Hakika siku ya leo sitaisahau maishani mwangu

jerrybanks

JF-Expert Member
Jan 4, 2017
3,544
2,000
Habari,

Katika maisha ya binadamu kuna mapito ambayo huwezi kuyapitia nami siku ya jana na leo huenda zikawa siku ngumu zaidi maishani mwangu kwa kupata wagonjwa 3 kwa kipindi kimoja na wote kuwa hoi kwa wakati mmoja.

Kwa sisi waislamu ugonjwa ni ibada lakini hakuna kitu kinachouma kama unampeleka mgonjwa hospital halafu anawekewa mpaka oxygen lakini hamuambiwi tatizo ni nini.

Wagonjwa wenyewe ni baba yangu mzazi, baba yangu mkubwa na mjomba wangu wote wa familia moja.

Tumepambana tuwezavyo jana saa 2 asubuhi amefariki baba yangu mkubwa, wakati tunaandaa mwili, mjomba nae amefariki.

Tukiwa katika hali ya kuendelea na taratibu nyengine asubuhi hii baba yangu amefariki.

Wagonjwa wote ilibidi wawekwe I.C.U kati hospital ya Regency, Hindu Mandal, na TMJ lakini zote I.C.U zilikuwa zimejaa.

Kwa upande wa mochwari ningeomba nikae tu kimya

Yarrab naomba nipe nguvu katika kipindi hiki kigumu
 

Planett

JF-Expert Member
Mar 20, 2014
9,301
2,000
tumepambana tuwezavyo jana saa 2 asubuhi amefariki baba yangu mkubwa,wakati tunaandaa mwili,mjomba nae amefariki.

Tukiwa katika hali ya kuendelea na taratibu nyengine asubuhi hii baba yangu amefariki.
mkuu pole sana akika kila nafsi itaonja umauti
hakuna kitu kinachouma kama unampeleka mgonjwa hospital alafu anawekewa mpka oxygen lakin hamuambiwi tatizo ni nini.
it's painful.
 

Tate Mkuu

JF-Expert Member
Jan 24, 2019
10,436
2,000
Hii habari umei copy na kui paste kutoka mahali fulani kwa ajili ya kutoa funzo kwa sisi wasafiri wengine tunaoishi kwa matumaini, au? Kama inakuhusu mwenyewe, basi nichukue nafasi kukupa pole.

Hakuna namna. Kiukweli hali mtaani imechafuka. Vifo ni vingi sana! Hata mimi huku niliko, misiba haiishi. Corona imekuja kivingine. Ni aibu kuona serikali inafanya utani tu.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom