Hakuna Mikusanyiko: Hakuna pesa za show, tutarajie wasanii kuwa kimya kupita maelezo

dudu jeupe

JF-Expert Member
Mar 30, 2020
495
1,000
1587289627470.png

Katika kipindi hiki cha korona mikusanyiko hairuhusiwi, vilevile show nazo haziruhusiwi.

Tukiachana na Diamond Platnumz ambae hata asipopiga show anapiga pesa kwa Wasafi Media, YouTube views nyingi na kuwa balozi wa makampuni kadha na kadha, hali si hali kwa wasanii wengine ambao hutengemea vipato vyao asilimia kubwa kutoka mkwanja wa shows maana huko YouTube ili angalau urudishe pesa ya video na ya producer basi angalau uwe na views milioni 5 na ili kufaidika sana na YouTube basi angalau upige views milioni 10 kitu ambacho ni msanii moja tu anakiweza.

Show ni moja ya mkondo muhimu katika uchumi wa wasanii wetu wa hapa Tanzania, pesa hizo ndizo zinazowafanya watengeneze vichupa na ngoma. Zamani mambo yakifeli watu walibebeba ngada kuipeleka sauzi ila kwa sasa mambo sio mambo.

Kwa kipindi hiki tusishangae hata kidogo msanii kuwa kimya sana kwasababu mambo yamekuwa magumu sana, Ila haya matatizo pia ni kama "kufa kufaana" wasanii wengi hiki kipindi wanapokuwa na wakati mgumu basi wenye nazo ndio muda wao huu.
 

innocent dependent

JF-Expert Member
Jun 8, 2019
5,126
2,000
Hili pia liwe Kama funzo kwako wasitegemee pekee mziki kuendesha maisha yao wajitahidi kutumia brand zao vizuri kubiga pesa nje ya mziki.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom