Uliza_Bei
JF-Expert Member
- Feb 17, 2011
- 3,216
- 988
Nimeona niishauri serikali ya CCM iweze kusitisha maandalizi ya bunge la bajeti 2012/13 na sababu yangu kubwa ni kuona bajeti ya 2011/12 hadi sasa haijatekelezwa. Siyo halmashauri wala serikali kuu;ofisi zote hazipokei pesa na hazifanyi kazi, naiomba serikali sasa ipeleke pesa za maendeleo na pia isimamie bajeti ambayo hadi sasa imevurugwa kuliko kuitisha bunge litakalotumia pesa tena. Kama serikali imeshindwa kazi ni vizuri kuomba msaada wa kitaalam hata nchi jirani kama siyo kuitisha uchaguzi kabla ya 2015. Nionavyo yatatufika mabaya kuliko ya serikali ya mzee RUKSA