Hakuna mgogoro wowote CHADEMA-Wenje

Hakuna mgogoro wowote CHADEMA-Wenje

Mbunge wa Nyamagana na Mkurugenzi wa mambo ya nje wa Chadema Ezekiah Wenje amesema kwamba chama chake hakina mgogoro wowote.

Akihutubia umati wa watu katika mkutano mkubwa wa hadhara wa wafuasi wa Chadema Gongolamboto DSM Wenje alisema kwamba kilichopo ni baadhi ya viongozi wa CCM kuwanunua baadhi ya watu wasio waaminifu na wenye njaa na kuanza kuropoka hovyo mambo ya kijinga kwenye vyombo vya habari.

Wenje alisema bahati njema wasaliti wote wanafahamika na taratibu za kuwashughulikia zinaendelea kufanywa dhidi yao.

Chadema wanaendelea na operesheni kubwa za M4C huku viongozi wake mashuhuri wakiwa maeneo mbalimbali ya nchi.Viongozi walioko maeneo mbalimbali wakihaha kuimarisha chama ni Godbless Lema,John Heche,James Millya na Alphonce Mawazo walioko maeneo mbalimbali ya Kanda ya ziwa.Wengine ni Tundu Lissu,Peter Msigwa na Joseph Mbilinyi wanaohaha maeneo ya nyanda za juu kusini.Pia mbunge Vicent Nyerere alikuwa akizunguka mikoa kadhaa kuimarisha chama.Naye Mkiti wa chama Freeman Mbowe alikuwa Karatu.

Source:Tanzania Daima.

Naomba msaada. Mawazo ana wadhifa gani katika chama, huyu jamaa nichali angu kwasana tumecheza nae bol mchangani tukiwa makid enzi hizo nikiwa Arachuga. I know him, hatanii anapokuwa kazini ni mpiganaji wa ukweli, ila sikumbuki level yake ya elimu lakini haijalishi.
 
Ni kamanda mkuu wa M4C Kanda ya ziwa.
 
mkuu molemo umewamudu masalia..

Mkuu wangu Masalia ni kundi haramu la uasi dhidi ya Chadema kama kundi la M23 lilivyo kundi la uasi dhidi ya Congo DRC
 
Wewe unashikiwa akili na viongozi wako. Makundi yapo na viongozi wao ni freeman na zito pili kati ya wewe uliyeandika hapo juu na zito nani ananjaa. Acha kushikiwa mawazo tumia akili aliyokupa Mungu
 
Ni kweli hizi habari za migogoro CDM ni ya kuzusha na ccm wanaitumia kuivuruga ccm. CDM wanatakiwa kusimama na kukanusha uzushi wote unaoelekezwa kwao, maana wakikaa kimya watu wataamini kama ni kweli kuna mgogoro.

Back
Top Bottom