Hakuna aliye juu ya UKAWA sasa

Hakuna aliye juu ya UKAWA sasa

kavulata

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Posts
16,252
Reaction score
16,171
Sitaki kuamini kama yupo mtu yeyote sasa ambaye anaweza kuwa yuko juu ya joto la matamanio ya watanzania wanaotaka mabadiliko ya uongozi wa nchi. Morali wa wananchi uko juu na matumaini yao yote yamebebwa na ukawa. Kila mtu ni lazima asome alama za nyakati na asome mioyo ya watanzania kwa sasa kuelekea October 2015.

Watanzania wako tayari kumsikiliza, kumheshimu na kumthamini mtu yeyote atakayewasaidia kuiangusha CCM October 2015 bila kujali rangi, kabila, dini, umaarufu wake wala itikadi ya chama anachotoka. Watanzania sasa wako tayari kumkasirikia milele mtu yeyote atakayeonekana kwa wazi au kwa kificho kuwa chanzo cha kuvunjika UKAWA na chanzo cha kushindwa uchaguzi 2015. Watamuandama kwa kumzomea na kumdharau mtu huyo popote atakapokuwa iwe msikitini, kanisani, barabarani au kwenye shughuli za kijamii kama misiba, atakosa raha ya kudumu ndani ya jamii yake.

Mfano, sitaki kuamini kuwa Dr. Slaa anaweza kupata amani ya roho kama akitoka chadema kwa wakati huu, wale watu waliomkweza hadi kuwa maarufu watamshusha chini tena kwa kasi ya ajabu sana kama atajitenga nao kwenye kipindi hiki kigumu na muhimu kwao.

Hataweza kupata maelezo yatakayowatosheleza mashabiki wa Ukawa ili kuhalalisha kujitenga kwake nao. Lowassa ni tegemeo sio tu kwa UKAWA lakini hata kwa CCM kwenyewe anakotoka. Lowassa ana rasilimali watu, fedha na software muhimu ambazo ndio vipuli muhimu kwenye gari la kuleta mabadiliko ya kisiasa nchini. Kumsusa Lowassa ni sawa na kuwasusa mashabiki wako na safari yao ya kuitoa CCM madarakani, lazima watakupa adhabu ya kisiasa unayostahili kwa kosa kama hili.

Ushauri wangu kwa mzee Dr. Slaa, sijui nani alikuahidi nini ndani au nje nchi ya nchi kama ukiwa rais wa nchi hii kinachokufanya hata usimuone tembo aliyeko kwenye sitting room yako, lakini wale tuliokufikisha hapo ulipo leo hii wanakuhitaji uwe nao katika kipindi hiki bila ya masharti yoyote kwa wafuasi, mashabiki na wasioipenda CCM kuingoza nchi hii tena miaka 5 ijayo.

Rudi kundini muda huu sio mwafaka kwa wewe kusemwa hivyo unavyosemwa sasa kwa kukaa kwako kimya
 
Tatizo ni kwamba,kuna watu wa ilmradi na watu wa misingi.
Dr Slaa kamwe sio mtu wa ilmradi.
Siamini hata kidogo kuwa ataondoka CHADEMA ila naamini kabisa hata kama alishiriki vikao vya kumleta Lowassa,binafsi hakuridhia.
Slaa bora abaki na msimamo ila uwe passive,vinginevyo ataleta hasara.
 
Aliyeinunua UKAWA yuko juu ya UKAWA.

Ndio maana mambo yote anayabadilisha anavyotaka na sasa anafanya kazi ya kumuadhibu yule aliyekuwa kinara wa kumuita fisadi.

Huo ni mwanzo tu wa visasi ambavyo vitaendelea kwa miaka yote atakayokuwa na nguvu.

Choice is yours...
 
Mlianza kwa ZZK sasa mmeamia kwa Dokta...Watanzania wameshawajua Chadema ni Chama cha Demoghasia na Mapambano/Malumbano
 
Aliyeinunua UKAWA yuko juu ya UKAWA.

Ndio maana mambo yote anayabadilisha anavyotaka na sasa anafanya kazi ya kumuadhibu yule aliyekuwa kinara wa kumuita fisadi.

Huo ni mwanzo tu wa visasi ambavyo vitaendelea kwa miaka yote atakayokuwa na nguvu.

Choice is yours...

Hayawahusu.. jikiteni kwenye kumnadi mgombea wenu
 
kavulata

Unamdhalilisha Dr. Slaa. Asingefika alipofika kama asingekuwa na utashi wake binafsi. Binadamu bila utashi binafsi hatofautiani na kitu.
 
Last edited by a moderator:
Naona umaeamua kijifariji na kujiliwaza kwa sasa Lowassa ndiyo mmiliki wa CHADEMA.

CHADEMA kwa sasa hawana ubavu wa kumnyoshea kidole Lowassa na timu zake.

Lowassa kwa sasa ni chama ndani ya CHADEMA.

Hukumuona Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa anavyo mnyenyekea Lowassa mpaka anamsindikiza Lowassa kwenye gari yake wakati yeye ni mwenyekiti wa CHADEMA Taifa.

Kiitifaki, Lowassa inabidi amsindikize mwenyekiti wa chama taifa kwa sababu Lowassa ndani ya CHADEMA ni mwanachama tu na hana cheo chochote. Kwa sasa ni kinyume chake!

Pesa na umaarufu wake ndiyo unawafanya viongozi wakuu wa CHADEMA wajishushe chini yake.

Money talks and money alone sets the entire world in.
 
Nashauri watu tuwe na staha kwenye kujenga hoja. Tunahitaji Dr Slaa kipindi hiki lakini tumpe uhuru atatupa mrejesho kama tulimwamini kwa miaka zaidi ya ishirini kwa nini tusivumilie?
 
kavulata

Unamdhalilisha Dr. Slaa. Asingefika alipofika kama asingekuwa na utashi wake binafsi. Binadamu bila utashi binafsi hatofautiani na kitu.
Watu hawapendi Dr. Slaa, wanapenda CCM isiendelee kubakia madarakani tena. Kama Slaa kwakukaa kimya kwake kutasaidia kuiondoa CCM madarakani ni sawa lakini kama itakuwa chanzo cha CCM kusalia madarakani wale waliomfanya Dr. Slaa apate umaarufu aliokuwanao leo lazima watauchukua umaarufu wake na kumuacha kama alivyokuwa.

Ndo maana mimi nasema sio Mbowe, Lissu, Mnyika wala Sugu aliye juu ya UKAWA ni wananchi wapenda mageuzi tu, ndo maana hata hawakutaka kuhoji usafi wala ujio wa Lowassa chadema. Kama Slaa anataka kujipima ili aone kama ni maarufu au laa, hebu aendelee na msimamo wake wa kuuchuna. ZZK alikuwa maarufu sana chadema lakini alivyotoka chadema watu wameshaanza kumsahau kisiasa
 
Hii tabia ya hawa wahuni wa vijiweni kumuita CCM kila anaetoa ukweli kuhusu tatizo lililopo ndani ya CHADEMA itaisha lini, nasikitika sana kuskia mtu anambeza Dr. Slaa kiasi hicho na kudai kuna watu waliomuinua!!! Huenda ukawa uliifaham chadema kipindi cha M4C hivyo haufaham ni nguvu gani imetumika kuifikisha hapo. Acheni kujifariji kwa mitazamo rahisi, huenda pengo la Dr. Slaa lisionekane kama ataamua kuondoka, lakini bado haifuti ukweli kwamba uwepo wake ungeongeza nguvu kubwa sana.
 
Tatizo ni kwamba,kuna watu wa ilmradi na watu wa misingi.
Dr Slaa kamwe sio mtu wa ilmradi.
Siamini hata kidogo kuwa ataondoka CHADEMA ila naamini kabisa hata kama alishiriki vikao vya kumleta Lowassa,binafsi hakuridhia.
Slaa bora abaki na msimamo ila uwe passive,vinginevyo ataleta hasara.
Sasa naaza kuamini kuwa wazee ni wagumu kunyumbulika haraka hata kunapotokea dharura, chama hakifai kuwa na wazee wengi kupita kiasi kwani walio wengi ni watu wa kushikilia misimamo hata ile isiyo na maslahi kwa taasisi wazoziongoza. Hata hivyo kunguru huwa hana kibiongo, ukiona ana kibiongo lazima atakuwa kainama anaokota kitu, sasa ni juu yako kumuahi kabla hajaruka nacho kama ni kitu chenye thamani kwako.

Unajua Dr. Slaa hatujui chanzo cha ukimya wake, tunaomba asiwe vuguvugu ajitokeze mapema hadharani aseme asikike kwa wana ukawa wote ili watu wamtungie nyimbo zinazomstahiki, maana wasanii wapo na data zake zipo. Ni kwanini ni lazima yeye atake awe mgombea urais kwa lazima? kuna nini?
 
Nashauri watu tuwe na staha kwenye kujenga hoja. Tunahitaji Dr Slaa kipindi hiki lakini tumpe uhuru atatupa mrejesho kama tulimwamini kwa miaka zaidi ya ishirini kwa nini tusivumilie?
Muda sio rafiki kwa wapenda mageuzi nchini, hakuna muda wa kubembelezana kuna muda wa kupanga mikakati ya namna ya kukabiliana na bao la mkono la Nape. Aseme tu kuwa kaacha chadema ili sisi mapunda wake tuliombeba hadi kufikia hapo alipo tujue nini cha kufanya mapema bila yeye.
 
Ritz

Uchaguzi mkuu ni pesa, chadema ilikuwa ikishindwa kuwafikia watanzania wote wakati wa uchaguzi kutokana na kukosa rasilimali fedha, kama kuna mtu kaja na pesa kwenye kipindi hichi basi pesa hiyo imekuja wakati mwafaka chadema na ukawa.

NI yale mazuzu tu ndo ambayo yanashindwa kuziona na kuzitumia fursa adimu kama hizi. Hata kama Lowassa asingejiunga Chadema CUF, NCCR, ACT na hata DP wangempokea Lowassa bila mashariti yoyote, Lowassa ni assert.
 
Last edited by a moderator:
kavulata

Dr.Slaa alivunjika mkono na hadi sasa ana ulemavu wa kudumu kwa sababu ya kuitetea chadema. yeye mwenyewe alipigwa na kuharibiwa mimba mwaka 2011 kwa sababu ya chadema halafu leo wanapuuzwa kama vile si chochote ndani ya chama.
 
Ritz

Jamani, kama CDM imeingiliwa na kupoteza mwelekeo nadhani ndiyo furaha ya CCM, inakuwaje sasa jambo hili linawasumbua sana watu wa CCM? Hamdhani kuwa watu ambao hawajachagua upande wanaweza kupatwa na mashaka na jitihada zenu?
 
Last edited by a moderator:
Mbona Lowasa yupo juu ya ukawa au huelewi kinachoendelea ndani ya taifa hili.
 
Back
Top Bottom