Hali itakuwaje mtaani wakifukuzwa maaskari wenye vyeti visivyokuwa vyao?

The Listener

JF-Expert Member
Feb 5, 2012
993
213
Kutokana na kanuni za Utumishi wa Umma kutumia mbinu yoyote ya ulaghai ni kosa. Zoezi la Kutengeneza vitambulisho vya utaifa limezaa scandal japo ni kwa sehemu ndogo tu ya watumishi wa Serikali. Kada ya uaskari ni nyeti sana katika nchi yetu. Kama askari polisi 700 na wanajeshi 248 wamekutwa na matumizi ya majina ya watu wengine ambao hatuna uhakika hata baadhi yao kuwa bado wako hai au la. Nisaidieni kujua wana jamii kama watumishi hawa kwa mujibu wa taratibu wanaweza kupewa adhabu inayoweza kufikia kufukuzwa kazi? Mimi nauliza hivi nikiwa na hofu kubwa kwamba kundi hili (ambalo ni la hapa DSM tu) likifukuzwa kazi huko mtaani kutakuwaje.
 
Hapo tufanye tu Kama kristo alivyosema sisi wote tume tenda dhambi na tumepungukiwa na utukufu wa mungu(we are all sinners and we have fall short of glory of Gods)maana bila kufanya hivyo itkuwa ni kazi kweli kweli lakini haina maanishi tuendelee kuvivumilia vitendo hivyo
:glasses-nerdy::boxing:
 
Hakuna kufumba macho hapa, hao watu takribani 1,000 wameziba riziki za wenye vigezo ambao walistahili nafasi ambazo wao wameghushi kuzipata. Nategemea NIDA wataendelea kuwaumbua wengine wengi tu. WAFUKUZWE! Sheria msumeno.
 
...sina uhakika juu ya kufukuzwa kwao.
Japo sheria inasema hivyo, mtaani wataongeza majambazi wenye taaluma.
 
Ndiyo maana hawana uelewa,utu na uchungu wa hii nchi,wakati wa kudai haki wao kukupiga risasi ni sawa na kukuchana kiwembe,kweli kilio cha watz kimesikika,waende tu
 
Kutokana na kanuni za Utumishi wa Umma kutumia mbinu yoyote ya ulaghai ni kosa. Zoezi la Kutengeneza vitambulisho vya utaifa limezaa scandal japo ni kwa sehemu ndogo tu ya watumishi wa Serikali. Kada ya uaskari ni nyeti sana katika nchi yetu. Kama askari polisi 700 na wanajeshi 248 wamekutwa na matumizi ya majina ya watu wengine ambao hatuna uhakika hata baadhi yao kuwa bado wako hai au la. Nisaidieni kujua wana jamii kama watumishi hawa kwa mujibu wa taratibu wanaweza kupewa adhabu inayoweza kufikia kufukuzwa kazi? Mimi nauliza hivi nikiwa na hofu kubwa kwamba kundi hili (ambalo ni la hapa DSM tu) likifukuzwa kazi huko mtaani kutakuwaje.

Hii cha mtoto bado uozo haujawekwa wazi! watakapoingia wizara ya elimu walimu wa shule ya msingi na sekondari watanaswa kibao, manesi huko usipime ni kundi kubwa sana, wataalam wa kilimo ngazi ya certificate na diploma acha kabisa. masecretary pia wapo kibao tena hadi ofisi nyeti kama mawizara na idara za serikali. Hapa ni sawa na kumwomba daktari ashone jipu. Hiki ni kizaza! BIG UP NIDA!
 
Back
Top Bottom