Hakuna atakayeachia ngazi sakata la Escrow

Hakuna atakayeachia ngazi sakata la Escrow

Status
Not open for further replies.
Mapendekezo ya Zitto ya watu kuachia nyadhifa zao ni ya kishabiki na hayana mshiko, watu hawaachii tu nyadhifa zao kwa habari kama hizi ambazo hazina mshiko wa kisheria.

katika uwanja wa siasa, mtu anatakiwa kujiuzulu wadhifa wake kwa kuzingatia athari za kisiasa kwa chama chake na kwa taifa kwa ujumla. hapo mambo ya "kisheria" hayapo, wala mambo ya "haki ya mtu" hayapo. cheo ni dhamana, na hizo si nafasi za ajira kusema kwamba mtu anatetea haki yake. kuwajibika kisiasa ni kutokana na athari za kisiasa, wala siyo kusema haki ya mtu. mtu anatakiwa kuweka maslahi ya chama chake na ya taifa lake mbele, wala si maslahi binafsi. Pia, michakato ya kisheria inaweza kuchukua miaka kupata ufumbuzi wake, lakini kisiasa, inatakiwa maamuzi yafanyike, kumbuka mambo yakisiasa yana ratiba zake tofauti kabisa.

Kuna mengi sana ya kuchambua lakini tusubiri kesho, tusiandikie mate na wino upo. Ni matumaini yangu kuwa wote waliotajwa watapewa fursa ya kujibu. Na hapo ndipo mtamjuwa Chenge ni kichwa.

Ama kweli, tumeshaona kweli CHENGE NI KICHWA. bingwa wa kupiga fedha za walalahoi. kila skandali yumo...
 
Mnasikiliza lakini hamsikii, mnasoma lakini hamuelewi, Mna-matatizo makubwa sana, na twayajuwa yako wapi.

Huna unalolijuwa wewe kaa kimya. Huna tofauti na bibi-bomba mwenzio aliyefukuzwa kazi jana. Eti "Nikijiuzulu rais atanishangaa sana!: "!! Atakushangaa labda kwa kumpre-empty maamuzi yake ya kukufukuza! Nyambafff!!!
 
Wapi FaizaFoxy..???
Vipi kuhusu 'kuachia ngazi' kwa mawaziri..??
'Ulitabiri' kuwa hakuna waziri atakayeachia ngazi..??
 
Last edited by a moderator:
huyu bibi faiza yuko wapi na aliandika bumba hapa, leo amekimbia aibu. halafu huyu bibi nahisi sio mtanzania kwani mtanzania wa kweli hawezi kuwa anatetea maovu ambayo yanaweza kuliangamiza taifa
 
Kufanya kazi kwa mahaba na mazoea, na kunywa viroba kwa kujificha ficha ni tatizo kubwa la hawa watu wanaojiita watabiri au sijui wapiga ramli. Issue kubwa kama hii wanairahisha kama vile wao ndio wako kwenye kiti kile anachokalia mkuu wa nchi ikulu....kumbe pengine ni wafungua mageti tu.
 
Facts zipi zaidi, niliyosema na kuyatetea humu siku zote ndio hayo hayo aliyeyasema Kikwete, kipi hukukielewa nikuendelezee darsa.

Vipi ile lecture, ulikuwa unapiga porojo tu?
na waalaniwe wote ambao walitaka kuigeuza issue ya escrow kuwa ni ya kidini, na walaji wanatoka dini Fulani, kama kawaida yao na unafiki wao wa kila siku , baada ya jana, utawaona wako kimya wamelowa. sasa mimi nawauliza kwa nini wasiligeuze hall ya diamond kuwa kanisa , na muumini mkuu ni mukluk wa nchi. msiwe wanafiki nyie, hela hazirudi ng'oo na sio zenu kapikeni pilau
 
Wapi FaizaFoxy..???
Vipi kuhusu 'kuachia ngazi' kwa mawaziri..??
'Ulitabiri' kuwa hakuna waziri atakayeachia ngazi..??

Nipo nimejaa tele.

Nani kaachia ngazi? Tibaijuka hakuachia kaambiwa ondoka, hata mimi nimngemwambia aondoke, hajuwi maadili ya uongozi? ukipewa msaada kuna kanuni zake kwa watumishi wa umma.

Kama ni AG, huyo alishatangaza bungeni na alisema na kachukuwa majukumu yote kiume kabisa na ndivyo inavyotakiwa kuwa kama kosa hakuna lakini isiwe tabu mimi nnabeba majukumu kwa kuwa mimi ndiye niliyetoa maamuzi, kwanini wengine wawajibike?

Ukishayajuwa hayo, nenda kwenye mada ukaisome vizuri nilichokiandika kikuingie, usiwe na kiherehere cha kusoma kichwa cha mada ukauacha utumbo wa mada.

Cha msingi, naona Kikwete jana kafafanuwa vizuri sana, maazimio karibia yote kayafafanuwa na mengi kayapiga chini kidiplomasia kabisa.

Kikwete juu.
 
hapo kwenye Kikwete juu wala sikusupport

ila Tibaijuka hajaondolewa kwa sakata la ESCROW, ameondolewa kwa sababu ya maadili ya uongozi, amepokea kiwango kikubwa cha pesa bila kufuata utaratibu wa kudeclare,

JK Kumjumuisha huyu mama na mambo ya Escrow ni makosa, kuna watu walikuwa wako moja kwa moja kwenye huu ufisadi na wala hawajagusiwa kwenye hiyo hotuba yake na wazee wa Saigon
 
Faiza Foxy alikua sahihi. Hakukuwa na mtu wa kujiuzulu wala kuwajibika kwa linaloitwa sakata la eskrow. Msimamo wa Raisi hauna tofauti na msimamo rasmi wa serikali uliotolewa na wa waziri Muhongo na Werema bungeni na kupelekea Muhongo kuitwa muongo. Prof. Tibijuka ameponzwa na kiherehere chake cha kuongea na waandishi wa habari.
 
hapo kwenye Kikwete juu wala sikusupport

ila Tibaijuka hajaondolewa kwa sakata la ESCROW, ameondolewa kwa sababu ya maadili ya uongozi, amepokea kiwango kikubwa cha pesa bila kufuata utaratibu wa kudeclare,

JK Kumjumuisha huyu mama na mambo ya Escrow ni makosa, kuna watu walikuwa wako moja kwa moja kwenye huu ufisadi na wala hawajagusiwa kwenye hiyo hotuba yake na wazee wa Saigon

Wepi hao, mbona Kikwete kaelezea maazimio yote na kayachambuwa.

Hilo la Tibaijuka ndivyo ilivyo, yule mama kuondolewa hata mimi nimefurahi sana, alikuwa ni mzigo usiobebeka.

Siku nyingi ukifatiilia post zangu nilisema, huyu hafai kabisa.
 
Sawa humpendi lakini kama alikiuka miiko na maadili kama Kiongozi, ilikuwaje JK aje amtoe huku akimlink na issue ya Escrow?, angemtoa tu kwa muda wake bila kumuhusisha na hiyo Hotba, JK anataka kutufumba mambo tu, issue sio kuwafukuza watu uwaziri, issue ni kuwapeleka watu mahakamani, NGEREJA, CHENGE, NK wamastahili kesi
 
Wewe sasa unajaribu kuweka maneno yako kinywani mwangu, wapi nilisema simpendi? inahusu nini mambo ya kupendana na kutokupendana?

Nikimpenda au nisipompenda inasaidia nini kwenye kuongoza nchi?

Maazimio ya bunge ndiyo ya lim-link na escrow si Kikwete.
 
Siwezi kukubadirisha, na mahaba yako kwa JK, lakini Tibaijuka katolewa sadaka kwa issue ya Escrow, ili ionekane JK kafanya maamuzi, kulikuwa hakuna sababu ya kuongelea mambo ya Escrow na mwisho kumpiga chini waziri Tiba
 
Umekazana mahaba, mahaba yanhusu nini kwenye escrow?

Tibaijuka ndio kishavuna alichokipanda na bado ana majibu ya kuwajibu pccb na tume ya maadili.
 
Baada ya kusikiliza ripoti rasmi ya PAC iliyowasilishwa na Zitto Kabwe na Deo Filikunjombe nnadiriki kusema kuwa hakuna cha maana kwenye ripoti yao cha kuwafanya mawaziri kuwachia ngazi.

Ni drama tu lakini hakuna kipengele chochote cha sheria ambacho hakijibiki au kilichooneshwa kuwa kimekiukwa.

Hukumu ya Mahakama ni ya halali na haina utata na Zitto wala CAG wala TAKUKURU hawajaonesha kuwa ilikuwa ni batili au ya kughushi.

Zitto kapiga porojo nyingi sana kuliko ukweli, na mwanasheria yoyote mahiri anazisambaratisha hoja zake zote ndani ya nusu saa.

Zitto ametetea sana BoT lakini alichoshindwa kuelewa ni kuwa Bot kama wakala ndiye alitakiwa aridhike na vielelezo vyote kabla hajalipa na kama havijakamilika hawezi kutoa fedha. Zitto anasema eti Mwanasheria Mkuu wa Serikali ndiye alimuamuru Gavana hizo fedha zitolewe, toka lini Gavana wa benki anatoa fedha kwa amri ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali?

Utata wa IPTL na Standard Chartered ni huko-huko kwao si IPTL iliyokopa, iliyokopa ni Mechmar na Mechmar haiwezi jitokeza kwani imeshafilisika kisheria, Standard Chartered karata yao ya mwisho ni hii na hapa wamepata mwanya.

Nnasikitika kusema na nnaliona linakuja la Serikali kuingia gharama kubwa ya kulipa zaidi ya mara mbili au tatu hizi fedha ikiwa watafata akili za akina Zitto.

Nnashauri, wajadili hili suala bungeni lakini shauri liwachwe kesi kumi zilizopo mahakamani zinazoihusu IPTL zikamilike.

Mapendekezo ya Zitto ya watu kuachia nyadhifa zao ni ya kishabiki na hayana mshiko, watu hawaachii tu nyadhifa zao kwa habari kama hizi ambazo hazina mshiko wa kisheria.

Isitoshe, fedha zilizolipwa escrow si kamili, hizo zilizobaki zilizuiliwa kwanini? Jibu tutalipata kesho na ndilo litakalosambaratisha hoja ya kodi ya Zitto.

Kuna mengi sana ya kuchambua lakini tusubiri kesho, tusiandikie mate na wino upo. Ni matumaini yangu kuwa wote waliotajwa watapewa fursa ya kujibu. Na hapo ndipo mtamjuwa Chenge ni kichwa.

wGdNhqkCu5onwAAAABJRU5ErkJggg==

Soma uzi wako huu uliouanzisha na majibu ambayo umenijibu kule kwenye ''Tweets za binti wa tibaijuka"
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom