Hakuna "wawekezaji" wanaotetewa kimagumashi kama kampuni za simu

njaakalihatari

JF-Expert Member
Feb 12, 2019
4,084
8,663
Nina hakika hata wenyewe wanashangaa hawana mikimikimikiki yoyote hawa jamaa wanaweza wakaamka kesho wakasema tshs 5000 unapata data ya mb 80 na wasifanywe kitu

Sanasana watu wakilalamika wataambiwa nyie hamjui kutumia simu zenu kuna APPS zinakula data, mara Tanzania ni ya sita afrika kwa kuwa na bei nafuu ya bando..Godamn it. wakipiga kelele sana kuna waziri huyo atawachamba hadi wakome kijeuri kabisa kaamua kuwapuuza

Mbaya zaidi ukiangalia kwa karibu sana hawa jamaa ni kama CARTEL wanapandisha bei kwa pamoja na kwa uwiano unaofaana ili ikitokea mtu akadhani anakimbilia mtandao mwingine akate tamaa, maana kuna kipindi ilikuwa inaonekana halotel ni nafuu watu wakakimbilia huko ila kwa sasa hakuna tofauti kabisa sijui ile FCC ina faida gani sasa

HONGERA WAZIRI NAPE NNAUYE NGUVU INAYOTUMIKA KUWATETEA HAWA WANYONYAJI NA WEZI WA DATA SIYO YA KAWAIDA, bei juu na hata ukifunga macho ulipie baada ya dakika kumi unasikia sms umetumia aslimia 75
 
Mkuu kiukweli Tanzania bando ni bei rahisi haswa..tembea uone mwenyewe...
 
Mkuu kuhusu MB ni serikali ndio imepandisha Bei elekezi kwa hiyo hizo Bei mpya ni sawa tu mfano Mb 1 ni Tsh 10 Ina maana kihalalali kabisa wanapaswa WAKUPE MB 50 kwa Jero ila unakuta wanauza mpaka Sh 4 Kwa MB moja.

Ukitaka kujua Jinsi hili kasome miongozo ipo website ya TCRA utagundua Halotel inauza MB chini ya Bei elekezi!! Kwahiyo wakulaumu ni serikali ikipunguza makodi kwenye hizo bundle sidhani kama MB zitakua na gharama.

Kuhusu kuisha haraka ni sababu hiyo hiyo wanaweza kukupa Data nyingi ila wanapunguza bandwidth Ili iwe slow au Wanaikuza spidi Ili wazimalize haraka!! Ni mbinu tu Ili ununue vocha zaidi wafidie makodi Yao!
 
Huko Halotel ndo pa kuhamia, Tigo leo wamenikatia bando saizi yako nilikuwa napata MB900 kwa tsh 1500 leo nimepewa MB750. Zinashuka tu maana mwanzo ilikuwa G1 ikaja MB900 leo MB750 kesho nimepanga wanipe MB500 nihamie Halotel
 
Nani wa kuwafokea hawa watu wa mitandao? Hajipendi huyo mtu? Waziri nayehusika akithubutu atateuliwa kuwa DAS wa wilaya ya Nsimbo kule mkoa wa Katavi

Nchi ngumu hii
 
Back
Top Bottom