Hakika wewe ni Mwanamke wa karne

Hakika wewe ni Mwanamke wa karne

Ryan The King

JF-Expert Member
Joined
Oct 6, 2016
Posts
2,789
Reaction score
2,706
Nawasalimu kwa lugha zenu kwa kuzingatia rika, Imani, itikadi, mila na tamaduni zenu.

Nikirudi kwenye mada:

Nani asiyejua kuwa mapenzi ni matamu Asali ni kivuli chake? Pengine yupo, basi kama upo nataka nikuambie rafiki yangu kuwa mapenzi ni matamu saana kuliko kitu chochote.

Utamu wa mapenzi huletwa na mambo mengi sana, miongoni mwa mambo hayo ni pamoja na Maamuzi na uchaguzi sahihi.

Ili mapenzi yawe matamu yanakuhitaji uwe na maamuzi sahihi na uchaguzi sahihi kwa yule Umpendae, Lazima ujue kwa nini umeamua kumpenda huyo uliyekuwa nae na kwa nini umemchagua yeye na si Mimi ninayeandika hapa au yule apitaye barabarani.

Hakika maisha nayaona, maisha matamu. Mapenzi yamenifanya niwe tajiri japokuwa ni masikini, Yamenifanya niwe nafuraha wakati wote japokuwa nipo katika dhiki ya ugumu wa Maisha.

Utamu wa mapenzi ni kupeana bila choyo, japo kupeana huko kuwe na kanuni au sheria ambazo pengine ndio mipaka.

Utamu wa mapenzi ni kujisikia huru kwa mahabuba wako. Uhuru wa mwili wake, Mali zake, Fikra zake na pia katika maamuzi.

Haka katoto kakiafrika nimekaona ni zaidi ya chochote hapa duniani. Hakika wewe ni mwanamke wa karne.

Napenda ukitabasamu jinsi mng'ao wa meno yako meupe unavyonimulika machoni. Huwa natamani nikukumbatie kila Mara sema wakati mwingine tunakuwaga mbele za watu wengi.

Wewe ni Jojo, wewe ni tunda langu la Msimu. Umzuri kama kitu chakula, kitu chenye ladha tamu ulimini mwangu.

Nilikuahidi nitakubeba kila asubuhi, kila jioni mpaka kifo kitakapo tutenganisha.

Sijui kama ulichukua rambi rambi zako maana kwako nilikufa siku nyingi. Naiona furaha yako ikitimizwa na uzuri wa Pendo langu la dhati katika kisima cha moyo wako.

Wewe ni mwanamke wangu wa karne.
Mwanamke ambaye naishiwa irabu kuuelezea upendo wangu kwako.
Mwanamke wakiafrika, uupendao uzuri wako wa asili.

Rangi yako ndio hunifanya nipumue mithili ya bata dume, rangi ya hudhurungi yenye mwako hafifu wa weusi mpauko. Hakika ile tafiti ya vichaa inasema kweli kwani Mimi nami ni miongoni mwa vichaa kwako.

Napenda nywele zako ndefu na nyeusi kama ngozi ya mnubi. Nywele ambazo hujazichakachua na madawa ili ziwe kama za kizungu. Sijui ulijuaje kuwa nazipenda zikiwa hivyo. Zikipeperushwaga na upepo ndio huniacha kinywa wazi. Nakupenda saana My Jojo Wang.

Napenda nikikutania ukiwa umemaindi na kuungunja uso wako. Alafu ujitetee, daaaaaaa! Yaani unanimalizaga saana.
Macho yako makubwa kiasi ukiyavimbisha ndio nabaki nikiduwaa.

We ndiwe mwanamke wa Karne.
Karne ya 21, umenitega nikategeka, tego lako lahuba limenikamata.

Napenda ninavyokupenda, najisikia raha nikikuona unafuraha.

Kukupenda ndio furaha yangu na furaha yako ndio uzima wangu.
Mwaaaaa!


~Michaelray
 
Back
Top Bottom