Hakuna taka ofisini kwangu.. Kwanini wananidai hela???

Hakuna taka ofisini kwangu.. Kwanini wananidai hela???

Watanzania jifunzen kuchangia maendeleo ya mitaa yenu bila kulalamika,shiling 5000 tu unakuja jf we ukikutana na matatizo ya kufilisiwa si utajinyonga kbs!
 
Ungesoma sheria zilikupa leseni nafikiri hayo mambo ya kulipia taka yalikuwepo.
Unapokuwa kwenye eneo ambalo watu wengine wanalipia taka,kulingana na sheria ya eneo husika, basi inakubidi nawe ulipie tu hata kama uzalishi hizo taka ili kuepuka usumbufu na faini zisizo za lazima
 
Suala La kulipia Taka lipo kisheria huku mtaani kwetu tunalipa elfu kumi kwa mwezi na usafi kweli unafanyika pia kumbuka wanafanya kazi hii wanatakiwa kulipwa mishahara maana Kuna wanaofagia na wanaozoa katika maisha ya sasa lazima tugawane fursa usigome kulipa weka jiji lako safi kama ujachafua ww atachafua Mteja wako ndugu yako mgeni wako anayekuja eneo la biashara yako
 
Pole sana...

Sheria zipo ila mambo mengine inatakiwa binadamu mwenyewe atumie utashi wake... hilo hawatumii ni kama marobot...

Nadhani watakua wanakutoza taka unazozalisha tumboni...


Cc: mahondaw
 
Wakuu

Mimi ni mfanya biashara.. Nina fremu nimekodisha kwaajili ya mambo ya mihamala ya mitandao (tigo pesa, mpesa n.k)
Hakuna ninachofanya zaidi ya mihamala... Hivyo sizalishi taka yoyote zaidi tuu huwa nafagiaga mchanga unaoletwa na baadhi ya wateja

Sasa kuna mtu kutoka serikalini(kwa afisa mtendaji Kata ) huwa anapita kukusanya pesa ya taka taka na hajawahi kubeba takataka yoyote kutoka kwenye hii fremu.. Kila mwisho wa mwezi nampatia shilingi elfu 5

Je, nisahihi kwa wao kuchukua fedha mahali ambapo hawachukui taka?

Nimejaribu kuwaeleza viongozi kwa afisa mtendaji nimeambiwa kuwa huo ni utaratibu kuwa kila mwenye fremu atalipia sh 5000

Niligoma kulipa kwa takribani miezi miwili nikaishia kupelekwa kwa mtendaji na kulipa sh 60000..yaani faini 50000 na 10000 ni pesa ya miezi miwili niliyo goma kulipa

Sasa najiuliza tena ni sahihi kwa wao kuchukua hela mahali ambapo hakuzalishwi taka?

Je, nawezaje kuhakikisha hawa watu hawanidai tena maana nimechoka kutoa pesa ambayo sioni wanachofanya kwangu

Nawasilisha
Mkuu!kiuhalisia kila mtu anazalisha takataka,hata km biashara yako haizalishi taka lkn kitendo cha ww kukaa hapo na kusubiri wateja tayari ni chanzo tosha

Kwani mtu anaweza kuja kupata huduma kwako akiwa na ganda la big G karatasi yeyote alafu akaitupa hapo maana yake tayari umezalisha taka

Kwa sababu ukifagia ule uchafu itakubidi uhifadhi ktk chombo cha taka na mwisho unatakiwa uwape wahusika(wazoa taka)wakatupe sehem husika.
 
Sometimes mambo madogo madogo kama hayo ni kuyafumbia macho tu.
Biashara kibongo bongo sometimes zinakuwa na mambo ya hovyo hovyo kama hayo.
 
Back
Top Bottom