Ferruccio Lamborghini
JF-Expert Member
- Apr 15, 2020
- 1,664
- 2,517
TUNAFAHAMU kwamba katika ukanda wa Afrika, nchi ya Tanzania ndio ilikuwa inaongoza kwa kuwa na bei rahisi za mabando ya simu kuliko nchi yoyote hapa Afrika (Sub Saharan).
Jambo hili liligeuka kuwa silaha kwa tasnia yetu ya muziki wa Bongo Fleva katika sura ya Bara la Afrika, ilikuwa rahisi sana Msaga Sumu kugonga views milioni kuliko msanii wa Afrika Kusini, Kenya, Ghana, Zambia, n.k kupata hata robo ya hizo views.
Views zilikuwa ni silaha yetu, ziifanya hata watu wa mataifa mengine kuanza kutufatilia, hata kwenye tuzo za kimataifa hizo views zilikuwa na uzito wake.
Ukija pia kwenye platform za kusikiliza miziki kupitia Boomplay na Audiomac nako pia tulikuwa tunakimbiza maana internet ilikuwa bei rahisi. Lakini mambo yamebadilika sasa, tangu wiki iliyopita kumekuwa na mabadiliko makubwa sana kwenye mtandao wa YouTube.
YouTube, hali ni mbaya, hata Lavalava aliekuwa havumi sana ilikuwa kawaida kupata views laki 4 ndani ya siku lakini hadi sasa ana views kupata views 252K na hizi huenda nyingi ni za mashabiki namba 2 wa bongo fleva kutoka Kenya.
Maua Sama nae ngoma yake ipo trending number 1, tulizoea ngoma kishika usukani basi kwenye siku ya 4 itakuwa na views walaki laki 7 mpaka milioni 2, lakini cha kushangaza hadi sasa ni views laki 2 tu nazo si ajabu zikiwa nyingi kutoka kenya.
Malkia wa Wasafi, Zuchu nae naona upepo umemwendea ndivyo sivyo, video ina wiki ila ni views laki 745 tu, kiukweli Zuchu ilibidi hapa awe na views hata milioni 2 au 3, hapa napo wakenya wamehusika sana.
Kiufupi tutarajie anguko la kazi za wasanii kwenye online platforms, mabando kwa sasa mtu anaingia YouTube kwa machale sana, ni heri aingiziwe video kwenye simu yake huko vibandani. Kwa kipindi hiki mashabiki wa Kenya huenda watajaza views zaidi kuliko Watanzania.
Kwa sasa nadhani wa nigeria wamefurahia sana hili suala, na pengine kabla mwaka haujaisha mabando yatapandishwa tena na huu utakuwa msumari wamoto kwenye upande wa YouTube views.
Upande mwingine najaribu kujiuliza, au wameacha kununua views ndio maana wanapata views wa kawaida? Hata zile stori za kwamba mimi nimeibiwa views na upande wa pili hazisikiki….. Bado sina majibu, nisaidie na wewe mawazo yako.
©GP