Mhaya
JF-Expert Member
- Aug 20, 2023
- 1,826
- 5,454
Anayekwambia ukweli, jua anataka upone. Maisha yetu yameandamwa sana na siasa kiasi kwamba sasa hata vitabu vya dini tunavipiga teke. Ndiyo! Tunataka kila mtu apewe usawa, watu wote wawe sawa kwenye nyanja mbalimbali.
Lakini ukweli ni kwamba, anguko kubwa la mwanaume linaanzia kwa mwanamke. Angalia hata kwenye Biblia, soma tu; watu wenye nguvu waliangushwa na nani? Samsoni, Sulemani. Mambo haya tusiyape kisiasa, tuyachukulie jinsi yalivyo.
Siku hizi, wanawake hawataki kuwa wasaidizi; wanataka kuwa vichwa. Mwanamke anataka akuongoze kwa sababu tu ana pesa. Pesa haikufanyi kuwa mkubwa. Unaweza kuwa na pesa nyingi, lakini bado utampa heshima baba yako. Leo hii, mwanamke akiwa na pesa zaidi ya mume, mwanaume anaonekana kituko. Ama hii haipo?
Biblia imeandika: ishini na wanawake kwa akili. Kama hauna akili, usiishi na mwanamke hata kidogo. Wanawake wanaibuka na kujazwa fikra kwamba wao ni sawa na wanaume. Wanaleta usawa, lakini huo usawa ni kwenye baadhi ya mambo, si kwenye kila kitu. Usawa haupo kwenye kuhudumia familia, lakini wanataka usawa kwenye ufanyaji kazi.
Ukiwa na pesa, tafuta mwanamke ambaye unaamini hata akipata pesa hatoota mapembe. Wanawake wa aina hiyo ni mmoja kati ya kumi unaowaona njiani. Ndiyo maana mwanamke akipata pesa, anafikiria kuzaa mtoto ili aishi maisha yake peke yake, lakini mwanaume akipata pesa, anafikiria kuoa kwa kuwa anaamini bila mwanamke, hana msaidizi. Mwanamke akipata pesa, anaamini anaweza kuishi peke yake bila kiongozi.
Ndugu zangu, mwanamke hata ukiwa na pesa zote duniani bado utahitaji uwepo wa mwanaume kukuongoza. Hapa duniani hakuna mwanamke anayeweza kujiongoza peke yake—nasema hakuna. Kila mmoja anahitaji kuongozwa na mwanaume, ndiyo maana mwanaume amechaguliwa kuwa kiongozi wa familia. Hata uwe na mapesa, kama umeolewa, hautoitwa kichwa cha familia. Mungu aliyetuumba anatujua sana; anajua mwanaume bila msaidizi hawezi, na mwanamke anahitaji kiongozi.
Roho za kishetani ndizo zinaongoza dunia hii na kutaka kupinga ukweli wa Mungu. Niliwahi kusema kwamba sasa watu wanajaribu kwa kila njia kuhakikisha mpango wa Mungu unatoweka, ndiyo maana wanakuja na hoja za usawa wa haki. Mwanamke na mwanaume wawe sawa, huu ni mpango wa shetani. Mungu hakutaka iwe hivyo kwa sababu anajua alivyoumba viumbe hawa wawili. Kutaka usawa wa haki ni kuungana na mpango wa kishetani na kuzifuata roho za shetani kukuongoza.
Mwanaume anaweza kufanikiwa bila mwanamke kwa sababu Mungu kampa nguvu na maarifa makubwa, lakini anapofanikiwa anamuhitaji mwanamke kwa ajili ya kumpa faraja, kumpumzisha baada ya mihangaiko mingi. Hata hivyo, hamuhitaji ili afanikiwe; nguvu alizopewa na Mungu zinatosha kumfanya awe tajiri. Mpango wa Mungu ni wewe kuwa chini ya mwanaume, lakini mpango wa shetani ni mwanamke kujiona ana nguvu sawa na mwanaume.
Kama una mwanamke ambaye amefanikiwa na bado akawa mnyenyekevu kwa mumewe, huyo anastahili maua yake. Mafanikio yakianza kumjia mwanamke, kama ni pesa, huona ni zake na za mtoto pekee, si za mwanaume. Kesho atasimama na kudai usawa. Mwanamke kuwa mnyenyekevu akiwa na kipato kikubwa kuliko mumewe inahitaji sana hofu ya Mungu.
Utabisha, lakini tunayaona mitaani. Ama kama unaishi mbinguni. Dada zangu, kuwa wanyenyekevu. Nyenyekeeni na muoneshe kwamba ninyi ni wasaidizi wa mwanaume. Mungu alitaka iwe hivyo. Achana na wapuuzi wanaokutaka uwe juu ya mwanaume au sawa naye. Mungu hakutaka hivyo. Ama kama unapingana na Mungu, endelea kudai usawa. Maana dunia ya sasa hivi, watu wanaanza kuona Mungu si lolote wala chochote.