jerryempire
JF-Expert Member
- Jan 4, 2017
- 5,128
- 8,648
Habari,
Katika maisha ya binadamu kuna mapito ambayo huwezi kuyapitia nami siku ya jana na leo huenda zikawa siku ngumu zaidi maishani mwangu kwa kupata wagonjwa 3 kwa kipindi kimoja na wote kuwa hoi kwa wakati mmoja.
Kwa sisi waislamu ugonjwa ni ibada lakini hakuna kitu kinachouma kama unampeleka mgonjwa hospital halafu anawekewa mpaka oxygen lakini hamuambiwi tatizo ni nini.
Wagonjwa wenyewe ni baba yangu mzazi, baba yangu mkubwa na mjomba wangu wote wa familia moja.
Tumepambana tuwezavyo jana saa 2 asubuhi amefariki baba yangu mkubwa, wakati tunaandaa mwili, mjomba nae amefariki.
Tukiwa katika hali ya kuendelea na taratibu nyengine asubuhi hii baba yangu amefariki.
Wagonjwa wote ilibidi wawekwe I.C.U kati hospital ya Regency, Hindu Mandal, na TMJ lakini zote I.C.U zilikuwa zimejaa.
Kwa upande wa mochwari ningeomba nikae tu kimya
Yarrab naomba nipe nguvu katika kipindi hiki kigumu