barafu
JF-Expert Member
- Apr 28, 2013
- 6,739
- 32,958
Ni fedheha sana kuwa muumini wa uwongo…ni fahari kwa mwanadamu kuusimamia kweli…tunu ya ukweli na haki ni heshima!!! Nimefadhaika sana na vijana wanaotumia jukwaa hili kuwasemea watu wa Isimani, watu wanaoishi ktk mazingira magumu ya umasikini kisa tu ni sera mbovu ya Chama Tawala…kwa mtu aliyepata kutembelea Jimbo la Isimani atakubaliana nami kuwa kati ya majimbo yenye watu masikini Tanzania hii basi ni Isimani…Jimbo lisilowahi hata kutamkwa Bungeni katika mijadala ya maana,watu wake hawana msemaji..wanakufa kwa uhaba wa maji na huduma bora za afya.
Ukitembelea Jimbo loooote la Isimani huduma ya maji ni shida sana,watu wanakunywa matope na sio maji,huduma ya maji ktk eneo hili ni duni duni isivyo kawaida.Anaepiga zumari kuwa Fulani kaleta maendeleo atapata laana.
Bila kuwa na hiyana,katika eneo lote la JImbo la Isimani Serikali haijawahi kupeleka mradi wa maana..miradi yote mikubwa ya kimaendeleo ktk eneo hilli imeletwa na mashirika ya dini,na hasa wamisionary wa kanisa katoliki..shule zilizojengwa zimejengwa na kanisa,vituo vya afya na visima vya maji ni kazi ya masirika ya dina…unaweza kudiliki kusema kuwa "mbunge" wa jimbo hili ni mashirika ya dini
Mbunge huja uchaguzi mpaka uchaguzi…hakuna juhudi zinazofanywa na mbunge kuleta miradi ya maendeleo….mradi mkubwa wa maji ktk eneo la tarafa ya Isimani unafadhiliwa na wamisionary toka Italy ambao wamekuwapo hapo toka miaka ya 70.eneo la Pawaga linafaidika na uwepo wa mpaka na Mbuga ya Ruaha,hivyo TANAPA kupitia MBOMIPA hutoa misaada ya kimaendeleo ili kudumisha ujirani mwema,huku Migoli huduma za afya,maji na elimu ni kazi za mashirika ya dini…na ndio maana eneo hili wamisionary ndio kila kitu…Kwa kifupi nina data za kutosha zinazoonyesha kuwa eneo hili serikali haijawahi kupeleka mradi wowote na kufanya serikali kuwa kama haipo.
Kielimu watu wa eneo hili wako chini chini sana,hata kaika uchaguzi wa 2010 Chadema ilisimamisha mtu kutoka Iringa mjini,maana wazawa hakuna,,,hata huyo Dr.Kapwani alilubuniwa na hatimaye siku ya krudisha form alijichelewesha mpaka mda ukapita…Hili dalili za watu kutumwa humu waje wajifie ni kuwa Upinzani sasa umeimalika…nenda Pawaga, Idodi,Isimani, Izazi na Migoli…Chadema inashika kasi sana…Watu hawa wanahitaji kusaidiwa, wanaishi ktk umasikini wa hali ya juu,njaa kila mwaka, huduma mbovu za afya na maji…Viongozi wa kitaifa Chadema tembeleeni Isimani..
Vijana wamejenga Ofisi za Chama kwa kujichangisha..nendeni mkawape moyo..huu ujio wa watu humu kujipa" Promo" ni tayali wameona moto uko juuu…mfike mkawape moyo vijana...Jimbo la Isimani ni kama YATIMA...Wananchi wake hawajawahi kusikia katika mijadala ya Bunge jina la jimbo lao kutajwa...hawana msemaji...
Wasaisieni ili kilio cha shida na matatizo yao kiwe masikioni mwa serikali....Wamechoka kuendesha maisha kwa kutegemea misaada na hisaani za masirika ya dini..chonde chonde nao wanataka mabadiliko(jengo la ofisi za chama vijana wamejitolea kutengeneza BILA KUSHURUTISHWA)