gambalakobe
Member
- Jul 1, 2015
- 55
- 74
Niliwahi kusema humu kuwa huwezi kuelewa tunachokilalamikia humu mitandaoni kuhusu Maamuzi mbali mbali ya kukurupuka yanafonywa na serikali mpaka uwe mhanga wa jambo fulani, nashukuru kadri siku zinavyosonga tunazidi kuelewana.
Jana rafiki yangu aliemaliza form 6 mwaka jana ila hakufanya vizuri, alikuwa amelipa ada ya miezi 6 kusoma 'bridging course' a.k.a kupigwa msasa ili apate sifa za kujiunga Degree ya UDAKTARI mwakani, sasa baada ya Ndalichako kutema cheche majuzi kuwa amefuta hizi kozi, jana alijikuta akiikana itikadi ya chama chake na kujikuta akipost status ya matusi dhidi ya chama kwa mara ya kwanza. Nilimsihi anywe maji kisha afute status maana milioni 7 hana na angefungwa,
Niseme tu hivi hakuna aliyezaliwa kuwa mkosoaji tu, hakuna mwenye MB za kuweka ili aposti negatives humu, hakuna anayelipwa mshahara kwa kukosoa, ila inabidi tu mda mwingine, fikiria watoto wa IFM waliovulishwa majoho katika ya sherehe kisa agizo la binadamu mmoja alie lala na kuamka asbh na kutamka, bila kushirikisha hata wadau.
Ufute mahakimu wa diploma na cheti, ufute kujiendeleza diploma kwenda degree wakati hata rais alianzia diploma hadi PhD
Busara inatakiwa katika maamuzi yagusayo maslahi ya taifa, hatuwezi kunyamaza na kuacha nchi iendeshwe kwa weledi wa mtu mmoja mmoja. Nchi imezidi matamko bwana! Ebo!!!!!!!