Nguvu za kiume na uwezo wa mwanaume kumtungisha mwanamke mimba ni vitu viwili tofauti...mwanaume anaweza akawa rijali kweli, mtarimbo unasimama, una nguvu, na anaenda round kadhaa, lakini manii anayotoa haina mbegu (sperm cells) za kutosha, au ni dhaifu, na hivyo hatungishi mimba. Na hili ndio tatizo kwa wanaume wengi ambao hawana uwezo wa kutungisha mimba. Tatizo huwa sio kusimamisha au kumudu round kadhaa za mechi.
Kama unaongelea uzazi kwa ujumla ni wigo mpana sana...sio wanaume tu! Mwanaume anaweza akawa hana tatizo, lakini mwanamke ana tatizo labda la kuzalishwa kwa mayai kwenye ovaries, au mayai yake ni dhaifu hata yakirutubishwa, au mirija ya mayai (fallopian tubes) imeziba, au kizazi chake (uterus) hakiwezi shikilia yai lililorutubishwa (implantation).
Ukiachilia matatizo hayo kwa mwanaume au mwanamke...siku hizi kampeni za uzazi wa mpango zimefika (naweza sema) kila sehemu, na uelewa wa watu unaongezeka kila kukicha, na hivyo kupunguza kuzaa, na hii aoutomatically inapunguza kuzaa watoto wengi (nadhani hii ndio sababu kuu). Miaka 10 iliyopita ilikuwa ni kawaida mwanamke kuwa na watoto 6, 7, 8 au hata 10....siku hizi hata vijijini hali si hiyo, na hilo linahusiana zaidi na uzazi wa mpango kuliko 'kungukiwa nguvu za kiume'!