Hakuna kitu huwa sikipendi kama kuwatupia Lawama washauri

lee Vladimir cleef

JF-Expert Member
Feb 5, 2013
9,154
33,354
Hapa Tanzania kumezuka na kauli za hovyo za kutetea ujinga kwa kuwatupia Lawama washauri.

Kwa mfano utasikia baadhi ya watu wakimtetea kiongozi fulani pale Jambo linapoharibika kwa kusema"Unajua kiongozi inawezekana Hana Nia mbaya ila Anawashauri wabaya" au unajua kiongozi Ana Nia njema ila Sema Ana shauriwa vibaya,watu wanamshauri kwa Maslahi Yao"

Hizi kauli zipo Sana na zimechuku kasi kubwa Sana. Ki ukweli Ukiwa na kiongozi ambae hajui kutofautisha Kati ya ushauri mbaya na ushauri mzuri huyo hafai kuwa kiongozi.

Kiongozi Bora ukiona mshauri anakushauri vibaya piga chini,ila ukipokea ushauri huo ujue wewe ndo wa kuwajibika. Tundu Lissu hajafa, karudi na Moto kuliko alivyokuwa.

Dunia nzima inafuatilia kila hatua anayopiga.
 
Awamu hii tumepata hasara kubwa mno,labda apelekwe kwenye semina za leadership skills
 
Tundu Lissu mashine ya kazi! Watakula mahindi, watakunywa kahawa lkn kipigo kipo palepale!

Awamu ile alipiga push ups lakini awamu hii ataruka kichura chura.
 
Back
Top Bottom