Hakuna watu limbukeni kama baadhi ya mama lishe

kinyamkela mahaba

JF-Expert Member
May 4, 2022
1,181
1,574
Haya wengi wao ni wajinga mno na limbukeni, wanadharau mno za chini chini wakati wana shida. Ni leo asubuhi nimeamka safi tu, nimepiga 'jogging' nimeoga, sasa ile saa 4 nakwenda kupata japo supu ndipo haya yaliponitokea.

Niliagiza vitumbua vya 2000 nikawa nakula viwili viwili kwa wakati, nikamaliza nikaagiza supu ya 4000 ya kongoro na nikashushia uji wa ulezi wa 1000. Sasa nasubiri chenchi yangu nao wananiangalia tu ilhali chakula nishamaliza kula, yaani tunaangaliana tu bila sababu.

Ghafla naona amezubaa, anakonyezana na wenzake kwa siri kisha kama wanateta. Ni utaratibu mbovu, mteja anaweza hisi hata mnapanga njama za kumuua.

Pia siyo lazima wakati mteja anakula naye anakaa hapo hapo mnaangaliana, huu ni ujinga. Mteja akila we' toka na upotee. DSM imeshamiri sana hii.

Badilikeni, acheni kuingilia faragha za wateja wenu.
 
Haya mengi yao nimajinga mno na malimbukeni.wanadharau mno za chini chini wakati wanashida, ni leo asubuhi nimeamka safi tu,nimepiga jogging nimeoga, sasa ile saa 4 nakwenda kupata japo supu ndipo haya yaliponitokea...
Kakunyima namba umekuja kumpaka humu🤣
 
Back
Top Bottom