adakiss23
JF-Expert Member
- Jan 23, 2011
- 4,949
- 5,399
Kuna familia ilikuwa na nyumba ya urithi baada ya wazee wao kufariki. Mara wazo likatoka nyumba iuzwe wagawane pesa. Wako karibu ndugu 7 hivi. Mmoja wao akawa anawahisi wasiuzwe bali wairekebishe waweke frem za biashara ili iwasaidie cz iko pembeni ya barabara. Ndugu wengine hakuunga mkono walisimama na zao lao na hatimaye nyumba ikaamuliwa iuzwe kwa Tsh 50m. Kwakuwa yule m1 (dada) aliyekuwa anapinga wazo la kuuza anajiweza basi akasema atainunua hiyo nyumba kwa pesa hiyo Tsh50m. Huku nae kwakuwa ana gawio lake atalikata uko uko. Zikapigwa hesabu. Kila m1 akala chake wakasepa. Yule mdada akabaki akairekebisha fresh akaweka frem ukawa mradi wake. Mara wale ndugu wengine wakachezea pesa zikaisha wanaanza kurejea m1 m1 ktk ile nyumba. Mdada kakomaa hataki kuona mtu. Ndugu wanakomaa wanasema nyumba ya baba yao hawatoki.
Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums