Hakuna haja ya kuandika Wosia kama Mahakama inaubatilisha

Sexless

JF-Expert Member
Mar 11, 2017
21,563
50,410
Tunaaminishwa kwamba ili kuondoa migogoro ya kugombea mali za Marehemu ni muhimu kuandika wosia.

Maana ya wosia: refers to the document written by a testator that details what is to happen to property owned by that testator upon death.

Kwa mantiki hiyo wosia ni matakwa ya mwenye mali kuamua ibakie kwa nani mara atakapokuwa amepumzika kwa amani. Sasa kwanini kuna mtu au taasisi inaingilia matakwa hayo?

Kilichofanywa na mahakama kwa Jacqueline Mengi kutengua wosia wa Mzee Mengi, ndiyo kinawapa nguvu familia ya Mrema kumfanyia vurugu mjane wake.

Mapendekezo:
Itungwe sheriaya ya kuzuia mtu mzima(miaka 25+) kugombea/kupewa mali za marehemu hata kama ni mtoto wa kuzaliwa.

Swali: Kama Mahakama inaweza kutengua wosia kizembe namna hii kuna haja gani ya kuandika wosia?
 
Wachaga shikilieni happo hapo,

Mmetusaidia sana kunyoosha Hawa wajasilia mwili sampo za kina mtoa mada

Ukiandika wosia kopi baki nayo kopi nyengine peleka mahakamani na shahidi kazi imeisha hapo
 
Watanzania wanalazimisha mifumo ya Kikristu lkn hawailewi, wanataka kuitumia inapowanufaisha, kwa kifupi Wakristu au Wakristu wengi Tanzania bado ni wapagani hata kama hawataki kukubali na wanakwenda Kanisani kila siku lkn ukweli ni kwamba wengi hawako tayari kuuishi Ukristu au labda niseme hawauelewi bado na ndiyo maana Wanaume wengi wanaojiita Wakristu Tanzania wamezaa nije ya Ndoa na wanatetea polygamy!
Hakuna neno sipendi kulisikia kama WAKRISTU badala ya WAKRISTO
 
Ila tuwe wakweli tu! Ishu ya Doreen Wa Mrema ina makanganyiko. Yaani watu wameishi miezi kadhaa!! Mwanamke kamkuta mzee wa watu na mali zake, halafu leo na yeye apange mstari kudai mirathi!!

The same to Jackline Ntuyabaliwe! Amemkuta Mzee Mengi na mali zake alizochuma na mke wake wa kwanza, pamoja na watoto wake! Leo anakuja na sound za kutaka kumiliki kirahisi tu, kila kitu!! Kisa amezaa na marehemu watoto wawili mapacha!!

Wosia wa aina hii lazima ulete tu utata. Ifikie wakati tujifunze kutafuta vya kwetu, huku tukiwa na wenzi wetu. Mambo ya kitumia njia za mkato, hayana tija kwenye hii dunia ya kidijitali.
 
Hivi kwa mfano mimi mzee wangu ana miliki duka na nimekuwa nikilisimamia duka la mzee toka nikiwa na umri wa miaka 14 mpaka sasa nina miaka 24, miaka 10 yote mzee hajanilipa kama muuza duka ww unadhani nimeingiza bei gan kama faida kwa mzee

Haya basi miaka yote hiyo mama yangu anapika chakula anaenda dukan kuuza pia kwa miaka 30 iliyopita imetokea mama kafariki bahati mbaya mzee akakuoa ww mtoa mada umekuta kila kitu kipo vzr hujui sisi watoto, mama (marehemu) na mzee (marehemu) tumesota kiasi gani kuzipata mali hizo

Umeolewa na mzee umekaa miaka miwili mzee kafariki, kweli hata huruma huna unataka kuwa mrithi wa mali huoni kama huo ni utapeli?

Ulithi nini hapo? Bahati mbaya wazee wetu nao hawajui kama hamna mapenzi kwao bali mmefuata pesa, nataman itokee mzee mmoja aoe binti mdogo wakubaliane kuanza upywa (mali zibaki kwa familia muanze upya kutafuta kingine)
 
Tunaaminishwa kwamba ili kuondoa migogoro ya kugombea mali za Marehemu ni muhimu kuandika wosia.

Maana ya wosia: refers to the document written by a testator that details what is to happen to property owned by that testator upon death.

Kwa mantiki hiyo wosia ni matakwa ya mwenye mali kuamua ibakie kwa nani mara atakapokuwa amepumzika kwa amani. Sasa kwanini kuna mtu au taasisi inaingilia matakwa hayo? Kilichofanywa kwa Jacqueline Mengi kutengua wosia wa Mzee Mengi, ndiyo kinawapa nguvu familia ya Mrema kumfanyia vurugu mjane wake.

Mapendekezo:
Itungwe sheriaya ya kuzuia mtu mzima(miaka 25+) kugombea/kupewa mali za marehemu hata kama ni mtoto wa kuzaliwa.

Swali: Kama Mahakama inaweza kutengua wosia kizembe namna hii kuna haja gani ya kuandika wosia?
Hilo nalo neno
 
Wachaga shikilieni happo hapo,

Mmetusaidia sana kunyoosha Hawa wajasilia mwili sampo za kina mtoa mada

Mtoa mada anabanduliwa kitambo sana, kuna mada yake nyingine analalamika ameachwa na mimba juu.
 
Ila tuwe wakweli tu! Ishu ya Doreen Wa Mrema ina makanganyiko. Yaani watu wameishi miezi kadhaa!! Mwanamke kamkuta mzee wa watu na mali zake, halafu leo na yeye apange mstari kudai mirathi!!

The same to Jackline Ntuyabaliwe! Amemkuta Mzee Mengi na mali zake alizochuma na mke wake wa kwanza, pamoja na watoto wake! Leo anakuja na sound za kutaka kumiliki kirahisi tu, kila kitu!! Kisa amezaa na marehemu watoto wawili mapacha!!

Wosia wa aina hii lazima ulete tu utata. Ifikie wakati tujifunze kutafuta vya kwetu, huku tukiwa na wenzi wetu. Mambo ya kitumia njia za mkato, hayana tija kwenye hii dunia ya kidijitali.

Unaweza kuandikia wosia kwa yeyote umtakaye.

Kama mke mliyefunga ndoa halali hawezi kurithi na unasema atafute chake vp ndugu ambao nao wanagombania wao hawatakiwi kutafuta vyao? Watoto watu wazima hawatakiwi kutafuta vyao? Kumbuka Mengi ana watoto wawili na Jacq.

Mzee Mrema kaoa baada ya mke wake wa kwanza kufariki I believe na watoto wake washakua watu wazima, ulitaka mali amuachie nani? Ndugu wanatokea wapi kupinga wosia? Hawapaswi kuwa na vyao?

Mahakama za bongo are opening a can of worms kwa kubatilisha mirathi.
 
Ndugu mtoa mada, napenda kukupongeza kwa kutoa mada nzuri, Kwa hakika maoni yako ni mazuri sana.

Lakini, Kabla ya kufikia hitimisho lako yatupasa tukumbuke kuwa mara nyingi mahakama za Tanzania zimekuwa zikiheshimu mapendekezo ya marehemu juu ya nani apewe nini kwenye mali zake.

Mara nyingi mgogoro huwa inatokea pale inapoonekana wazi kabisa hata Kwa mtu wa tatu (Reasonable man test) kuwa mgawanyo wa mali aliofanya marehemu ni wa ajabu na mtu yeyote mwenye akili ya kawaida tu asingeweza kufanya hivyo.

Mfano katika hali ya kawaida mtu hawezi kuacha kuwarithisha wanae wa kuwazaa mali zake na badala yao amrithishe Jirani au mke mdogo pekee, katika akili ya kawaida hii inakataa.Ndo maana hata sheria yenyewe mfano sheria za kimila zinakataza kum disinherit mwanao wa kumzaa isipokuwa Kwa sababu zifuatazo; Awe alitembea na mama yake (mke wako),Awe alitaka kukuua Ili arithi Mali,Awe hakukuhudumia wakati unaumwa haliyakuwa uwezo alikuwa nao.

Lakini pia endapo mahakama itajiridhisha wosia ulikuwa una mapungufu ya kisheria au labda mtoa wosia hakuwa katika hali nzuri ya kiakili,mahakama huingilia kati ili kulinda maslahi ya watu wengine waliotakiwa kuwa wafaidika.

KWENYE ISSUE YA MAREHEMU MREMA.

Kwa kuwa bado ni tetesi, Kwa kiasi kikubwa tunazoandika hapa ni hisia tu.

Labda inawezekana wosia wa mzee Mrema umeacha mali nyingi Kwa bi mdogo na haujaacha chochote Kwa Watoto. Kiubinadamu hata kama watoto tayari ni wakubwa na wana mali zao lazima itawauma na watachallenge huo wosia na wanaweza hata kuutilia shaka kama umeandikwa na baba yao.

Lakini pia Kwa sasa Kuna trend mbaya inaendelea ya mabinti wadogo kuolewa na vikongwe, Kwa kiasi kikubwa jamii hutengeneza dhana kuwa mabinti hao hufuata Mali, Kama itakuwa si kweli na badala yake hufuata mapenzi tujaribu kukuuliza kwanini mzee akiondoka tu wanaanza kugombea Mali. Kama ulimfuata mtu na mtu huyo hayupo kwanini usiondoke kimya kimya tu bila kudai chochote?

Wanaume tuache kuandika wosia tukiwa vifuani Kwa wake zetu (Joke).
 
Back
Top Bottom