Zitto
Former MP Kigoma Urban
- Mar 2, 2007
- 1,562
- 10,880
Hakuna Diplomasia Bila Wanadiplomasia: Tuna Uhaba Mkubwa wa Watumishi Kwenye Balozi Zetu
[Sehemu ya Tatu ya Hotuba ya ndugu Kabwe Z. Ruyagwa Zitto (MB) Juu ya Bajeti ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kwa mwaka 2018/19]
Mheshimiwa Spika
Msingi wa tano wa Sera ya Mambo ya Nje ya Tanzania unatutaka tushirikiane kikamilifu na Nchi, Mashirika pamoja na Taasisi mbalimbali katika nyanja za Diplomasia, Siasa, Uchumi, Utaalam na Teknolojia. Wizara hii ina jukumu la kubuni na kusimamia utekelezaji wa misingi yote ya Sera yetu ya Mambo ya Nje.
Pia Wizara hii pia ina jukumu la kusimamia na kuratibu mahusiano kati ya Tanzania na nchi pamoja na mashirika mbalimbali. Utimizaji wa jambo hilo unafanyika kupitia balozi zetu zilizotapakaa kwenye nchi mbalimbali ulimwenguni. Kwa sasa ufanisi wetu si mkubwa kwa sababu ya uhaba wa watumishi kwenye balozi zetu mbalimbali duniani.
Kwa wastani ukimuondoa Balozi, kila kituo cha Ubalozi wetu nje ya nchi kinapaswa kuwa na Mhasibu, mtu wa TISS/Mwambata wa Jeshi na pamoja na Mwanadiplomasia (FSO). Vituo vingi vya balozi zetu havina kabisa Maafisa wa Diplomasia (FSO’s). Wale wachache waliokuwepo awali walirudishwa nchini kwa sababu mbalimbali (ikiwemo kumaliza muda wao wa utumishi Nje ya Nchi). Tumerudisha watu bila kupeleka mbadala wao.
Kwenye balozi zetu mbalimbali watendaji hasa wa kazi za Kibalozi na kidiplomasia ni hawa maafisa wa Diplomasia (FSO’s). Sasa kwa uhaba huu tunawezaje kufanya Diplomasia ya nchi yetu? Hiyo Diplomasia ya Uchumi tunaifanyaje bila kuwa na hao Wanadiplomasia?
Nitatoa tu mfano wa balozi zetu chache ulimwenguni. China, nchi ambayo ni mshirika wetu mkubwa kidiplomasia na kiuchumi, hatuna kabisa FSO huko, labda ndio sababu mauzo yetu kwenda China yameshuka mno, maana biashara ya nje ni Diplomasia, sasa wakati Spika unamtaka ndugu yangu Mwijage asafiri, ni nani atakayemuandalia hiyo mikutano ya kupata wawekezaji huko China kama hatuna FSO hata mmoja? Wenzetu Uganda wana FSO’s 8 huko China, Kenya na Sudan wao wanao 9 Kila mmoja.
Nchi nyengine ambayo hatuna kabisa FSO ni Ethiopia - Makao Makuu ya AU, utaona tunavyodharau nafasi yetu katika Afrika. Pia hatuna FSO Afrika Kusini, nchi rafiki na moja ya zenye uchumi mkubwa Afrika, hatuna kabisa FSO Ujerumani - Nchi kubwa zaidi kiuchumi katika Umoja wa Ulaya (EU). Hata India ambako tangu Bunge lianze wabunge tunalalamikia kukosa soko la mbaazi kutoka huko nako hatuna FSO hata mmoja. Tumeufanya kuwa ubalozi wa kupokea wagonjwa tu.
Nchi za Brics (ukiondoa China, India na Afrika Kusini ambazo hatuna kabisa FSO’s) zilizobaki, Brazil na Urusi tuna FSO mmoja mmoja tu. Hata DRC Congo - Nchi ambayo zaidi ya theluthi moja ya mizigo ya Transit inayopita kwenye bandari ya Dar inatoka, nayo tuna FSO mmoja tu tofauti na watatu ilivyozoeleka. Kenya - Nchi ya Afrika Mashariki tunayofanya nayo biashara zaidi nayo ina FSO mmoja tu.
Hali iko hivyo karibu katika balozi zetu nyingi ulimwenguni. FSO’s ndio maafisa hasa waliofundwa na kupikwa kutekeleza Sera yetu ya mambo ya Nje. Foreign Service Officers (FSO’s) ndio diplomats (wanadiplomasia wetu). Kama hawapo vituoni, na hatuwatumii maana yake hatufanyi diplomasia, na kwa kuangalia mbali tunaua diplomasia yetu.
Mimi sitapitisha bajeti hii mpaka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa itakaponihakikishia kuwa itapeleka Maafisa wa Diplomasia (FSO’s) katika vituo ambavyo hatuna kabisa na pia kuwaongeza katika vile vituo ambavyo wako wachache.
Kabwe Z. Ruyagwa Zitto
Mbunge, Kigoma Mjini
Kiongozi wa Chama, ACT Wazalendo
Bungeni Dodoma
Mei 23, 2018