Hakuna jambo baya kama baba kumtegemea mwanaye

hata Mimi SIKUBALIANI naye huyu haiwezekani watoto wasipowaangalia wazee alitaka Nani awatizame hapa ndio utaona tofauti ya dini ya kweli Na dini batili

Mkuu hapa atuzungumzii ishu ya dini. Lakini kwa muktadha huo dini husika inaendekeza uvivu eti kisa watoto watakulea. Ndio maana waamini katika dini husika hujiolea tuu na kuzaa hovyo bila akili kama wanyama
 
Baki na laana zako mzee...
 
Mkuu hapa atuzungumzii ishu ya dini. Lakini kwa muktadha huo dini husika inaendekeza uvivu eti kisa watoto watakulea. Ndio maana waamini katika dini husika hujiolea tuu na kuzaa hovyo bila akili kama wanyama
Labda Kuna mtu unakusudia kumtukana hapa vinginevyo umejibu kichuki zaidi kwa hiyo naomba uelewe kuwa kuoa ni ibada Na kuzaa ni majaaliwa ya mungu wangapi wana wake lkn hawajazaa Yaani wagumba Na wangapi wanabaka. Na wamejaza watoto
 
Hahahahaaaa... Wazee marijali siyo?
Ni balaa kuna watu sijui huwa wanawaza nini, huna investment yoyote unazaa mtoto katika umri wa miaka 60
Nazani siyo Tanga tu bali mwambao wa Pwani Kwa ujumla kuna hiyo kasumba!
Unakuta Mtu umri umeenda lakini anatotoa tu kisha akiondoka anaachia wenzie wigazi!
Mkuu hii ipo maeneo mengi tu, kwingine unakuta migogoro ya kifamilia inapelekea kutengana mzee anatafuta mke mwingine anaendelea kuzaa hata kama ana watoto wakubwa tayari
 
Hii inatuhusu sisi wenyewe na wala si baba zetu. Baba zetu pengine muda wao umekwishapita. Sisi tuna muda wa kutokuwa baba-jinga. Tusiwe mababa-jinga.

Kuna watu wamemwaga povu hapa. Nguo zimeniishia
 
Labda Kuna mtu unakusudia kumtukana hapa vinginevyo umejibu kichuki zaidi kwa hiyo naomba uelewe kuwa kuoa ni ibada Na kuzaa ni majaaliwa ya mungu wangapi wana wake lkn hawajazaa Yaani wagumba Na wangapi wanabaka. Na wamejaza watoto

kuoa bila utaratibu ni upumbavu. Haina tofauti na wanyama. Kila kitu kwenye maisha ni ibada ila usipofuata utaratibu ni upumbavu
 
Mkuu inauma sana kuona tabia hii ikiendekezwa katika jamii. Amini nakuambia ukifanya kazi vizuri ujanani na kuwekeza uzeeni utakuwa msaada mkubwa kwa watoto na wajukuu zako wasio wepesi wa kuchangamkia fursa
Nadhani hapo nimekuelewa kwamba kila mtu(mwanaume) apambane kwa nafasi yake kujiwekea akiba ya uzeeni,kwa hiyo hata watoto wa kiume hakuna kuwawekea utajiri uliopambana kupata,na wao wapambane watengeneze za kwao (si ndiyo uanaume!???)

Sasa ukipambana ukawaachia wao watapambanaje wakati wewe umeshapambana kwa niaba yao???

Vijana wa leo,pambaneni kujiandalia uzee wenu,watoto wenu nao watapambana kupata vyao,miradi yako komaa nayo mwenyewe,na watoto wako watapambana kutafuta miradi yao!!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…