Hakuna rafiki wala ndugu wa kweli duniani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hakuna rafiki wala ndugu wa kweli duniani

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by NOT ENOUGH, Sep 1, 2011.

 1. NOT ENOUGH

  NOT ENOUGH JF-Expert Member

  #1
  Sep 1, 2011
  Joined: Dec 8, 2010
  Messages: 526
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Jamani mwenzenu nimejifunza kitu kikubwa na ningependa kushare na nyie wenzangu. Katika dunia hii hakuna ndugu wala rafiki wa kweli. Katika rafiki zako wote ulio nao 99.9% si wakweli na ukitaka kujua ni wakati una matatizo kama kufukuzwa kazi, kusimamishwa na kuugua wewe mwenyewe. Na katika ndugu zako ulio nao 98% siyo ndugu wa kweli ukitaka kujua vigezo navyo ni hivyo hivyo au subiri watoto warudishwe shuleni kwa kukosa ada.

  Mimi sasa hivi ndugu zangu ninaowaamini ni watoto wangu na mama yangu, kidogoooooooooooooooo na mume/mke. Ogopa sana wale marafiki unaokula nao maisha huwa hawafai kabisaaaaaaaaaaaaaaa. Binafsi nimepunguza marafiki kwa 99% likewise na ngugu
   
 2. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #2
  Sep 1, 2011
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,650
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Kuna ukweli mwingi katika hayo uliyosema.
   
 3. NOT ENOUGH

  NOT ENOUGH JF-Expert Member

  #3
  Sep 1, 2011
  Joined: Dec 8, 2010
  Messages: 526
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Huo ndo ukweli Nyani Ngabu
   
 4. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #4
  Sep 1, 2011
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  Hivi ulikuwa hujui shost? mie nilijua sina rafiki kipindi cha harusi yangu wale nilioamini kuwa ndo marafiki tungeshilikiana pamoja walikaa pembeni wakiniangalia ,rafiki wa kweli naona ni mme kababy kangu na wazazi...
   
 5. NOT ENOUGH

  NOT ENOUGH JF-Expert Member

  #5
  Sep 1, 2011
  Joined: Dec 8, 2010
  Messages: 526
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Kwenye harusi huwa wanakuja kwenye kikao cha kwanza kisha huwaoni tenaaaaaaaaaaaaaaaaaa mpaka wiki moja kabla ili kuja kucheki kama mambo yameharibika.
   
 6. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #6
  Sep 1, 2011
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,650
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Bajeti ya harusi yako ilikuwa milioni ngapi? Manake huenda waliona unataka kuwaongezea umaskini kwa kuchangia harusi kuuubwa isiyo na ulazima. Binafsi michango ya harusi siifagilii hata kidogo. Sielewagi kwa nini watu huwa hawaridhiki na harusi ndogo ndogo zisizo na gharama.
   
 7. S

  Sharo hiphop JF-Expert Member

  #7
  Sep 1, 2011
  Joined: May 17, 2011
  Messages: 662
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  wengine ni marafiki kwa marafiki zetu,
  by the way huwezi jua nani kutokana na ukweli halisi ulio ndani ya mioyo ya watu................
  jiulize kama hakuna rafiki wa kweli au ndugu wa kweli wewe tukuweke kwenye kundi gani?
  huenda wewe unadhani hakuna rafiki wa kweli kwa vile na wewe sio rafiki wa kweli kwa wengine...........
   
 8. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #8
  Sep 1, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 583
  Trophy Points: 280
  Ni kweli na hata kama una marafiki usitegemee waje wakufanyie mazuri au wakusaidie. Lolote laweza tokea.
   
 9. RedDevil

  RedDevil JF-Expert Member

  #9
  Sep 1, 2011
  Joined: Apr 30, 2009
  Messages: 2,287
  Likes Received: 903
  Trophy Points: 280
  Umeongea kama nimekutuma!! Its better to define our own direction na vingine tunaweka kama secondary. Lakini unakuta mtu ndo anang'ang'ana na ndugu au marafiki kana kwamba bila hao hawezi kupumua. Lakini pia marafiki, ndugu nk ni mhimu katika maisha yetu kwa kiwango chao (I mean, you must leave something for you when you gota friend or ndugu kwenye anga zako).

  Thanx for nice bandiko.
   
 10. VoiceOfReason

  VoiceOfReason JF-Expert Member

  #10
  Sep 1, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 5,234
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 0
  Kwa mentality hii na kila mtu akifikilia hivi no wonder kutakuwa hakuna rafiki wala ndugu wa kweli...

  "Tenda wema uende zako, usingoje kurudishiwa....." That's my motto and am never disappointed, badala ya kungoja kutendewa wema mimi hutenda wema kila ninapoweza na kuwa ndugu kwa kila anayenihitaji... kwa kufanya hivyo hata wale ambao sio wema mwisho wa siku wataona aibu na kuchoka kukutenda.... "For Every Action there is an Equal and Opposite Reaction"

  Ubaya wa mwingine usikufanye na wewe huwe mbaya

  Spread love everywhere you go. Let no one ever come to you without leaving happier.
  Mother Teresa

  One of the greatest diseases is to be nobody to anybody.
  Mother Teresa
   
 11. NOT ENOUGH

  NOT ENOUGH JF-Expert Member

  #11
  Sep 1, 2011
  Joined: Dec 8, 2010
  Messages: 526
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Sharo tunza hii thread siku moja utaelewa nilikuwa na maana gani.
   
 12. NOT ENOUGH

  NOT ENOUGH JF-Expert Member

  #12
  Sep 1, 2011
  Joined: Dec 8, 2010
  Messages: 526
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Good explanation and justification but I have had my experience and I now I have restructured my lifestyle
   
 13. Shantel

  Shantel JF-Expert Member

  #13
  Sep 1, 2011
  Joined: Feb 7, 2011
  Messages: 2,021
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 0
  Yaani we acha tu
   
 14. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #14
  Sep 1, 2011
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  NN bajeti yangu haikuwa kubwa bwana lakini siku tu yule boyfriend aliyekuwa anatutoa out tuna have fun pamoja alipotangaza kutaka kunimiliki urafiki ulikufa kabisa..hehehehe sio kwa sababu ya bajeti bana baada ya hapo na mie nikajifunza nikafunga vioo na kuendelea na life yangu thanks god maisha yanaenda hata bila marafiki wa karibu
   
 15. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #15
  Sep 1, 2011
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  Lakini Husninyo wajua rafiki wa kweli ni asiyekutupa kwenye dhiki na faraja ?
   
 16. lutamyo

  lutamyo JF-Expert Member

  #16
  Sep 1, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 633
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 45
  Yeah!! ni kweli nyani haoni kundule huwezi kuleta tuhuma nzito namna hiyo bila kujiuliza aje wewe ni rafiki wa kweli au ndugu wakweli maana inawezekana na wewe wenzio wanakuona hiyohivyo ingawa uyasemayo yanaweakuwa yapo maana ni dhana tu. Hujawahi kuingia kwenye moyo wa mtu awaye yeyote awe ndugu au rafiki. YALE UYAPENDAYO KUWATENDEA WENGINE NAO WATAKUTENDEA HIVYO HIVYO.
   
 17. Gaga

  Gaga JF-Expert Member

  #17
  Sep 1, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 4,565
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  Yaan mie ndio sisemi, nilishawahi kulalamika humu huwa always nawajali sana rafiki zangu wa kike ila wao huwa hawanijali kabisa sijui kwa nini
  kwa mfano sasa hivi napitia wakati mgumu sana maishani mwangu, naumwa hakuna hata aliyekanyaga kuja niona ni ndugu zangu tu,
  pia humu, hakuna rafiki aliyenotice sipo sana humu except for ashadii, ndio maisha lakini

  Usitegmee sana kupokea wema just tenda wema nenda zako tu thread yako leo imenigusa sana mpendwa, upo lakini?
   
 18. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #18
  Sep 1, 2011
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280

  pole sana Gaga yaani post yako imenifanya nismile tusamehe mpenzi mie siku hizi nadhani Jf naingia mara mbili au tatu kwa week nipe basi namba yako PM niwe nakutwangia jamani inawezekana wewe ni jirani yangu nije hata kukusaidia kupika.
  Pole na kuumwa mungu akusaidie upone haraka
   
 19. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #19
  Sep 1, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 583
  Trophy Points: 280
  <br />
  <br />
  najua ila tatizo tumekuwa tunataraji rafiki zetu watufanyie mambo makubwa au vile tunapenda sisi kwahyo wakienda kinyume tunawaona wabaya au hawafai.
  Hebu fikiria upo kwenye shida na rafiki yupo kwenye shida. Ni vipi ataweza kukusaidia?
  Kama akishindwa kukusaidia utamuona hafai na kuvunja urafiki?
   
 20. NOT ENOUGH

  NOT ENOUGH JF-Expert Member

  #20
  Sep 1, 2011
  Joined: Dec 8, 2010
  Messages: 526
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Nipo Gaga, mashost hawafai. Usione watu wanakuchekea hamna kitu hapo. Pole sana unaumwa na nini tena?
   
Loading...