Hakuna movie kali ya kivita kuzidi Saving Private Ryan

FORTALEZA

JF-Expert Member
Jan 1, 2017
6,845
2,000
Hii movie nimeiona zamani hebu nijaribu kukumbuka leo...

Utamu wa hii movie kwanza ni story yake ambayo ni kisa cha kweli kilichotokea katika vita kuu ya pili ya dunia.

Story iko hivi, wanajeshi wa Marekani wakiwa vitani wanapigwa kipondo cha kufa mtu hali iliyopelekea wengi wao kupoteza maisha.

Sasa baadhi ya miili inarejeshwa kwenda kuzikwa Marekani.

Mama mmoja anapewa habari kuwa watoto wake watatu wamefariki katika uwanja wa kivita, mama analia sana lakini anawaambia watoto wake walikuwa wanne, hivyo kuna mmoja atakuwa aksalia kwenye uwanja wa kivita.

Basi kinatumwa kikosi kwa ajili ya kwenda kumtafuta mtoto wa nne wa yule mama, ambaye ni private ryan.

Wanamkuta private ryan katika uwanja wa vita anakiwasha kweri kweriiii (in mwendazake's voice) katika hali ya kushangaza private ryan anagoma kurudi nyumbani

Balaa sasa lipo hapo...
 

souljar

JF-Expert Member
Feb 16, 2021
390
1,000
Hii ni mwisho wa matatizo, kwanza mwanzo tu wa movie kama una roho nyepesi huwezi kuendelea kutazama. Watu walichakazwa na risasi yaani sio poa.

Hivi kuna movie ya kivita kali zaidi ya hii? Nitajie kama ipo
Nenda kaangalie LONE SURVIVOR, alafu urudi tujadiliane upya baada ya kubadilisha title ya post yako.

Sent from my 601SO using JamiiForums mobile app
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom