Hakuna aliye juu ya UKAWA sasa

Hakuna aliye juu ya UKAWA sasa

Magamba yameshikwa vibaya sasa yanapukutika kila nikiangalia taarifa ya habari ... CCM kwishnei
 
Tatizo ni kwamba,kuna watu wa ilmradi na watu wa misingi.
Dr Slaa kamwe sio mtu wa ilmradi.
Siamini hata kidogo kuwa ataondoka CHADEMA ila naamini kabisa hata kama alishiriki vikao vya kumleta Lowassa,binafsi hakuridhia.
Slaa bora abaki na msimamo ila uwe passive,vinginevyo ataleta hasara.

SLAA lazima awashikishe adabu CHADEMA
 
Dr.Slaa alivunjika mkono na hadi sasa ana ulemavu wa kudumu kwa sababu ya kuitetea chadema. yeye mwenyewe alipigwa na kuharibiwa mimba mwaka 2011 kwa sababu ya chadema halafu leo wanapuuzwa kama vile si chochote ndani ya chama.

Unajua mkuu R.B kuna watu wamekuja juzi cdm sasa wanataja kujifanya wajuaji kwel hawajui kustawi kwa CHADEMA kuna watu wamepoteza kazi,kupunguza marafk et2 sasa leo watu wanajiropokea tu
 
Watu hawapendi Dr. Slaa, wanapenda CCM isiendelee kubakia madarakani tena. Kama Slaa kwakukaa kimya kwake kutasaidia kuiondoa CCM madarakani ni sawa lakini kama itakuwa chanzo cha CCM kusalia madarakani wale waliomfanya Dr. Slaa apate umaarufu aliokuwanao leo lazima watauchukua umaarufu wake na kumuacha kama alivyokuwa. Ndo maana mimi nasema sio Mbowe, Lissu, Mnyika wala Sugu aliye juu ya UKAWA ni wananchi wapenda mageuzi tu, ndo maana hata hawakutaka kuhoji usafi wala ujio wa Lowassa chadema. Kama Slaa anataka kujipima ili aone kama ni maarufu au laa, hebu aendelee na msimamo wake wa kuuchuna. ZZK alikuwa maarufu sana chadema lakini alivyotoka chadema watu wameshaanza kumsahau kisiasa

Inasemekana siasa ni umalaya, lakini siyo kila mwanasiasa ni malaya.
 
''... Hiyo sabuni au brashi ya kumsafisha haipo hata Nakumatt ''
Hii ni hatari..
http://www.raiatanzania.co.tz/dk-slaa-natishwa/
 
naona umaeamua kijifariji na kujiliwaza kwa sasa lowassa ndiyo mmiliki wa chadema.

Chadema kwa sasa hawana ubavu wa kumnyoshea kidole lowassa na timu zake.

Lowassa kwa sasa ni chama ndani ya chadema.

Hukumuona mwenyekiti wa chadema taifa anavyo mnyenyekea lowassa mpaka anamsindikiza lowassa kwenye gari yake wakati yeye ni mwenyekiti wa chadema taifa.

Kiitifaki, lowassa inabidi amsindikize mwenyekiti wa chama taifa kwa sababu lowassa ndani ya chadema ni mwanachama tu na hana cheo chochote. Kwa sasa ni kinyume chake!

Pesa na umaarufu wake ndiyo unawafanya viongozi wakuu wa chadema wajishushe chini yake.

Money talks and money alone sets the entire world in.

duuh!..........
 
Ritz

Jamani, kama CDM imeingiliwa na kupoteza mwelekeo nadhani ndiyo furaha ya CCM, inakuwaje sasa jambo hili linawasumbua sana watu wa CCM? Hamdhani kuwa watu ambao hawajachagua upande wanaweza kupatwa na mashaka na jitihada zenu?
Kamanda, hii ni forum tujadili tu.
 
Last edited by a moderator:
Unajua mkuu R.B kuna watu wamekuja juzi cdm sasa wanataja kujifanya wajuaji kwel hawajui kustawi kwa CHADEMA kuna watu wamepoteza kazi,kupunguza marafk et2 sasa leo watu wanajiropokea tu
Mkuu chadema ni taasisi sio mtu mmojammoja, maana mabomu yakirushwa kwa Mbowe, Slaa, Lipumba , n.k hayampati Mbowe, Slaa wala Lipumba tu, yanatua pia hata kwa wanachama na mashabiki wa vyama hivyo, hivyo chadema haina mtu maarufu pekee ila chama, viongozi na wanachama wote kwa pamoja. Slaa anaweza kuondoka cdm lakini chama kikaendelea kuwepo. Tunaomba katibu wetu Dr. Slaa atambue uhusiano uliopo kati ya kuku, yai na mapumba. La msingi hapa Slaa anatuhitaji na sisi tunamuhitaji, na Lowassa kama yalivyo mapumba kwenye uhusiano wa kuku na yai anahitajika pia. Hakuna mshabiki atakayemuona Lowassa kuwa hafai kuja cdm kwasababu yeyote ile,maana Mbowe, Lipumba na Dr. Slaa kwa nyakati tofauti tulishawasimamisha kugombea urais miaka iliyopita lakini tulishindwa kuiondoa CCM, hivyo ujio wa UKAWA na Lowassa mwaka huu ndio mbinu nyingine mpya ya kujaribu kufikia lengo hilo. Kama Slaa atang'ang'ania kuwa yeye ndo apewe nafasi hiyo tena atakuwa anakosea na anatukosea sisi wafuasi wake pia.
 
sisi hatutaki ccm madarakani..kwa njia yoyote iwe haramu au .....
 
Mbowe alimpisha Slaa kugombea baada ya kuona ana mvuto na alitoka huko huko. Now its Lowassa. ukiangalia kwa upeo mdogo hutaelewa kinachofanyika. That is how politics works. sema kanunua chama sema kahonga watanzania wote sema ni fisadi (with no proofs) sema yupo above UKAWA, sema Zanzibar hawata kubali.. say it all. Lipumba sion Mpuuzi namna hiyo na viongozi wa UKAWA wameangalia in a bigger picture. Mwanzo ilikuwa Lissu katoka, Mdee katoka, Mnyika katoka, Slaa katoka.... tutaenda sawa tuu

Slaa haondoki, that is for sure. pigeni makelele tu. He is not that much predictable.
 
Nionavyo mimi ni kuwa, si haki na si sawa kumdhihaki na kumtukana au kumrushia lawama Dr. Slaa. Hakuna shaka wala wasiwasi nikisema Dr. amefanya kazi kubwa sana kuinyanyua CDM mpaka hapo ilipo, na mtu anaposema Dr. kinamsumbua madaraka au mke wake alikuwa ameji-tune kuwa first lady seriously is not fair at all!!! Yes,Dr. Slaa ikumbukwe ni binadamu wa kawaida, huumia na huumizwa kama mwanadamu awaye yote. Kilichofanyika hakikumpendeza sababu haikuwa sawa na makubaliano yao, hata kama tungekuwa sie tunaojua kuandika na kutoa lawama si ajabu tayari tungeshakimbilia Media kujitoa uanachama. Dr. Slaa amekuwa mtulivu,anatafakari na lazima atakuwa nafikiria from day one he joined CHADEMA mpaka hivi leo. Ni busara aachwe atafakari kama akili yake inavyomtuma.
Ushauri wangu tu kwa Dr. Slaa,asichukue uamzi kwa hasira na afikirie Tanzania kwanza kabla ya kufikiria CHADEMA. Ni vizuri awe na subira na ajue watanzania wengi wanamwamini na tutakuwa wanyimi wa fadhira tusipomshukuru kwa kazi kubwa alofanya kuusogeza upinzani toka ulikokuwa chini na kuupaisha juu kiasi hiki. Dr. Slaa ni vizuri ajitokeze tu na kuongea kuliko kuwa kimya, ni vizuri wakiongea viongozi wote wa CDM ngazi ya taifa wafikie maridhiano na tu kawaida ya demokrasia saa zingine huumiza lakini kama ni kwa maslahi ya wengi hata kama haukubariani na na issue iliyopo huna budi kwenda na wengi. Ila ni vizuri kutoa yake ya moyoni vikaoni, wala sidhani kama kutoonekana ndo kutaweza kusolve matatizo yaliyo ndani ya CDM.
Tena na tena, mzee wangu na baba yangu kama utapitia uzi huu, nakuomba tena kwa unyenyekevu mkubwa mno, angalia Tanzania kwanza, achana na maneno ya watu, tumekusema sana wewe na familia yako lakini hebu jitokeze tu mbele ya kikao na kwa vile ndo mkutano mkuu,toa yako ya moyoni ili usiendelee kuumia mzee wangu.
Naamini wewe ni mcha Mungu, kumbuka agizo la kusamehe saba mara sabini. Samehe wote akiwemo na EL uyaseme na uwe huru, usipojitokeza na kuyasema mbele ha hadhara ya mkutano mkuu,utabaki nayo moyoni yakikuumiza na kikristo ni dhambi.....acha dhambi iwe upande wao wewe jiepushe nayo!!!
 
Mkuu umesa kitu kizuri, unajua mzee Dr. Slaa kwenye sakata hili la EL hapaswi kusema sana kwabababu za conflict of interest zake. EL kahamia cdm na kupewa nafasi na ukawa kugombea urais kwa tiketi ya UKAWA kupitia chadema nafasi ambayo ni wazi ilikuwa ya Dr. Slaa. Hivyo kila kitu Slaa anachokisema kuhusu Lowassa watu ndani na nje ya chama na UKAWA wanakiona kwa kutumia jicho hilo la Slaa. Binafsi Slaa alipaswa kuendelea kuwa katibu mkuu shupavu wa chadema sawa na walivyo makatibu wakuu wenzake wa CCM, CUF, NCCR na NLD ili kuhakikisha chama na ukawa vinashika dola na kuingiza wabunge na madiwani wengi. Shida ya Slaa ni pale na yeye anavyotamani kuwa mgombea urais kupitia UKAWA. Lakini ukiangalia kwa karibu wanachama wanaounda UKAWA wako radhi kumsimamisha Lowassa kuliko Slaa, sasa kwanini Slaa aendelee kung'ang'ania kuwa Lowassa ni fisadi, atafanya hivyo hadi lini? YEYE ni katibu wa chama kwanini hakuamuru wanasheria wa chama wampeleke Lowassa mahakamani kwa kutumia ushahidi alionao mkononi? atamuita Lowassa fisadi hadi lini na kwa ushahidi gani? tungetegemea mtu anayetaka kuwa rais wa nchi asiwahukumu watu kwa tuhuma tu bali ushahidi wa kimahakama. Sasa Slaa amekazana kila siku Lowassa fisadi fisadi fisadi hadi lini? mahakamani anakwenda lini kumshitaki Lowassa? Jambo hili ndilo linalovunja hoja ya Dr. Slaa na kuonekana kuwa shida hapa sio ufisadi wa Lowassa bali urais uliopokonywa na EL. Kimkakati Lowassa ni bora kuliko Slaa katika nafasi ya urais. Mimi binafsi ninamheshimu sana Slaa, lakini nampenda Lowassa zaidi kama mbinu ya kisasa ya kuingusha CCM.
 
Kweli EL is now the king of Tz politics!

Aliwapelekesha ccm mpaka wakajikuta wanapata mgombea ambaye hawakuwa wamempanga.

Alipokatwa akaamua ku-defect na kuacha migongano ndani ya chama dola.

Alikohamia akasababisha sintofahamu hadi ukawa wakajikuta wanampata mgombea ambaye hawakuwa wamempanga.

Na huko nako hakuko salama, ni migongano.

Waliokuwa wanasema Dr. Slaa hafai kuwa mgombea wa ukawa leo wanakula matapishi yao kwamba eti, Dr. Slaa ndiyo pekee aliyekuwa anafaa kupeperusha bendera ya chadema.

Walipomkata EL walisema ni fisadi na mzigo kwa chama, sasa kahamia kambi ya pili, badala ya kushukuru mzigo umeondoka, bado wanamfuata hukohuko.

Hii hofu hii inasababishwa na nini? Kweli EL ni kiboko!

Sisi ambao hatuna vyama tunawashangaa na kuwahurumia wenye vyama vyao,
....we salute you EL.
 
conflict of interest ya Dr. Slaa kuhusu ujio wa Edo isitupotoshe UKAWA. EL kachukua nafasi ya urais ya Slaa utategemea nini hapo?
 
sasa kijipambanue kuwa ni chama cha wezi na walaghai, chama cha walio shindwa
 
Nashukuru kuwa Slaa ni mtu mzima tena mwenye hekima. Kuna watu humu ndani wametafuta sana afumbue kinywa chake ili wawe na sababu ya kukigawa Chadema lakini mwenyewe amekataa kusema. Hata huo ni ukomavu! Asante Dr. Slaa!
 
Mkuu umesa kitu kizuri, unajua mzee Dr. Slaa kwenye sakata hili la EL hapaswi kusema sana kwabababu za conflict of interest zake. EL kahamia cdm na kupewa nafasi na ukawa kugombea urais kwa tiketi ya UKAWA kupitia chadema nafasi ambayo ni wazi ilikuwa ya Dr. Slaa. Hivyo kila kitu Slaa anachokisema kuhusu Lowassa watu ndani na nje ya chama na UKAWA wanakiona kwa kutumia jicho hilo la Slaa. Binafsi Slaa alipaswa kuendelea kuwa katibu mkuu shupavu wa chadema sawa na walivyo makatibu wakuu wenzake wa CCM, CUF, NCCR na NLD ili kuhakikisha chama na ukawa vinashika dola na kuingiza wabunge na madiwani wengi. Shida ya Slaa ni pale na yeye anavyotamani kuwa mgombea urais kupitia UKAWA. Lakini ukiangalia kwa karibu wanachama wanaounda UKAWA wako radhi kumsimamisha Lowassa kuliko Slaa, sasa kwanini Slaa aendelee kung'ang'ania kuwa Lowassa ni fisadi, atafanya hivyo hadi lini? YEYE ni katibu wa chama kwanini hakuamuru wanasheria wa chama wampeleke Lowassa mahakamani kwa kutumia ushahidi alionao mkononi? atamuita Lowassa fisadi hadi lini na kwa ushahidi gani? tungetegemea mtu anayetaka kuwa rais wa nchi asiwahukumu watu kwa tuhuma tu bali ushahidi wa kimahakama. Sasa Slaa amekazana kila siku Lowassa fisadi fisadi fisadi hadi lini? mahakamani anakwenda lini kumshitaki Lowassa? Jambo hili ndilo linalovunja hoja ya Dr. Slaa na kuonekana kuwa shida hapa sio ufisadi wa Lowassa bali urais uliopokonywa na EL. Kimkakati Lowassa ni bora kuliko Slaa katika nafasi ya urais. Mimi binafsi ninamheshimu sana Slaa, lakini nampenda Lowassa zaidi kama mbinu ya kisasa ya kuingusha CCM.

KAVULATA
Mimi nitatofautiana na wewe kwa kitu kimoja hapa, Dr. Slaa sidhani kama suala la kuwa mgombea kupitia UKAWA ni issue kubwa kwake....!!! Hapa tatizo ni kwamba, Dr. amejisikia mpweke na kapuuzwa mno!!! YES hata ningekuwa mimi, tumempigia mtu kelele za mwizi mwizi na kuwaamiinisha watu kuwa mwizi,mara mtu katuambia huyu si mwizi tuanzishe urafiki nae...!!! Sijui umenielewa? Kwa haraka haraka hapa , nitamuomba huyu mwizi awaeleze watu tuliowaaminisha kuwa mwizi kuwa YEYE si mwizi, wamwelewe then tufanye nae urafiki.....nje ya hapo inaweza kuleta sintofahamu kwa mtu yeyote!!! Ndo maana kwa binafsi ya moyo wangu bila kuleta ushabiki wa aina yoyote, nmemwomba mzee wangu na baba yangu kwa vile ni mcha Mungu,akumbuke kusamehe saba mara sabini...awasamehe wote akiwemo na EL ili asijehesabiwa dhambi ya kutosamehe.... Kavulata ni kweli Dr. Slaa wamemkwaza, utoto wa mjini umetumika katika hili wala si misingi na maadili ya kichama kama ambavyo mzee wangu Dr. Slaa amekuwa akiyasimamia....hapa tusitetee mtu, maadili ya kichama yamekiukwa. Ingekuwa busara kwa wakubwa wa chama pia kuachana na mambo ya mitaa ya Samora, wamuombe msamaha mzee kwa ajili ya kunusuru chama na mshikamano uliojengeka. Wakati huu si wa kuruhusu sintofahamu ya aina yoyote iwe ndogo au kubwa....Mwenyekiti nmekuwa nikimwamini sana kwa busara, kama ataamua potelea mbali atawavunja moyo sana watanzania walokuwa wakimwanini....Asijekengeuka kwa u-mimi ni mwenyekiti na yeye ni katibu tu!!! Tutafeli na EL wetu. Ikumbukwe upande wa pili nao wanautumia sana huu ufa kupenyeza siraha za maangamizi, kama mwenyekiti shupavu na makini, asijejidanganya kuwa hata akiachia ufa huu na Lowasa wake wataitoa CCM...NEVER!!! na kama haamini ajaribu, tunahitaji umoja wa hali na mali, si kwa EL na Dr Slaa tu bali kwa kila atakaeonyesha utayari wa kuungana na sisi. Tuwe kimkakati na si kiutoto wa mjini...Bila ushirika ulio thabiti CDM na UKAWA ni ndoto kwenda magogoni.
 
kaka laiti kama watu wote wangekuwa na mawqzo.kma yako dr angeshatoa mamuzi!!
ila kwa kuwa kuna watu wanatazama hapa walipo tu hawawezi kugundua ulichosema!!!

narudia tena dharau,,matusi na kila aina ya kejeli hazitamshurutisha dr slaa kuongea jambo.
kwa maneno yenu mungi,okwiboban sunzu,,shardcole na vijana wengi wa bavicha mkiendelea na huu upuzi!!!haki ya mungu huyo masai wenu hatoboi hata kwa robo ya kura!!!
 
Hakuna mtu alie juu ya UKAWA isipokua tajiri LOWASA tu
 
Back
Top Bottom