mpango mzima uko hivi,
1. alinunua kwa kufyata utaratibu wa mirathi? na ushahidi na kisha kubailisha hati kwa jina lake? kama Ndio.
a) Anaweza kuwafukuza, kwa mtindo wowote ule, polisi, mahakama, na kuwaitia ndugu wa ukoo.,... kama Hapana
b) auze nyumba hiyo, kwa njia mbili, kumuzia mumewe au nduguye, ila baadae atainunua tena toka kwa mtu huyo, ILA awe ni mtu wake wa karibu ambaye hataweza kumgeuka.
c) kama hakubaili umiliki wake auze yote kwa jumla na akaanze upya kwingine, hiyo itamsaidia kurudisha hela yake na kuokoa uhai wake.
d) kama ndugu zake wanakaa kwa sababu hawana pa kwenda maisha yamewapiga, basi awaache kama hawamsumbui maana pengine hataki kuwaona pale.
e) Awasiliane na wanasheria watampa mwongozo zaidi, kabla ya kwenda polisi, na kufanya maamuzi magumu.
Mwisho, hilo ni fundisho kubwa mali ya urithi hainunuliwi na mmoja wa wanafamilia, huuzwa tukose wote, ( hata kwa Muda) hivyo amefanya kosa kufanya ununuzi wa moja kwa moja , angefanya "third Party"
wakatabahu