Hakuna Diplomasia Bila Wanadiplomasia: Tuna Uhaba Mkubwa wa Watumishi Kwenye Balozi Zetu

Zitto

Former MP Kigoma Urban
Mar 2, 2007
1,562
10,879
Hakuna Diplomasia Bila Wanadiplomasia: Tuna Uhaba Mkubwa wa Watumishi Kwenye Balozi Zetu

[Sehemu ya Tatu ya Hotuba ya ndugu Kabwe Z. Ruyagwa Zitto (MB) Juu ya Bajeti ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kwa mwaka 2018/19]

Mheshimiwa Spika

Msingi wa tano wa Sera ya Mambo ya Nje ya Tanzania unatutaka tushirikiane kikamilifu na Nchi, Mashirika pamoja na Taasisi mbalimbali katika nyanja za Diplomasia, Siasa, Uchumi, Utaalam na Teknolojia. Wizara hii ina jukumu la kubuni na kusimamia utekelezaji wa misingi yote ya Sera yetu ya Mambo ya Nje.

Pia Wizara hii pia ina jukumu la kusimamia na kuratibu mahusiano kati ya Tanzania na nchi pamoja na mashirika mbalimbali. Utimizaji wa jambo hilo unafanyika kupitia balozi zetu zilizotapakaa kwenye nchi mbalimbali ulimwenguni. Kwa sasa ufanisi wetu si mkubwa kwa sababu ya uhaba wa watumishi kwenye balozi zetu mbalimbali duniani.

Kwa wastani ukimuondoa Balozi, kila kituo cha Ubalozi wetu nje ya nchi kinapaswa kuwa na Mhasibu, mtu wa TISS/Mwambata wa Jeshi na pamoja na Mwanadiplomasia (FSO). Vituo vingi vya balozi zetu havina kabisa Maafisa wa Diplomasia (FSO’s). Wale wachache waliokuwepo awali walirudishwa nchini kwa sababu mbalimbali (ikiwemo kumaliza muda wao wa utumishi Nje ya Nchi). Tumerudisha watu bila kupeleka mbadala wao.

Kwenye balozi zetu mbalimbali watendaji hasa wa kazi za Kibalozi na kidiplomasia ni hawa maafisa wa Diplomasia (FSO’s). Sasa kwa uhaba huu tunawezaje kufanya Diplomasia ya nchi yetu? Hiyo Diplomasia ya Uchumi tunaifanyaje bila kuwa na hao Wanadiplomasia?

Nitatoa tu mfano wa balozi zetu chache ulimwenguni. China, nchi ambayo ni mshirika wetu mkubwa kidiplomasia na kiuchumi, hatuna kabisa FSO huko, labda ndio sababu mauzo yetu kwenda China yameshuka mno, maana biashara ya nje ni Diplomasia, sasa wakati Spika unamtaka ndugu yangu Mwijage asafiri, ni nani atakayemuandalia hiyo mikutano ya kupata wawekezaji huko China kama hatuna FSO hata mmoja? Wenzetu Uganda wana FSO’s 8 huko China, Kenya na Sudan wao wanao 9 Kila mmoja.

Nchi nyengine ambayo hatuna kabisa FSO ni Ethiopia - Makao Makuu ya AU, utaona tunavyodharau nafasi yetu katika Afrika. Pia hatuna FSO Afrika Kusini, nchi rafiki na moja ya zenye uchumi mkubwa Afrika, hatuna kabisa FSO Ujerumani - Nchi kubwa zaidi kiuchumi katika Umoja wa Ulaya (EU). Hata India ambako tangu Bunge lianze wabunge tunalalamikia kukosa soko la mbaazi kutoka huko nako hatuna FSO hata mmoja. Tumeufanya kuwa ubalozi wa kupokea wagonjwa tu.

Nchi za Brics (ukiondoa China, India na Afrika Kusini ambazo hatuna kabisa FSO’s) zilizobaki, Brazil na Urusi tuna FSO mmoja mmoja tu. Hata DRC Congo - Nchi ambayo zaidi ya theluthi moja ya mizigo ya Transit inayopita kwenye bandari ya Dar inatoka, nayo tuna FSO mmoja tu tofauti na watatu ilivyozoeleka. Kenya - Nchi ya Afrika Mashariki tunayofanya nayo biashara zaidi nayo ina FSO mmoja tu.

Hali iko hivyo karibu katika balozi zetu nyingi ulimwenguni. FSO’s ndio maafisa hasa waliofundwa na kupikwa kutekeleza Sera yetu ya mambo ya Nje. Foreign Service Officers (FSO’s) ndio diplomats (wanadiplomasia wetu). Kama hawapo vituoni, na hatuwatumii maana yake hatufanyi diplomasia, na kwa kuangalia mbali tunaua diplomasia yetu.

Mimi sitapitisha bajeti hii mpaka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa itakaponihakikishia kuwa itapeleka Maafisa wa Diplomasia (FSO’s) katika vituo ambavyo hatuna kabisa na pia kuwaongeza katika vile vituo ambavyo wako wachache.

Kabwe Z. Ruyagwa Zitto
Mbunge, Kigoma Mjini
Kiongozi wa Chama, ACT Wazalendo
Bungeni Dodoma
Mei 23, 2018
 
Mkuu Malcom Lumumba,

Kwanza ahsante kwa kunikaribisha!

Niseme tu kwamba, hii ni very interesting subject ambayo inafaa kujadiliwa kwa mapana na marefu lakini wacha tu tuchokoze mada !!

Kwanza, kuna dhana ambayo watu tunashindwa kwenda nayo na wakati. Zama za akina Nyerere, dunia ilikuwa inazungumzia Uhusiano wa Kimataifa na ndio maana hata wizara yetu ilikuwa inaitwa Wizara ya Mambo ya Nje na Uhusiano wa Kimataifa!

Kinyume chake, zama hizi watu wanazungumzia Ushirikiano wa Kimataifa na ndio maana hata jina la wizara nalo limebadilika na kuwa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa (forget about EAC stuff)

Ni Uhusiano vs Ushirikiano... hizi ni dhana mbili tofauti! Ni dhana ambazo pia zilitakiwa kuakisi aina ya maofisa wetu huko kwenye balozi! Lakini kwa bahati mbaya kabisa, placement ya mabalozi na maafisa ubalozi haizingatii dhana mpya ya "Ushirikiano wa Kimataifa" bali inazingatia dhana ile ile ya akina Nyerere ya Uhusiano wa Kimataifa!

Tunapozungumzia ushirikiano hapa tunazingatia faida za kiuchumi wakati tunapozungumzia uhusiano tunaangalia sana faida za kisiasa, undugu, kijamii n.k! Kwamba, no matter what SADC ni ndugu zetu... tunaweza kutumia hadi senti yetu ya mwisho kuwapigania... hapa tunazungumzia international relation/uhusiano wa kimataifa na SADC!!

But the question is (mfano): Are SADC Members worthy economically?

Jibu utakalopata hapo juu ndio linalotakiwa ku-determine upeleke maofisa wa aina gani na kwa kipaumbele kipi!!

Kinyume chake, unaweza kurudi kwa nchi kama Israel!

Hapa unaweza kuiita Israel kwa majina yote mabaya... zimwi, muuaji, chinja chinja, dhalimu n.k!!

But the very same question tutatakiwa pia kujiuliza hapa: Is it worth economically?
 
Hakuna Diplomasia Bila Wanadiplomasia: Tuna Uhaba Mkubwa wa Watumishi Kwenye Balozi Zetu

[Sehemu ya Tatu ya Hotuba ya ndugu Kabwe Z. Ruyagwa Zitto (MB) Juu ya Bajeti ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kwa mwaka 2018/19]

Mheshimiwa Spika

Msingi wa tano wa Sera ya Mambo ya Nje ya Tanzania unatutaka tushirikiane kikamilifu na Nchi, Mashirika pamoja na Taasisi mbalimbali katika nyanja za Diplomasia, Siasa, Uchumi, Utaalam na Teknolojia. Wizara hii ina jukumu la kubuni na kusimamia utekelezaji wa misingi yote ya Sera yetu ya Mambo ya Nje.

Pia Wizara hii pia ina jukumu la kusimamia na kuratibu mahusiano kati ya Tanzania na nchi pamoja na mashirika mbalimbali. Utimizaji wa jambo hilo unafanyika kupitia balozi zetu zilizotapakaa kwenye nchi mbalimbali ulimwenguni. Kwa sasa ufanisi wetu si mkubwa kwa sababu ya uhaba wa watumishi kwenye balozi zetu mbalimbali duniani.

Kwa wastani ukimuondoa Balozi, kila kituo cha Ubalozi wetu nje ya nchi kinapaswa kuwa na Mhasibu, mtu wa TISS/Mwambata wa Jeshi na pamoja na Mwanadiplomasia (FSO). Vituo vingi vya balozi zetu havina kabisa Maafisa wa Diplomasia (FSO’s). Wale wachache waliokuwepo awali walirudishwa nchini kwa sababu mbalimbali (ikiwemo kumaliza muda wao wa utumishi Nje ya Nchi). Tumerudisha watu bila kupeleka mbadala wao.

Kwenye balozi zetu mbalimbali watendaji hasa wa kazi za Kibalozi na kidiplomasia ni hawa maafisa wa Diplomasia (FSO’s). Sasa kwa uhaba huu tunawezaje kufanya Diplomasia ya nchi yetu? Hiyo Diplomasia ya Uchumi tunaifanyaje bila kuwa na hao Wanadiplomasia?

Nitatoa tu mfano wa balozi zetu chache ulimwenguni. China, nchi ambayo ni mshirika wetu mkubwa kidiplomasia na kiuchumi, hatuna kabisa FSO huko, labda ndio sababu mauzo yetu kwenda China yameshuka mno, maana biashara ya nje ni Diplomasia, sasa wakati Spika unamtaka ndugu yangu Mwijage asafiri, ni nani atakayemuandalia hiyo mikutano ya kupata wawekezaji huko China kama hatuna FSO hata mmoja? Wenzetu Uganda wana FSO’s 8 huko China, Kenya na Sudan wao wanao 9 Kila mmoja.

Nchi nyengine ambayo hatuna kabisa FSO ni Ethiopia - Makao Makuu ya AU, utaona tunavyodharau nafasi yetu katika Afrika. Pia hatuna FSO Afrika Kusini, nchi rafiki na moja ya zenye uchumi mkubwa Afrika, hatuna kabisa FSO Ujerumani - Nchi kubwa zaidi kiuchumi katika Umoja wa Ulaya (EU). Hata India ambako tangu Bunge lianze wabunge tunalalamikia kukosa soko la mbaazi kutoka huko nako hatuna FSO hata mmoja. Tumeufanya kuwa ubalozi wa kupokea wagonjwa tu.

Nchi za Brics (ukiondoa China, India na Afrika Kusini ambazo hatuna kabisa FSO’s) zilizobaki, Brazil na Urusi tuna FSO mmoja mmoja tu. Hata DRC Congo - Nchi ambayo zaidi ya theluthi moja ya mizigo ya Transit inayopita kwenye bandari ya Dar inatoka, nayo tuna FSO mmoja tu tofauti na watatu ilivyozoeleka. Kenya - Nchi ya Afrika Mashariki tunayofanya nayo biashara zaidi nayo ina FSO mmoja tu.

Hali iko hivyo karibu katika balozi zetu nyingi ulimwenguni. FSO’s ndio maafisa hasa waliofundwa na kupikwa kutekeleza Sera yetu ya mambo ya Nje. Foreign Service Officers (FSO’s) ndio diplomats (wanadiplomasia wetu). Kama hawapo vituoni, na hatuwatumii maana yake hatufanyi diplomasia, na kwa kuangalia mbali tunaua diplomasia yetu.

Mimi sitapitisha bajeti hii mpaka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa itakaponihakikishia kuwa itapeleka Maafisa wa Diplomasia (FSO’s) katika vituo ambavyo hatuna kabisa na pia kuwaongeza katika vile vituo ambavyo wako wachache.

Kabwe Z. Ruyagwa Zitto
Mbunge, Kigoma Mjini
Kiongozi wa Chama, ACT Wazalendo
Bungeni Dodoma
Mei 23, 2018
Mh Zitto, sasa wakisema wanapeleka ili upitishe na kumbe hawatapeleka Utafanyaje?Kwa sababu hata bajet zao hazitakuwepo huko
 
Ukishazi-profile hizi nchi ndipo pia utaangalia ni mabalozi na maofisa wa aina gani unatakiwa kuwapeleka huko!

Kama Israel is more worth economically than SADC, then, for international cooperation/ushirikiano wa kimataifa unaweka pembeni u-monster wake (but with caution) na kutoa priority ya masuala ya kibalozi kwa Israel over our SADC brothers!

Tutaendelea ku-maintain our relation/uhusiano with our SADC brothers kwa sababu undugu haufi.

Kinyume chake, tutawekeza nguvu zetu za Kidiplomasia kwa global monsters like Israel provided tunafahamu they're worthy economically na kuangalia ni maafisa wa aina gani tunatakiwa kuwa nao kule!!

Sasa tatizo ni pale, unapochukua maafisa wenye sifa (sio za elimu) za kuwa ubalozini Malawi unawapeleka Israel au China au Marekani!!

Maafisa wetu wengi kama sio wote wanaweza kuitumikia dhana ya Uhusiano badala ya Ushirikiano!

Ingawaje Balozi sio Mtendaji Mkuu still huwezi kumchukua mtu ambae is completely politician asiye na element zozote za kibepari na kibeberu na kumpeleka kwenye "strategic" embassies kama China, US, au UK!!

Nchi kama China tulitakiwa kuwa na maofisa ambao ni " economic monsters" na ikibidi wale wenye uzoefu na corporate culture!

Maofisa ambao kipaumbele chao ni kuimarisha ushirikiano na China na sio kuimarisha uhusiano!! Maofisa wasioona taabu kuanzisha na kuimarisha ushirikiano na "mazimwi" wengine duniani provided kuna maslahi kwetu na sio ambao hakuna wanachoweza zaidi ya kuimarisha uhusiano!!

Even at family level, hivi ndivyo inavyotokea!!

Unamwacha mdogo wako baba mmoja, mama mmoja (International Relations) anapiga msoto kwa sababu ni hopeless na unaenda kushirikiana kutengeneza pesa na mtu baki mliyekutana ukubwani (International Cooperation) kwa sababu anajitambua!

Hata hivyo, c kwamba humpendi mdogo wako, la hasha... ni kwavile s/he's not the right person in hustling!!

Na wala huyu Partner ambae ni mtu baki asijichanganye akadhani, kwenye mazingira ya hatari you can choose him/her over your brother/sister... we're only partners!
 
Mkuu Malcom Lumumba, mimi nina mawazo ya kibepari with minor socialism elements, no wonder nilianza kuhitilafiana na JPM a second alipoanza kucheza na private sector!

Leo hii, ningekuwa na maamuzi, basi baadhi ya balozi zetu huko duniani zingegeuka kuwa kama Tanzania Investment Centers!! Big brain kama za akina Malcom Lumumba ningezipeleka huko! Hata kama hazina uzoefu na corporate culture, zingeenda huko kutengeneza chemistry na za watu wenye uzoefu na corporate culture or at least, with corporate mind ili kupeleka business and other economic opportunities back home!

Ili kuto-sound too commercial, ningejaza vyeo kama Mwambata wa Utalii, Mwambata wa Teknolojia, Mwambata wa Biashara, n.k!! Lakini kwavile pia tupo kibizinez zaidi, lazima KPI zetu zingekuwa ni zile ambazo ni commercial oriented huku tukizingatia matokeo... results oriented!

Kama Kenya inapata Watalii 500K kutoka USA, sitakuelewa ikiwa watalii waliongia Tanzania kutoka USA ni 100K na wewe upo pale ubalozini unalipwa pesa za wavuja jasho... sitakuelewa never, ever! Lazima tufanye mambo kwa target!!

Nakupa 3-5 years contract na idadi ya watalii iwe 500K>>>700K>>>1M>>>>

TunataklKama performance yako ni completely mbovu, miaka 3 ikiisha, we rudi tu Tanzania kuna shughuli zingine kibao za kufanya!!

Kama performance yako inaridhisha, endelea kutumikia Watanzania mwaka wa 4 & 5 kisha unafanyiwa general review itakayo-determine kama uendelee kubaki US au urudi Malawi kwavile performance yako inaridhisha, au urudi kabisa nyumbani ukafanye shughuli zingine!!!
 
asante kwa mada nzuri mh Zitto
sina uelewa mpana sana kwenye diplomasia,ila nina mashaka na utezi wa mabalozi ndio chanzo cha diplomasia iliyodorara kwa tanzania
teuzi nyingi za mabalozi sidhani kama zina tija(wengi ya wateuliwa ubalozi kama chaka la kuwa ficha baada ya kukataliwa na system au CCM)
 
Halafu unataka ku-brand Tanzania kama kivutio cha utalii. Aisee....
 
Kama Kenya inapata Watalii 500K kutoka USA, sitakuelewa ikiwa watalii waliongia Tanzania kutoka USA ni 100K na wewe upo pale ubalozini unalipwa pesa za wavuja jasho... sitakuelewa never, ever! Lazima tufanye mambo kwa target!!

Nakupa 3-5 years contract na idadi ya watalii iwe 500K>>>700K>>>1M>>>>

TunataklKama performance yako ni completely mbovu, miaka 3 ikiisha, we rudi tu Tanzania kuna shughuli zingine kibao za kufanya!!
Asante sana, Mkuu, naunga mkono hoja yako hasa hapa kweye hili...watu wapangiwe/wapewe kazi na target za matokeo ya kazi zao, kweli, wakichemsha wapangiwe kazi nyingine.
 
Kuna mdau juu hapo kazungumzia KPI, kuna haja ya kuwa na kipimo cha performance za watu wetu kwenye hizi wizara na ikiwezekana kazi ziwe za mikataba..
 
Uzi unaanzia sehemu ya tatu ya hotuba, kwa tunaotaka kuanza mambo mwanzo, sehemu ya kwanza na ya pili ziko wapi?
 
19 Reactions
Reply
Back
Top Bottom