Hali bado Ngumu sekta ya Afya, Temeke wagonjwa walala Chini!

Barbarosa

JF-Expert Member
Apr 16, 2015
22,584
27,811
Hiyo picha ni leo hii Hospitalini Temeke ambapo kama inavyoonekana tatizo siyo vitanda bali tatizo ni nafasi ya kuweka vitanda, kuna wagonjwa wengi klk nafasi, hivyo wito wangu kwetu Watz hali inaweza tu kupungua kama tukizingatia uzazi wa mpango na tupunguze kuzaa sana, hakuna njia nyingine ni lazima tulifanye hili!

Serikali iwagawie vidonge vya kuzuia Mimba wasichana wote waliofikisha Umri wa kuweza kujamiiana, bila kufanya hivyo tutakuwa tunatwangia maji kwenye kinu kwani hata kama tukijenga Hospitali nyingine haitasaidia kwani kasi ya ongezeko la watu ni kubwa sana kwa wastani kila Mwanamke TanZania anapata watoto 5.6 sasa hii idadi kubwa sana na ni lazima tuipunguze!

Tanzania_mothers_459847artw.jpg
 
Hivi wewe akili zako zinakutosha au? Wewe hujui kama Hospitali ya temeke ni "Muhimbili" ya temeke, kigamboni, mbagala, rufiji, kisiju nk? Tujenge na tuziimarishe hospitali za pembezoni ili tuweze kuyadhibiti magonjwa madogomadogo hukohuko; wagonjwa isiwe kila kitu temeke, Amana au Muhimbili. Dunia hairudi nyuma dada, usijidanganye.
 
Kuna tofauti kati ya "kusikitishwa" na wagonjwa kulala chini ukatoa "amri" ya papo kwa papo vitanda vinunuliwe viwekwe haraka , au jengo fulani libadirishwe matumizi NA Kuyachukua matatizo ukaita wadau, ukataka waje na utafiti wa tatizo liko wapi katika hospitali za nchi nzima, ukaunda chombo cha kusimamia ubora wa huduma za serikali, ukatenga bajeti, vitu vikanunuliwa , halafu Vikasambazwa hospitali zote nchini iwe ni kwa awamu au mkupuo!. Otherwise leo utasolve tatizo la wagonjwa kulala chini katika wodi ya Wazazi halafu kumbe mita kadhaa kwenye wodi ya vichaa nao tatizo liko!
 
Wakishindwa changamoto au pale ubunifu wao unapoisha hizi ndio uwa kauli zao za mwisho madharau watu wapewe vidonge wasizae, omba omba wawekwe kwenye malori warudishwe walipotoka au kutoa lawana na kufukuza watu kwa huduma hafifu wakati budget yenyewe waliyowapa ya mwezi mmoja wao wanataka itumike kwa miezi mitatu; hawa ndio viongozi wa Tanzania ya leo.
 
Hiyo picha ni leo hii Hospitalini Temeke ambapo kama inavyoonekana tatizo siyo vitanda bali tatizo ni nafasi ya kuweka vitanda, kuna wagonjwa wengi klk nafasi, hivyo wito wangu kwetu Watz hali inaweza tu kupungua kama tukizingatia uzazi wa mpango na tupunguze kuzaa sana, hakuna njia nyingine ni lazima tulifanye hili!

Serikali iwagawie vidonge vya kuzuia Mimba wasichana wote waliofikisha Umri wa kuweza kujamiiana, bila kufanya hivyo tutakuwa tunatwangia maji kwenye kinu kwani hata kama tukijenga Hospitali nyingine haitasaidia kwani kasi ya ongezeko la watu ni kubwa sana kwa wastani kila Mwanamke TanZania anapata watoto 5.6 sasa hii idadi kubwa sana na ni lazima tuipunguze!

Tanzania_mothers_459847artw.jpg
wewe ni mnafiki tena mnafiki mkubwa hapo kwenye vitanda wako wawili wawili na sio kwamba tatizo ni majengo na vitanda pia ni tatizo sasa nakushauri wewe na wanafiki wenzio mkimaliza msimu wa kusifia muanze kumwambia jpm kwamba kuna hospital zetu nyingi tu zinahitaji kuboreshwa mfano temeke inakusanya wagonjwa mpaka mkuranga na ilala pia inakusanya mpaka mvuti na idadi ya wagonjwa ni wengi.
ila kwa sababu ya ufinyu wa mawazo ya watu wa lumunba ni kusifia tu.
amtaki kuambiwa ukweli
 
Hata kama Serikali ikijenga Hospitali kama Temeke nyingine 10 ndani ya Dar bado kwa kasi hii ya ongezeko la watu yaani watoto 5.6 kwa kila Mwanamke baada ya miaka 5 hali itakuwa kama ilivyo leo kwa maana tunaongezeka kwa kasi kubwa sana na ongezeko letu haliendani na kasi ya ukuaji wa uchumi wetu hivyo kama kweli tunataka kutatua hili tatizo ni lazima Wasichana wapewe vidonge vya kuzuia Mimba mpaka wafikie muda ambao watakuwa tayari kuwa na mtoto na siye kila msichana anayelala na Mwanaume aruhusiwe kuleta mtoto Duniani!
 
pole kwa mawazo yako finyu.
kwa sasa idadi ya wajawazito imepungua tofauti na miaka iliyopita tatizo lililopo ni kwamba tunaangalia hospital za mjini tu na kusahau za vijijini na ndio maana wagonjwa wote wanakimbilia hospital za mjini
 
Suluhisho alilotoa mwanzisha mada ni afadhali na Makonda kuratibu walimu wapande daladala bure.
 
Back
Top Bottom