Hali Mbaya kwa WaTZ wafanyabiashara nchini CHINA | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hali Mbaya kwa WaTZ wafanyabiashara nchini CHINA

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MaxShimba, Jun 12, 2012.

 1. MaxShimba

  MaxShimba JF-Expert Member

  #1
  Jun 12, 2012
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 35,816
  Likes Received: 129
  Trophy Points: 160
  [​IMG]

  HALI ya hatari imewazingira Watanzania walioko nchini China kwa biashara, baada ya Wachina kuanza tabia ya kuwadhulumu, kuwapiga na kuwapa mateso mbalimbali.

  Habari kutoka China, zilizojazwa nyama kwa picha za matukio ya Wabongo wakiloa damu kwa kichapo, zinaeleza kwamba jamaa hao wamegeuka waonevu wa kiwango cha juu kwa Watanzania.
  CHANZO CHA STORI

  Mtanzania, Bicklen Nazaleno Kibiki alipewa kichapo na Wachina waliomvamia hoteli aliyofikia kwenye Jiji la Guangzhou.
  Chanzo chetu kilisema: "Bila sababu, Wachina walimvamia huyu mwenzetu wakati anapandisha mizigo yake hotelini, wakampiga. Tulipompeleka Kibiki polisi kuripoti, tukageuziwa kibao, akaambiwa alipe faini.
  "Kuna Mtanzania mwingine mbali na huyu Kibiki, yeye alipigwa barabarani baada ya kwenda polisi, akalipishwa faini, bahati nzuri Waafrika wenzetu kutoka Nigeria, waliungana na sisi, tukamsaidia akatoka, amesharudi Tanzania na hataki tena kurudi China."
  WACHINA BWANA!

  Mtoa habari wetu alisema Wachina pia wamekuwa na tabia mbaya mno wanapokutana na Watanzania, akatoa mfano: "Mtanzania akienda saluni kunyoa, anaweza kuambiwa, mfano shilingi 10,000 lakini akishamaliza, anaambiwa shilingi 20,000.
  "Hapo ni lazima ulipe hiyo pesa, vinginevyo utapigwa na ukienda polisi utageuziwa kibao. Hawa watu wakiwa kwao ni wakatili sana, lakini sisi kwetu tunaishi nao vizuri."
  USHUHUDA MWINGINE
  Mtanzania Jas au maarufu kama Mchungaji ambaye kwa sasa yupo hapa nchini, alimueleza ripota wetu: "Nilikaa China kwa miezi minane nikiwa nafanya kazi zangu kwa usalama. Nilipokamilisha mizigo yangu wakati nataka kurudi Bongo nilivamiwa na Wachina.

  "Ilikuwa hivi, wakati nashusha mizigo kwa kutumia toroli la Hoteli ya Dong Feng ambayo ndiyo nilikuwa naishi pale Guangzhou, alitokea Mchina akaanza kutupa mizigo yangu. Nikamuuliza kwa nini anafanya hivyo, akanijibu tenda ya kushusha mizigo hotelini ni yake, kwa hiyo lazima nimlipe pesa.

  "Tukaanza kubishana, kwani siyo lazima kumlipa yeye pesa ukizingatia, nikitumia toroli la hoteli, silipii hata shilingi moja. Wakati tunabishana, wakatokea wenzake wakaanza kunipiga. Nikiwa nimejeruhiwa, tulikwenda hospitali, huko nikaambiwa nilipe faini vinginevyo viza yangu itafungwa.

  "Ikabidi nitoe dola 600 (zaidi ya shilingi 900,000) kuwalipa wale Wachina. Hii ndiyo hali halisi, bila kutafuna maneno ni kwamba Wachina wakiwa kule kwao wanawatesa Watanzania na polisi wa kule muda wote wanawalinda.
  "WABONGO WALA KICHAPO CHINA


   
 2. Big One

  Big One JF-Expert Member

  #2
  Jun 12, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 759
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  da polen sna wafanyabiashara yanayowakuta kwel ndugu zetu wakienda kule wanakuwa uwanja wa ugenini pole zao
   
 3. Watu8

  Watu8 JF-Expert Member

  #3
  Jun 12, 2012
  Joined: Feb 19, 2010
  Messages: 47,319
  Likes Received: 2,605
  Trophy Points: 280
  Tatizo lenu mkija huku mnataka mhandle kila kitu maana hamtaki kutupa madeal ndugu zenu tunaoishi huku...Sasa kweli hapo Dong Feng upigwe wakati ndio mitaa ya nyumbani ya Waafrika loh!
  Ukweli ni kwamba Wachina ni wakatili na msipokuwa makini wataanza kuwachinja na kuwaskin mkiwa hai...yinwei tamen shi zhongguo ren haishi zanmen shi hei ren..
   
 4. Mamndenyi

  Mamndenyi JF-Expert Member

  #4
  Jun 12, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 29,060
  Likes Received: 6,509
  Trophy Points: 280
  Tuwachape na wao mbona wamejaa huko kariakoo.
   
 5. K

  Kiumbo JF-Expert Member

  #5
  Jun 12, 2012
  Joined: Feb 4, 2012
  Messages: 561
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Duuu hiii mbaya kweli lazima itafutuwe ufumbuzi maana wafanyabiashara wa bongo. Kiama.
   
 6. kimpe

  kimpe JF-Expert Member

  #6
  Jun 12, 2012
  Joined: Jan 26, 2012
  Messages: 745
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 80
  hebu sema hulipishwa fine ya nini baada ya kupigwa
   
 7. S

  Same ORG JF-Expert Member

  #7
  Jun 12, 2012
  Joined: Jun 10, 2012
  Messages: 323
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  jamani nyinyi wabongo hawa wachina mumeshawaua mara ngapi kwa ujambazi hapa kwenu? tabia zenu pia mbaya mkiwa kwenu musilalamike jambo dogo linawatoa roho punguzeni wizi. vinginevo baadae mutashindwa kusafiri ukionekana tu na paspot ya tz unarejeshwa. mnadhalilisha, mnawauwa wageni, na nyie mutatendwa.
   
 8. kichwat

  kichwat JF-Expert Member

  #8
  Jun 12, 2012
  Joined: Mar 4, 2010
  Messages: 1,824
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  Nachojua Tanzania ina ofisi kubwa ya UBALOZI huko China, nadhani hii imo ndani ya uwezo wao, na hata kutoa tamko kuhusu ukweli wake na hali halisi. Vinginevyo matukio haya yanaweza kuwakumba wale tu wanaoenda kinyemela, na aghalabu kwa malengo 'mixed'.
   
 9. Ulukolokwitanga

  Ulukolokwitanga JF-Expert Member

  #9
  Jun 12, 2012
  Joined: Sep 18, 2010
  Messages: 8,418
  Likes Received: 3,905
  Trophy Points: 280
  Tumkamate mmoja tumle tigo halafu aende akasimulie kule kwao nao waanze kutuogopa maana wanajua kuwa sisi kun fu haipandi
   
 10. F

  FJM JF-Expert Member

  #10
  Jun 12, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Taarifa za waafrika wakiwemo watanzania kuvamiwa na kupigwa vibaya na wachina wakiwa nchini china zinaongezeka kila siku. Kuna tatizo la ubaguzi ambalo wakubwa wa China hawajakubali kuliangalia. Ajabu ni kwamba China inakomba kwa serikali za Afrika kwa sababu ya raw material. Muda sasa umefika kuwaambia ukweli officials toka china.

  Viongozi wetu wanaweza kwana kuongea na ubalozi wa china hapa nchini, lakini pia ningependa kuona AU ikiongea hili jambo maana kuna udhalilishwaji mkubwa wa mwafrika huko China.
   
 11. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #11
  Jun 12, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Kumbukeni kuwa kama hiyo chuki imeanza sasa, ni baada ya Mchina kuuliwa hapa Dar. Mmesha sahau?
   
 12. F

  FJM JF-Expert Member

  #12
  Jun 12, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  zomba, haya matukio yamekuwepo muda mrefu kabla hata ya mkasa wa mchina hapa Dar. Waafrika wanadhalilishwa sana China. Ukienda police ndio utaona madharau na ubaguzi wa wachina.
   
 13. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #13
  Jun 12, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Siyo huko tu, hata hapa wameshawapiga watu sana, kuna habari nilisoma washamkandika makofi mpaka mkuu wa kituo cha polisi. Lakini bado tunawakumbatia tu.
   
 14. F

  FJM JF-Expert Member

  #14
  Jun 12, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Ukweli wanatia kinyaa. Halafu ukiwa mitaani huko kwao wakijua unatoka Tanzania utasikia wanasema 'Tanzania good!!. Nadhani walishaambizana hapa ni mteremko.
   
 15. Davie S.M

  Davie S.M JF-Expert Member

  #15
  Jun 13, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 720
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 35
  Wabongo Kupigwa ? Hata sishangai...kwanza utapigajwe bila sababu Haiingii akilini ...ishu ni kwamba wabongo maarifa mengi tunapenda ku-bypass tukishajua vichochoro tu baasi...ukijifanya mjuaji wacha ubondwe...hata huku wanaibiwa,wanapigwa risasi,wanadhurumiwa ndo maana wapo makini sasa

  Sent from my BlackBerry 9900 using JamiiForums
   
 16. Globu

  Globu JF-Expert Member

  #16
  Jun 13, 2012
  Joined: Jan 12, 2011
  Messages: 7,975
  Likes Received: 175
  Trophy Points: 160
  Ni kweli kabisa kuhusu unyanyasaji wa sisi WaAfrika. Binafsi yalishawahi kunikuta nikiwa HONGKONG.
   
 17. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #17
  Jun 13, 2012
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,489
  Likes Received: 81,786
  Trophy Points: 280
  Mie kwa maoni yangu tafuteni nchi nyingine za kwenda kufanya biashara au kama mnaenda kuchukua mali basi mwende nchi nyingine ambazo mtakuwa na uhakika wa uhai/usalama wenu kama wafanyabiashara badala ya kwenda China. Kule sasa hivi pia umeingia mtindo wa kuwakamata weusi na kwenda kuvuna organs mbali mbali ambazo zinauzwa kwa bei ya juu sana.
   
 18. Jidu

  Jidu JF-Expert Member

  #18
  Jun 13, 2012
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 1,167
  Likes Received: 302
  Trophy Points: 180
  Mwe!duo xie!
   
 19. denoo49

  denoo49 JF-Expert Member

  #19
  Jun 13, 2012
  Joined: Mar 29, 2011
  Messages: 5,647
  Likes Received: 5,240
  Trophy Points: 280
  kidogo hili litapunguza idadi ya kutuletea bidhaa feki huku kwetu. Maana asilimia kubwa ya wafanyabiashara wa kibongo wanaoenda china husukumwa na tamaa bila kujali utu wa wenzao walio waacha tz kwa kuwaletea bidhaa feki.
   
 20. RRONDO

  RRONDO JF-Expert Member

  #20
  Jun 13, 2012
  Joined: Jan 3, 2010
  Messages: 25,796
  Likes Received: 20,748
  Trophy Points: 280
  Endeleeni kumkumbatia Mchina soon hayo wanayowafanyia huko kwao watakuja kuwafanya hapa hapa kwenu...Y'ALL GONNA SPEAK CHINESE!
   
Loading...