HAKUNA MTANZANIA ANAYEIOMBEA NCHI MABAYA

HAKUNA MTANZANIA ANAYEIOMBEA NCHI MABAYA

James88

JF-Expert Member
Joined
May 14, 2017
Posts
1,700
Reaction score
1,765
Ninasema hivyo kwa sababu hata hayo mabaya yakifika hakuna mtu ambaye atakuwa salama,

Labda nijaribu kutoa mfano, Kuna baadhi ya watu wanasema kwamba nchi yetu inaweza ikaja kukumbwa na balaa la njaa hasa kutokana na kudorora kwa bei ya mazao especially mahindi, Tumeona bei ya gunia la mahindi ikifika sh. 20000/= tu.

Kutokana na bei ya mahindi kufika hapo ilipo... kuna watu ambao wanafurahia hasa Consumers lakini je hali iko vipi kwa Producers?

Ukweli ni kwamba waliozalisha mahindi kwa kiasi kikubwa mwaka huu imewagharimu sana na wameingia hasara kubwa mno.

Sasa basi kutokana na hayo hapo juu, njaa inakujaje?

Tukija theory ndogo tu ya uchumi(mliosoma uchumi mnaweza kunisaidia pia) kuhusu demand and supply utaona kwamba kwa sasa supply ya mahindi nchini imekuwa ni kubwa mno na hilo limechangiwa sana na kufungwa kwa mipaka hivyo watu wameshindwa kusafirisha mahindi kupeleka nje ya nchi na hivyo mahindi yote yamejazana soko la ndani.

Kwa maana hiyo kitakachotokea katika msimu ujao ni kwamba watu watalima tu kidogo kwa ajili ya kutosheleza mahitaji ya chakula majumbani mwao na si kwa sababu ya biashara kwa sababu hakuna mtu atakayetaka kufanya biashara ambayo anajua fika kwamba itamkata.

Hivyo basi demand ya mahindi itakuwa kubwa mno na hili litapelekea bei ya mahindi kwenda juu sana na hapa ndipo njaa itakapotokea....

Hivyo basi watu wanapokuwa wanaongelea mambo ambayo yanaweza kuikumba nchi huko mbeleni siyo kwamba wanaitakia nchi mabaya.

Ni hayo tu...
 
Back
Top Bottom