Sio kila kitu serikali ifanye direct, haya mashirika ya dini yanawezeshwa kiasi fulani na sera za nchi ili ziweze kusaidiana nazo katika kutoa huduma za kijamii, kwa mfano kutoa misamaha ya kodi, ruzuku (hospitali zinazomilikiwa na taasisi za kidini na NGOs). Hii ni kwa sababu serikali haina rasilimali za kutosha.
Watanzania tunahadaiwa na wanasiasa (CCM, CDM,CUF, nk) kwa ahadi ambazo hazitekelezeki kwa muda mfupi. Hata iweje, nchi nzima haiwezi kupata huduma za maji, umeme, matibabu, barabara, shule bora kwa wakati mmoja, maeneo mengine lazima waumie kidogo, ndio maana kunakuwepo na mipango mikakati (muda mrefu na mfupi). Tunachotakiwa kupigania ni mgawanyo sahihi wa rasilimali badala ya kuelekezwa katika maeneo machache ya nchi.