Hakika wewe ni Mwanamke wa karne

Hakika wewe ni Mwanamke wa karne

Sijuti kukupenda Mpenzi wangu, namshukuru Mungu kwa uthubutu alionipa kukuangazia Nuru hii ya mapenzi.

Hakika umegeuza jangwa lililokuwa moyoni mwangu kutiririsha vijito vya furaha katika maisha yangu. Hujui ninamna gani ninavyopenda jinsi ukiwa na furaha.

Endapo utaniuliza ni kiasi gani nakupenda basi nitashindwa kutoa jawabu kwani nakupenda kusiko elezeka.

Karibu katika ulimwengu mpya wa mapenzi, nitakupa mahaba moto moto mpaka mwisho wa dahari.
Nitakupenda hata nikifa, nitakupenda hata nikiwa peponi tutakapofufuliwa.
Nimejitoa muhanga kwaajili yako, nipo radhi niupoteze ulimwengu mzima kwaajili yako.

Najiona Mshindi kukupenda mpenzi Wang, nakupenda jamani.
Nakumbuka siku ile, ndio naikumbuka haswa, siku ya kwanza uliponiambia unanipenda. Kiukweli nilihisi nimezaliwa upya, Nimezaliwa nikiwa mtu mzima, nikiwa ninameno, ndevu na sifa zingine za utu uzima.
Ndio maana nakuita mwanamke wa karne mwanamke uliyeweza kunizaa nikiwa naongea, meno, Sauti nzito n.k

Najua wapo wataniona Mimi ni kichaa kwaajili yako, Mahabibi wala usiwajali, maana hawajui ni kiasi gani unanipa uzima wenye manufaa.

Acha nigeuke Kamusi kwako uyasome maneno matamu, maneno kutoka kwa Mfalme wa moyo wako.

Sitakuacha hata katika njozi naam katika ndoto za usiku, nitakuenzi katika maono yangu maana wewe ndiwe mwanamke wa karne Hii. Nimekupa Nobeli ya mahaba kwani umeushinda Mtima Wang.

Najua unapenda maneno matamu, maneno Asali, maneno ya huba, basi usijali hapa ndio nyumbani kwake.

Mwaaaaaa
kijana una maneno sana ila mm simuamini mwanamke ata 1% ni moja ya viumbe wa ajabu sana
 
kijana una maneno sana ila mm simuamini mwanamke ata 1% ni moja ya viumbe wa ajabu sana


Mkuu huwezi kuwa km mimi km hujakutana na mwanamke wa dizaini hii, mwanamke wa karne.

Siku ukikutana nae basi uje nawewe utoe ngonjera zako hapa.
 
Nilipiga sana mashairi kwa Liz mtoto wa Arusha lakini mpaka leo hajanielewa. Sasa wewe unakuja na gazeti la Mzalendo! Haya kila la heri.
 
Nilipiga sana mashairi kwa Liz mtoto wa Arusha lakini mpaka leo hajanielewa. Sasa wewe unakuja na gazeti la Mzalendo! Haya kila la heri.


Haya ni Mashairi kwa Wanawake wanaojielewa mkuu, wanawake wanaojua nguvu ulioitumia kufikiri haya, mwanamke mwenye kujua utamu wa kupetiwa petiwa.

Lakini ikiwa utamtemea mashairi mwanamke asiyejielewa atakuona kichaa, tena mwendawazimu.

Mwanamke kamili hupenda maneno rojo rojo Mkuu.
Huyo Liz wako hakuwa katika hisia ziile nizijuazo.

pia kuna point ambayo maneno haya hutolewa, ukiyatumia sehemu isiyotakiwa demu huwa anaona kero Fulani hivi.

Hivyo cheza na Mzunguko wake wa mwezi.
Ahsante
 
Back
Top Bottom