Hakika spika Makinda hajamwelewa Tundu Lissu. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hakika spika Makinda hajamwelewa Tundu Lissu.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Ringo Edmund, Aug 1, 2012.

 1. Ringo Edmund

  Ringo Edmund JF-Expert Member

  #1
  Aug 1, 2012
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 4,895
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  Katika kufuatilia kauli ya makinda nimegundua hajamwelewa kamanda lissu.

  Lissu alipoongea na wanahabari alitaja majina ya wana ccm walio na mgongano wa maslahi na tanesco na sio waliokula rushwa ili kuikataa bajeti ya wizara ya nishati na madini.kamati aliyounda makinda ni ya kuchunguza rushwa sasa akimwita lissu kutoa ushahidi wa rushwa lissu ataupata wapi?

  Na je kuwa na mgongano wa kimaslahi ndio kupokea rushwa?

  Madai ni kuwa kuna wala rushwa na wenye mgongano wa kimaslahi.

  Naombeni tulidadavue hili wadau.
   
 2. SG8

  SG8 JF-Expert Member

  #2
  Aug 1, 2012
  Joined: Dec 12, 2009
  Messages: 3,198
  Likes Received: 232
  Trophy Points: 160
  Mimi naona wewe ndio hukumwelewa Lissu. Mbona aliweka kila kitu wazi? Na alichosema ni kile kilichosemwa na Waziri Muhongo kama vile biashara ya matairi na mafuta. Huo pekee ni ushahidi na hata Tundu Lissu mwenyewe sidhani kama atashindwa kutoa ushahidi na ninafikiri Spika yupo sahihi
   
 3. I

  IDIOS Member

  #3
  Aug 1, 2012
  Joined: May 3, 2012
  Messages: 84
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Tusubiri tuone mwisho wa jambo hili ni nini.
  Mgongano wa kimaslahi ni nini wadau?
  Kuchua rushwa ni nini wadau?
   
 4. N

  NOD JF-Expert Member

  #4
  Aug 1, 2012
  Joined: Mar 31, 2011
  Messages: 388
  Likes Received: 250
  Trophy Points: 80
  Ringo kasema kweli. Inashangaza hata Nape kakurupuka kusema kuwa Mh. lissu kataja wala rushwa! Alichotaja Lissu ni watu wenye mgongano wa maslahi (conflict of interest).

  Nina hakika Mwanasheria huyu mahiri anachekelea jinsi uelewa wa watu wanokurupuka ulivyo mdogo.

  Mgomgano wa maslahi unaweza usiwe ni rushwa bali ukawa ni sababu ya mhusika kutokutenda haki ili kulinda maslahi yake.
   
 5. Mwanamayu

  Mwanamayu JF-Expert Member

  #5
  Aug 1, 2012
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 7,936
  Likes Received: 2,085
  Trophy Points: 280
  Nafikiri Lissu atawaambia nilimaanisha 'maadili' mabovu ya utumishi though rushwa ni mojawapo lakini nilimaanisha ilie la 'conflict of interest' na ushahidi ni Waziri wa nishati kupitia hansard!!
   
 6. S

  SURUMA JF-Expert Member

  #6
  Aug 1, 2012
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 2,908
  Likes Received: 124
  Trophy Points: 160
  Samahani kuuliza; kwani kuna wakati huwa anawaelewa waheshimiwa wa kambi ya upinzani??
   
 7. e

  evoddy JF-Expert Member

  #7
  Aug 1, 2012
  Joined: Nov 9, 2011
  Messages: 302
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Hapa kwenye mgongano wa kimasilahi kuna tatizo hili linaanzia kwa viongozi wetu,huwezi kuisimamia wizara na mashirika yake harafu wakati huo ukafanya biashara na mashirika hayo huu ni wizi na ni kosa kimaadili.
  Kuhusu rushwa na wizi je hizo kampuni zao zimeorodheshwa na kuonyeswa kwenye kamati ya maadili ya viongozi kuwa wanazimiliki?Kama hakuna basi hilo ni kosa lingine.

  Tunahitaji wazalendo katika kulisimamia taifa letu
  :A S cry:for TANZANIA
   
 8. Ndukidi

  Ndukidi JF-Expert Member

  #8
  Aug 1, 2012
  Joined: Jun 30, 2012
  Messages: 821
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 80
  Mgongano wa kimaslahi - Conflict of interest
  Mfano mdogo ni huu, mfano mimi ni mfanyakazi wa kampuni A meneja usafiri, lakini pia nina kampuni yangu binafsi ya usafirishaji. Sasa haiwezekani mimi leo niamue kuipa kazi kampuni yangu kusafarisha/kubeba mizigo kwenye kampuni ambayo nimeajiriwa yaani kampuni B.
   
 9. yegella

  yegella JF-Expert Member

  #9
  Aug 1, 2012
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 3,116
  Likes Received: 158
  Trophy Points: 160
  Kuna nchi za wengine mfano kama wewe ni mkulima wa matunda huruhusiwi kutengeneza juice, lakini hapa una kuna kiwanda kinacho tengeneza juice ndicho kincho safarisha, kinauza jumla jumla wakati huo kina uza rejareja.. hii naamini inatokea hapa kwetu tu.
   
 10. N

  Njaare JF-Expert Member

  #10
  Aug 1, 2012
  Joined: Sep 26, 2010
  Messages: 1,075
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Katika sheria ya Rushwa kuna kifungu kinachohusiana na kujipatia manufaa au Obtaining advantage without lawful consideration.

  Kifungu hicho kinasema ni kosa la rushwa kwa mtumishi wa uma kupokea chochote toka kwa mtumishi ambaye alimhudumia, anamhudumia, au atakuja kumhudumia wakati akitekeleza majukumu yake ya kazi.

  Mi si mwanasheria ila mi ninaona kuwa hawa wabunge wajipatia manufaa wakati wakijua kuwa wanaisimamia Tanesco. Hata kama Lisu hakutamka kuwa walipokea Rushwa, kujipatia manufaa toka Tanesco ni kosa la Rushwa.
   
 11. t

  thatha JF-Expert Member

  #11
  Aug 1, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  Haya wewe utakuwa wakili wa LISSU atakapohojiwa na kamati ya maadili ya bunge, Mkuu hilo LISSU analo hawezi kukwepa. Sasa tunaanza kuona hasara ya kuropoka.
   
 12. e

  evoddy JF-Expert Member

  #12
  Aug 1, 2012
  Joined: Nov 9, 2011
  Messages: 302
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Mfano nchi kama America huwezi kufanya biashara na taasisi unayo isimamia au kuiongoza Je!wakati hizi kamati zinateuliwa kuna kipengele kinachomzuia mbunge kufanya biashara na shirika au taasisi inayosimamiwa na kamati husika?Kama hakuna basi bunge na serikali walifanya hivyo makusudi
   
 13. T

  Tata JF-Expert Member

  #13
  Aug 1, 2012
  Joined: Dec 3, 2009
  Messages: 4,729
  Likes Received: 645
  Trophy Points: 280
  Mgongano wa kimaslahi ni dhana pana ndugu Idios.

  Kwa ufupi dhana hii inaanzia kwenye malengo ya uwepo wa kampuni au taasisi ya umma/binafsi. Kila kampuni/taasisi ya umma/binafsi inaanzishwa kwa malengo maalumu. Lakini bila kujali aina ya taasisi lengo kuu la taasisi yoyote ile ni kuwapatia ama faida au huduma bora wamiliki wake ambao ndio hasa walengwa wakuu. Haya malengo ya taasisi kwa ujumla wake yanaitwa maslahi ya kampuni au taasisi.

  Ili Taasisi ifikie maslahi yake hulazimika kuajiri wafanyakazi ambao jukumu lao kubwa hi kuhakikisha kuwa malengo makuu ya kampuni/taasisi yanafikiwa. Waajiriwa hawa hulipwa mshahara na marupurupu mengine ili waweze kutelekeza majukumu yao bila kuathiri maslahi ya waajiriwa wao. Lakini ni ukweli usiopingika kuwa kila mwajiriwa naye ana malengo binafsi ambayo yanatofautiana toka mtu mmoja mpaka mwingine. Haya malengo binafsi ya waajiriwa mara nyingi yanahitaji pesa zaidi ya mshahara na marupurupu ili kuyafikia. Haya malengo ya waajiriwa kwa ujumla wake yanaitwa maslahi binafsi.

  Inapotokea mwajiriwa akatumia mamlaka yake aliyopewa kwa ajili ya kuiwezesha taasisi kufikia malengo yake kupata pesa za ziada ili afikie malengo yake binafsi tunasema kuna mgongano wa maslahi.

  Mfano: Mhando wa Tanesco amepewa madaraka ya ukurugenzi mkuu ili aitumikie taasisi yake. Analipwa mshahara na marupurupu kwa ajili hiyo. Inapotokea Mhando akatumia mamlaka yake ya ukurugenzi mkuu wa Tanesco kutoa upendeleo kwa kampuni yake binafsi kupata kazi ya kusambaza stationeries kwa Tanesco anakuwa ameingia kwenye mgongano wa kimaslahi. Kwani ametumia madaraka ya umma kutoa kazi kwa kampuni itakayompatia faida binafsi.

  Unaweza ukaipanua dhana hii kwa wabunge ambao wameajiriwa na wananchi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuisimamia Tanesco ili itimize malengo ya kuanzishwa kwake. Wanapotumia nafasi hiyo kushinikiza na kupata biashara ya kusambaza mafuta ama bidhaa nyingine yoyote kwa shirika la Tanesco wanakuwa na mgongano wa kimaslahi kwani hawawezi tena kuisimamia Tanesco.

  Kuchukua rushwa
  ni kupewa pesa au upendeleo mwingine wowote ili ufanye maamuzi yanayompendelea yule aliyekupa pesa au kitu kingine chochote.
   
 14. J

  Joel gaby New Member

  #14
  Aug 1, 2012
  Joined: Jul 30, 2012
  Messages: 3
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tusubiri taa ya kijani tuone yatakayo jiri mapaka sasa wote tupo gizani tu
   
 15. Philipo Kidwanga

  Philipo Kidwanga Verified User

  #15
  Aug 1, 2012
  Joined: Jul 12, 2012
  Messages: 2,063
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  siwezi kuchangia mengi masikini tz inadidimia ardhini kila mwenye nafasi kidogo anazoa kilichopo,watu wanakula bila kunawa.ooooooooooh tz tunakupoteza kwa moyo wote.
   
 16. K

  KEBUKA New Member

  #16
  Aug 1, 2012
  Joined: Aug 1, 2012
  Messages: 4
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Natamani Mwl.Nyerere afufuke asimamie maadili ya viongozi.Jambo la conflict of interest linawatesa Watanzania wengi.Viongozi wa umma ambao ndio wasimamizi wa mali/maslahi ya umma ndio wafanyabiashara wakubwa na hao hao ndio wenye tenda nyingi katika mashirika ya umma.Kutokana hali hiyo kiongozi wa umma ambaye anayotenda mahali anapofanyia kazi i.e shirika la umma kamwe hawezi kulinda maslahi ya umma bali maslahi ya kampuni yake iliyopewa tenda ndani ya shirika la umma analoliongoza.Tokea raisi awamu ya tatu ndipo watumishi wengi walipoteza haki ya nyongeza ya mishahara kwa sababu wasimamizi wa haki za watumishi ndio wana makampuni makubwa hivyo kwa viongozo hao kukubali nyongeza za mishahara maana yake kampuni zao zinapunguza mapato kwa kulipa mishahara mikubwa!! Taifa limepotoka afufuke Mwalimu awachape bakora na kuwaweka vizuizini!
   
 17. M

  Mnyakatari JF-Expert Member

  #17
  Aug 1, 2012
  Joined: Oct 25, 2010
  Messages: 1,555
  Likes Received: 485
  Trophy Points: 180
  Kinachonishangaza kwenye hili ni kwa vipi jambo lililozungumzwa kwenye ofisi ya upinzani bungeni liwe na kinga ya bunge.Nilifikiri kuwa hili liwe suala la mahakamani badala ya kamati ya haki na madaraka ya bunge.Lakini kwa kutumia tafsiri mpya ya bunge ya bw.Ndugai siku ile alipomtoa Mnyika nje ya ukumbi wa bunge alisema kuwa aende nje kabisa kwa kuwa hata viunga vya nje ya ukumbi wa bunge ni ukumbi wa bunge bado!

  Kuna haja ya kuangalia upya tafsiri hizi za maneno kwenye kanuni za bunge kwani kwa mtazamo wangu mara nyingi kiti kinatoa tafsiri yenye maslahi nacho.Ni kwa jinsi gani jambo lililoongelewa nje ya ukumbi wa bunge linakuwa counted kama vile limezungumzwa kwenye ukumbi wa bunge.

  Mpaka sasa ni mambo mangapi upinzani wamezungumza kwenye hiyo ofisi yao ndogo hapo bungeni.Je yote yana kinga ya bunge au ni hili tu?

  Na kama Zitto pia leo ataitumia ofisi hiyo wakati akiongea na waandishi wa habari ina maana yote atakayoongea tayari yana kinga ya bunge na mtu yeyote hawezi kumshtaki mahakamani bila kupitia kanuni za bunge?
   
 18. Manyi

  Manyi JF-Expert Member

  #18
  Aug 1, 2012
  Joined: Dec 6, 2011
  Messages: 3,256
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Ni kweli mkuu, tatizo watu huwa wana generalise sana statements za Lissu, hawajui kuwa unatakiwa uziangalie kwa jicho la tatu! Manake huwa hakurupuki na taaluma yake ya Sheria inampa uelewa mkubwa sana, nashangaa watu wasiojua maana ya "Mtu mwenye Conflict of Interest" na yule ambaye ni Mla Rushwa, japo Conflict of Interest ina association kubwa tu na rushwa!
   
 19. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #19
  Aug 1, 2012
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,762
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  hii nchi itakuja kuendelea tu kama mijitu kama ninyi asilimia 20 ipotezwe!
   
 20. F

  FJM JF-Expert Member

  #20
  Aug 1, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Ndio sababu ni muhimu sana kiti cha Spika kikakaliwa na mtu aliyesomea sheria. Kanuni za bunge ziko wazi kabisa, kwamba kama mbunge ana maslahi kwenye jambo/shirika lazima aweke wazi. Baadhi ya wabunge wa CCM ambao wako kwenye kamati ya nishati na madini wanafanya biashara na Tanesco (e.g. supply matairi) lakini wakati huo huo wanaisimamia Tanesco! Na mbaya zaidi hawakuweka wazi mgongano huu wa kimaslahi kama ambavyo kanuni za bunge zinavyoelekeza.

  Mgongano huu maslahi ndio aliousema Prof Muhongo na ndicho hicho hicho alichosema Lissu. Tofauti ni kwamba Lissu kataja majina ya wabunge wenye maslahi. Tukumbuke uongozi wa Tanesco uliosimamishwa ndio uliotoa tender kwa hao wabunge waliotuhumiwa hivyo kitendo cha wao (wabunge) kumtetea Mhando wa Tanesco kinaweza kutafsiriwa kuwa ni kutetea 'tender' zao maana akiondoka Mhando mambo yanaweza kuwaendea kombo.


  Sielewe utashi wa Spika kwenye hili maana amerukia upande wa mipasho wakati anajua fika hoja iliyosemwa na Lissu ya mgongano wa maslahi. Tuna kazi sana.
   
Loading...