Je, hakuna kosa la kiufundi kidiplomasia lilifanyika kwenye 'briefing'?

Titicomb

JF-Expert Member
Jan 27, 2012
11,348
17,859
Ombi: Naomba nitangulize ombi la kusamehewa kama nitakuwa nimewakwaza watu katika mchango huu wa mawazo.

Nitatoa maoni kwa mtindo wa kuuliza swali ili tupate mawazo ya watu wengi, huenda tuna nguli wengi wa kidiplomasia humu JF.

Mawazo Yangu: Lile angalizo alilotoa kiongozi mkuu kuhusu kuwa makini na misaada ya kujikinga na COVID-19 nahisi kama lingetolewa kwa wahusika nyuma ya pazia.

Ufafanuzi Wa Mawazo Yangu:
Kuna misaada tuliyopewa na watu binafsi, taasisi binafsi, wafanyabiashara wa ndani na pengine wa nje ya nchi, na pengine kutoka kwa nchi rafiki kupitia wanadiplomasia wao waliopo nchini, au kupitia wanadiplomasia wetu waliopo nje ya nchi yetu.

Kwa kutoa angalizo kama lile bila kutaja msaada wa yupi hasa wa kutiliwa mashaka ni kuwaweka wote waliotoa misaada katika kundi moja la watiliwa mashaka. Je, hatuoni kwamba hii inazidi kutengeneza nafasi kubwa ya kujitenga au kutengwa kidiplomasia zaidi ya hali hii iliyopo sasa? Ninahisi tunaweza kunyimwa misaada au misamaha ya mikopo toka nchi washirika na wahisani.

Maoni Yangu Nini Kifanyike:
Katika nyakati kama hizi nahisi tunahitaji kila aina ya marafiki na wahisani tuweze kulishinda janga hili la ugonjwa wa COVID-19, kinachotakiwa hapa ni kuchukua zile tahadhari kama alivyotoa angalizo kiongozi wetu mkuu.

Tahadhari na angalizo kama hizi nafikiri ingekuwa bora kama tungewapa vyombo husika na watendaji wetu wote nyuma ya pazia, zile zinazo husu umma wote basi zifanywe hadharani kama ilivyofanyika.

Ninaona kutakuwa na uhitaji mkubwa wa ushirikiano zaidi ya huu wanao toa sasa hawa wahisani hasa baada ya kuisha ugonjwa wa COVID-19 katika nyakati zile za kujaribu kuokoa uchumi wetu utakao kuwa umetetereka kwa kiasi kikubwa sana na janga hili lililokuja ghafla bila kutegemewa. Sidhani sisi wenyewe kwa vyanzo vyetu vya ndani vya kipato kama tutaweza kusimama tena imara kirahisi bila msaada washirika/wahisani wa ndani na nje.
Tukiwakwaza sasa watakuja kutususa baadae tutakapo wahitaji.

Pia ningeshauri nyakati hizi viongozi na wawakilishi wetu wachukue tahadhari kubwa sana kwenye kauli au maoni yao, ikiwezekana waandike kabisa wanachotaka kusema na kihakikiwe na washauri na mhusika ahakikishe hatoki nje ya yale aliyo jiandalia kuzungumza hadharani.

Maoni binafsi ya kiongozi kama binadamu wa kawaida na siyo muwakilishi wa jamii fulani hayo ni vema yatolewe mbali sana na vyombo vya mawasiliano vya kisasa mfano SMART TV, SIMU (Aina zote), n.k. Funikeni utepe mweusi(Black cello tape) kwenye camera za Laptop, TV, ipad, Tablet na simu zenu.

Ondoeni (disable) vinasa sauti (mic and other voice recorder) kwenye hivyo vifaa. Msitumie kabisa vitu ambavyo vinapokea maelekezo kwa sauti kma vile Alexa na Apple Siri. Vifaa vingi vya kisasa vinakuwa na uwezo wa kurekodi sauti au na picha (video) vikiwa kwenye mtandao au vikiwa havijaungwa na mtandao kisha kutuma taarifa vikishaungwa kwenye mtandao(internet).

Katika ulimwengu huu wa sasa unaweza kudukuliwa na hivyo vifaa wakati unaongea na watu wako wa karibu na ulichoongea kikafika mikononi mwa adui wako au mshirika/ mhisani wako uliye mteta vibaya. Fuatilieni taarifa za Wikileaks na 'diplomatic cables' za taifa kubwa zilizovuja mitandaoni, ukienda Channel ya BBC huko Youtube utazipata taarifa hizi vizuri.
Ushauri huo hapo juu ni kwa viongozi wangu, najuwa mna watu makini na mmeshafanya yote hayo lakini mimi nimekumbusha tu wakuu wangu.

Ushauri Kwa Washauri:
Msisite kuwakumbusha mliokabidhiwa jukumu la kuwasaidia kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi. Shaurini, kumbusheni msiogope mkaacha watu wafanye makosa ya kibinadamu.

Viongozi na washauri wao fanyeni tathimini za kina juu ya makosa ya kiufundi au ya kibinadamu yaliyofanyika kwenye matukio kama hotuba za viongozi husika. Washauriwe viongozi nini kifanyike siku nyingine. Hapa najuwa washauri mnajuwa lugha ya hekima ya kumwambia mtu unaye mheshimu wapi au nini amekosea bila kumkwaza.
Huo usiwe wakati wa kulaumiana bali wa kusaidiana mawazo kama timu moja.

Hapa naongeza ushauri nje ya mada kidogo kwa Washauri (Make no mistake, Ushuri huu muhimu sana):-
Toeni elimu kwa mnao washauri juu ya kutambua habari zilizo thibitishwa huko mitandaoni, wateja wenu wawe makini sana na shauri za tiba na mengineyo toka mitandaoni.

Tiba nyingi hasa tiba mbadala za mitandaoni zinakuwa siyo za kweli au hazina ufanisi hivyo watu wakizitegemea sana na kuacha yale yaliyo shauriwa na wataalamu waliothibitisha ufanisi tunaweza kupata misiba kila kona. Nyingi ya hizi tiba zinakuwa na madhara hasi ambayo hayajagunduliwa bado.

Nitawapa mfano: Ukienda mitandaoni hasa Youtube utakuta ushauri tiba ya kupungukiwa nguvu za kiume sijui uponde na kusaga maganda ya mayai (egg shells) kisha uchanganye na asali au na maji ya moto, wengine usage maganda ya tikiti (Watermelon rind) unywe.
Lakini kula maganda ya mayai mengi kunaweza kusababisha matatizo ya figo na mengineyo, maganda ya tikiti hasa yaliyo pulizwa karibuni dawa ya kuzuwia wadudu waisitoboe ni hatari kwa afya ya binadamu, labda yangekuwa yamelimwa kilimo cha kijani (organic). Thahadhari hizi zote hazisemwi kule mitandaoni.

Ni muhimu kwa viongozi kutochangia maoni au mitazmo yenu moja kwa moja (direct) au kwa namna nyingine (indirect) kuhusu habari zinazo zagaa (trend) mitandaoni kuhusu tuhuma dhidi ya mataifa au taasisi flani. Habari zingine ni za kutengenezwa kwa makusudi flani. Hili janga la COVID-19 linaweza kuwa ni vita vya kibaolojia na kiuchumi baina ya mahasimu fulani.

Kwa uwezo wetu kiuchumi na kitekinolojia ni vema kutoingia mtego wa kuipa nguvu tuhuma fulani ya upande mmoja unao pigana vita. sababu hatuna uwezo mkubwa sana wa kuthibitisha ukweli au uhalali wa tuhuma husika. Kwa mfano sakata la barakoa zilizo rudishwa kwa tuhuma za kuwa na vijidudu vya Coronavirus, mbona baada ya sakata lile wale waliodai kupewa mzigo mbaya waliendelea kuagiza kwa wingi mzigo kama huo toka kwa walewale walio tuhumiwa kuwaletea mzigo mbaya?

Hatuoni kwamba kama kweli mzigo ulikuwa mchafu basi yalikuwa makosa ya kiufundi tu kiwandani na siyo hujuma kama inavyo dhaniwa na sisi wanyonge tunao ogopa misaada toka kwa hao wanao tuhumiwa kutuma mzigo mchafu?

Nafikiri tungejikita katika mlengo wa kutofungamana na upande wowote kama vile tulivyo achiwa na Mwalimu Nyerere.

Mnisamehe sina nia kuwafundisha kazi ambayo mimi mwenyewe siiwezi na siijui, kiukweli hadi sasa mmnafanya kazi kubwa sana kwa umakini mkubwa, nia yangu ni kukumbushana tu wakuu.

ANGALIZO: Namna nilivyoelewa angalizo la kiongozi wetu au niite maoni yake inaweza kuwa nilielewa tofauti sana na alivyo kusudia kufikisha ujumbe kwa hadhira, utofauti huo unaweza kuwa ulitokana na mimi kukosa au kupata mawasiliano ya kiwango duni cha matangazo ya moja kwa moja ya tukio husika. Hapa niseme wazi vyombo vya habari vya umma vimetuangusha sana.

Pia nikili kuwa sikusikiliza hotuba yote sababu kuu ni tatizo nililotaja hapo juu la mawasiliano.
NASISITIZA LENGO LA MAWAZO YANGU HAPA NI KUSAIDIA KUJENGA NCHI NA SIO KUBOMOA NCHI AU KUPOTOSHA WANANCHI.

Titicomb Wa JF
 
Titicomb,
Kumbe bado JF ina GT kama wewe Mkuu. Ushauri wa kina sana huu. Natamani hali iwe hivyo ulivyoshauri maaana naona hatari ya kutengwa na wadau au wahisani baadhi wakihofia kutemewa cheche baadae.
 
Kumbe bado JF ina GT kama wewe Mkuu. Ushauri wa kina sana huu. Natamani hali iwe hivyo ulivyoshauri maaana naona hatari ya kutengwa na wadau au wahisani baadhi wakihofia kutemewa cheche baadae.
Ahsante mkuu.
I'm humbled indeed!
 
Mkuu disregard and ignore Joowzey a.k.a Joseph fulani (Surname kwenye mabano ila namjuwa vizuri utambulisho wake).
Tuna watu wa kila aina humu wenye matatizo mbalimbali na umri tofauti.

Kuna wengine kuwa hasi au kushambulia watu ni tiba kwao ya tatizo la kiakili kama kukosa kujiamini au mambo mengine ya msongo wa mawazo.

Wengine wapo kazini ....

Wengine wanahisi kuna kitu umemzidi hivyo anajaribu kukushusha hadi kiwango chake mufanane.

Ningeweza kumsaidia maarifa yaliyo pendekezwa na wataalamu ambayo yeye anahisi nimedokeza kwa kuona kwenye filamu(movie). Ningemuwekea toka taasisi kubwa duniani au toka kwa wanazuoni link au attachments za vitabu au multimedia zingine kama video na sauti lakini naona havitamsaidia kwa uwezo wake wa ku-digest vitu kama hivyo.
Huko kwenye movie wanaigiza vitu vingi ambavyo tayari vinaendelea duniani au vipo kwenye hatua ya utafiti, Yeye halijui hili suala anaona wanaigiza tu kama kufurahisha watazamaji.

Tatizo lake ni kufikiri na kukariri kila anacho ona kwenye movie ni cha kufikirika tu hakiwezi kutokea katika maisha halisi duniani.
 
Back
Top Bottom