Hakuna mgogoro wowote CHADEMA-Wenje

Hakuna mgogoro wowote CHADEMA-Wenje

Molemo

JF-Expert Member
Joined
Sep 24, 2010
Posts
14,620
Reaction score
13,361
Mbunge wa Nyamagana na Mkurugenzi wa mambo ya nje wa Chadema Ezekiah Wenje amesema kwamba chama chake hakina mgogoro wowote.

Akihutubia umati wa watu katika mkutano mkubwa wa hadhara wa wafuasi wa Chadema Gongolamboto DSM Wenje alisema kwamba kilichopo ni baadhi ya viongozi wa CCM kuwanunua baadhi ya watu wasio waaminifu na wenye njaa na kuanza kuropoka hovyo mambo ya kijinga kwenye vyombo vya habari.

Wenje alisema bahati njema wasaliti wote wanafahamika na taratibu za kuwashughulikia zinaendelea kufanywa dhidi yao.

Chadema wanaendelea na operesheni kubwa za M4C huku viongozi wake mashuhuri wakiwa maeneo mbalimbali ya nchi.Viongozi walioko maeneo mbalimbali wakihaha kuimarisha chama ni Godbless Lema,John Heche,James Millya na Alphonce Mawazo walioko maeneo mbalimbali ya Kanda ya ziwa.Wengine ni Tundu Lissu,Peter Msigwa na Joseph Mbilinyi wanaohaha maeneo ya nyanda za juu kusini.Pia mbunge Vicent Nyerere alikuwa akizunguka mikoa kadhaa kuimarisha chama.Naye Mkiti wa chama Freeman Mbowe alikuwa Karatu.

Source:Tanzania Daima.
 
Mkuu Molemo jana nilitingwa na shughuli nyingine za kitaifa nikashindwa kuhudhuria mkutano huo uliokuwa uwanja wa nyumbani.
Nashukuru kwa kutuwekea kipande hiki cha yaliyojiri jana.
Masalia wamejulikana na sasa wanahaha kutafuta namna ya kujisalimisha.
 
Last edited by a moderator:

Heri ya mwaka mpya mkuu Mwita Maranya.Nimeona niwawekee wadau aliyoyasema mtoto wa mama Ntilie Ezekiah Wenje.

Kwa kweli makamanda wamejipanga.
 
Last edited by a moderator:
Hayo maneno yanapaswa kuzungumzwa kijijini ambapo hakuna vyombo vya habari
 
Ndugu Molemo , asante sana kwa taarifa , mungu akuwezeshe na mwaka huu uendelee kutujulisha mambo mazuri .
 
Ninachoipendea CHADEMA kimeanza kuwa na tasira ya wapiganaji wengi...safi sana si lazima DR aingie mzigoni ili movement iendelee...safi mno CDM
 
hata mie najua hakuna mgogoro chadema, ila ccm km kawaida yao wanataka kupenyeza chuki ili m4c isambaratike, lkn njia ya mwongo ni fupi itajulikana tu ni dhalimu ccm ndo anatafuta wa kufa nae
 
Hilo halina ubishi, CHADEMA hakina mgogoro bali kina kundi/makundi ambayo yako mbioni kuzaa mgogoro/migogoro kama chama kitaendelea kuyabeza kama kinavyofanya kwa sasa.
 
hayo maneno yanapaswa kuzungumzwa kijijini ambapo hakuna vyombo vya habari

kweli ccm ni chama cha ovyo kabisa yaani kwa miaka ya uhuru zaidi ya hamsini bado hawajaweza kufikisha vyombo vya habari vijijini!!!!? Hopeless kabisa hiki chama.
 
Ninachoipendea CHADEMA kimeanza kuwa na tasira ya wapiganaji wengi...safi sana si lazima DR aingie mzigoni ili movement iendelee...safi mno CDM

Ni kweli mkuu asigwa.Si lazima kila siku Dr Slaa aende mikoani kuhutubia.
 
Last edited by a moderator:
Hilo halina ubishi, CHADEMA hakina mgogoro bali kina kundi/makundi ambayo yako mbioni kuzaa mgogoro/migogoro kama chama kitaendelea kuyabeza kama kinavyofanya kwa sasa.

Chadema hakuna makundi bali kulikuwa na kundi moja tu la PM7 ambalo kwa bahati nzuri tayari limeshaelekezwa kibla.
Sasa huo mgogoro unaoutabiri utaanzia wapi? Au unajiandaa kuanzisha kundi? Tuko makini tutakubamba tu ukijaribu...
 
Mkuu,
Hizi swaga kama hizi hata CCM ndizo walizokuwa wanazitumia, unfortunate, hata wewe/ninyi mmezikwapua.

Uchaguzi wa ndani na kuelekea kwenye chaguzi za nchi ndizo zitathibitisha usemi wako. Mtaji wa kisiasa nchini ndio unaweza kuwa ni kitanzi chake kama viongozi wataendelea kuwa na swaga kama zako.

Hii nisemayo ni sauti tu ya nyikani. Take my word, CHADEMA kuna kundi/makundi.
 
Nakukubali sana kamanda Wenje, kweli CHADEMA hakuna mgogoro ila kuna baadhi vijana wenye njaa ambao wamekuwa waitumiwa na maadui wa CHADEMA waliopo ndani na nje ya CHADEMA ili kutoa matamko ya kipumbavu ili kukiua chama.
 
Hilo halina ubishi, CHADEMA hakina mgogoro bali kina kundi/makundi ambayo yako mbioni kuzaa mgogoro/migogoro kama chama kitaendelea kuyabeza kama kinavyofanya kwa sasa.
Ukificha maradhi kilio kitakuumbua. Karatu baadhi ya watendaji wamesimamishwa na uchunguzi dhidi ya ubadhirifu unaendelea. Ilemela mambo si shwari, Mpanda wamefukuzwa watu na Mbeya pia! Wenjen Mwl Nyerere alisema "Mubhisabhisa bhurweri ekirilo kilimubhura" yaan ukificha ugonja... Nawatakia mwaka 2013 mwema!
 
CDM acheni kujidangaja na kujipa sifa za kijinga ingawa ukweli unauma lakini ndani ya chama chenu hali sio shwari kama mnavyojidanganya hapa na kupeana moyo ukweli unajionesha hapa jf kutukanana viongozi kwa viongozi na wengine kuhama chama ingawa kwa akili zenu na mawazo mgando eti wamenunuliwa na ccm eleweni chechea ndio iliyoanzisha moto mkubwa
 
Mtu mnafiki ni mbaya kuliko mchawi.Kwa nini viongozi waseme uongo wakati kuna mambo hayaendi sawa ndani ya chama.Mficha ugonjwa mauti humuumbua.
 
Mkuu,
Hizi swaga kama hizi hata CCM ndizo walizokuwa wanazitumia, unfortunate, hata wewe/ninyi mmezikwapua.

Uchaguzi wa ndani na kuelekea kwenye chaguzi za nchi ndizo zitathibitisha usemi wako. Mtaji wa kisiasa nchini ndio unaweza kuwa ni kitanzi chake kama viongozi wataendelea kuwa na swaga kama zako.

Hii nisemayo ni sauti tu ya nyikani. Take my word, CHADEMA kuna kundi/makundi.
Poti ulisiza bhageshi,hivi nidokezee hayo makundi/kundi unavyothibisha kwa nguvu zote yako wapi vile je ni ya kina nani vile,nijuavyo mimi ilikuwa ni masalia aka PM7 lakini wamebainika na utaratibu wa kuwashughulikia uko mezani na tunajua waliouasisi na supoort kubwa pia wanapata kutoka CCM akiwemo Mwigulu.sasa naona bhageshi unauhakika kundi/makundi yapo wakati wengine hatuyaoni,au labda unajua yanenda kuanzishwa mengine?basi tudokezee poti,maana siku hizi mawasiliano ya kila aina yapo hata nikiwa Ikungulya bhashasi,au Senani taarifa zitanifikia,hebu nidokezee poti,maana mi najua kalikuwepo kajikundi ka masalia nako kamebainika.
 
Back
Top Bottom