Hakuna jambo baya kama baba kumtegemea mwanaye

Duh.. Kuna mtu alikuwa yupo vyr, mara bila kutarajia kageuzwa kuwa BABA JINGA na ile bomoa bomoa ya Kimara
 
Duh.. Kuna mtu alikuwa yupo vzr, mara bila kutarajia kageuzwa kuwa BABA JINGA na ile bomoa bomoa ya Kimara
 
Duh.. Kuna mtu alikuwa yupo vzr, mara bila kutarajia kageuzwa kuwa BABA JINGA na ile bomoa bomoa ya Kimara
 
Daaa aisee wacha niendelee kupigana
 
Kwamba amsubiri Israel kwa shauku kubwa[emoji1] [emoji1]
 
Naona mzee kazidi kukupiga mizinga mkuu mpaka umeona uanzishe thread[emoji1] [emoji1] [emoji1] ,ila wazee wengine wamezidi kwa kweli yani anakua kama anataka arudishe pesa zote alizotumia kukulea,mizinga kila kukicha na mbaya zaidi unakuta mzee ni mzima na ana nguvu zake tu [emoji4] ,kupigwa mizinga hatukatai ila iwe aste aste ,tutakua hatuendelei sasa kwa system hii
 
Watu wanamlaumu mtoa mada kadharau wazazi ila mi naona kaongea jambo jema na la kweli, .....vijana wengi sasa tunalea wazazi wetu kwa kuwa hawakuwekeza kwa sababu mbalimbali labda umaskin,ukubwa wa familia,maradhi etc,anachotushauri ni kwamba VIJANA TUWEKEZE TUSISUBIRI WATOTO WATUTUNZE UZEENI....mbona mifano mingi ipo mitaani wazee wanavyodhalilika hata hela ya panadol anakosa akiumwa,mtu huyu angekuwa na miradi endelevu hawez subir hadi watoto waitane wamsaidie....kama wewe unataka maisha hayo uzeeni endelea kupuyanga saizi ujanani
 


Wataelewa mbeleni huko.

Achana nao hao
 


Baba anamtegemeaje mtoto Kama sio upuuzi
 
Wanaume wa siku hizi wanaogopa sana majukumu hata kuoa tu mke asie na kazi hawawezi na akioa mwenye kazi anamwachia majukumu ya nyumbani.

Hao ndo watoto wakikua pia wanawahamishia watoto majukumu. Mwanaume mpambanaji anajua majukumu yake na anawajibika 100 percent kwa familia yake.
 


Alafu wepesi kujifanya wanatoka laana. Pumbavu
 
Wazee wetu huko nyuma hawakuwa na makosa bali nyakati na na exposure ndogo ndio ziliwafikisha hapo hatuna haja kuwalaumu ni kuwaombea mbele za Mwenyezi Mungu awabariki na kuwasamehe makosa yao..

Kizazi cha sasa kuanzia miaka 50 kushuka chini tuna kila kitu na hatuna haja ya kushindwa kuandaa uzee na kuandaa vijana wetu... tuna exposure, nyakati bora, fursa za kutosha kinachotakiwa ni uthubutu na kujitoa kutengeneza maisha yako binafsi ya uzeeni na watoto wako..
 
Hapa hata usipologwa utaonekana umelogeka maana utaona mambo hayaendi wallah😂😂
 
Umeupiga mwingi mkuu, Tuwaheshimu tu hawa wazee wetu maana wametutangulia na ndiyo waliotuleta duniani Ila wengi wanafeli sana hapo.... imagine 17yrs nimeachana na masomo kwa kuwa walishindwa kuniendeleza basi wakanisukumia Dar kwa Ndugu kwa lengo la wao kuniendeleza japo kwenye ufundi, Nao kama kawaida baada ya muda majungu na visa vikaanza ikabidi niingie kwenye hustling za maisha baada ya wao kusikia tu nimepata kiajira tu Simu zikaanza kuita.
 
Baba mwema huacha urithi mpaka kwa wana wa wanae yaani wajukuu.

Hiyo ni kwa mujibu wa Maandiko Matakatifu.

Sasa kama hadi wajukuu wanakuta mali ya babu/ bibi huyo baba atalalamika saaa ngapi? Mali zake zitazidi kumsaidia maisha yake yote.
Sasa ukiona baba analalamika kutokuhumiwa ujue hakuwajibika vyema mahali fulani kwenye maisha yake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…