie vijana wetu wa sokoni na vijana wa vijiweni. Katika nchi mbalimbali ambazo wananchi wametimiza adhma yao kwa kutumia maandamano yamewajumuisha wakulima,wafanyabishara,wanavyuo,wafanya kazi ni wale wote wasio na kazi kwani wote hawa ndo waadhirika wa mfumo mbovu wa serikali. Watanzania tusiwe wanafki wala waoga na kuwaachia vijana wasio na kazi au wenye vipato vya chini pekee ndio washike mabango na kuandamana kupinga mfumo mbovu wa serikali yetu sote. Tuonyeshe kujitambua na kuionyesha serikali nia ya wazi ya kutokubaliana na mwenendo wake kwa kudai haki yetu ya msingi kwa njia ya maandamano kama mataifa mengine yalioonyesha utayari huu. Tunayoyasoma kwenye historia yasiishie kwenye vitabu tu, bali yatupe motisha wa kufanya yaliyofanywa na wenzetu waliotangulia kufanya. Tusione aibu kushika bango linaloonyesha haki ya msingi tunayoidai.
Hili ni janga la taifa zima kwa ujumla hatunabudi kuweka pembeni hisia zetu za vyama kwa kuzingatia ukweli na haki. Kwa pamoja tupaze sauti na kuikemea serikali pale inapokosea, Tukubali ukweli na kupingana na uongo, tuweke misimamo yetu ya kichama pembeni ili kwa pamoja tukatae giza na kukubali mwangaza. Tusigawanywe na vyama alafu tufumbwe na tupumbazwe ili tusiseme ukweli na kudai haki. Tukipaza sauti kwa pamoja pasipo kupumbazwa na hisia za kivyama hakika tutasika na mkoloni mweusi atadondoka pale anapotunyima tusulubu kwa mfumo mbaya wa uongozi.
Kenyatta mkubwa alishawai kumuambia Mwl Julius Kambarage Nyerere kuwa "Mwalimu unaongoza maiti" akiwa anamaanisha Watanzania wamepumbaa kiasi cha kupelekeshwa kwa namna yoyote viongozi wao watakavyoamua.
Tubadilike tufanye maamuzi magumu sote kwa pamoja tuseme ndio pale tunaporidhiswa na mfumo mzuri wa serikali, pia tupaze sauti kwa pamoja tuseme hapana pale ambapo hatutaridhishwa na mfumo mbovu wa serikali. Tusikubali tena kupoteza golden chance ya kuinyooshea serikali kidole kwa kuandamana tutakayoipata pale mfumo mbovu wa serikali utakapojitokeza.
TUAMKE USINGIZINI WATANZANIA.
 
Back
Top Bottom