Kipindi nipo chuo mwaka wa 3 DSM nilikuwa na wasichana wengi sana ila miongoni mwao wawili wamekufa na ngoma, cha kushangaza mimi sijaunasa namaanisha umenikosakosa.
Inanishangaza sana kwani mmoja kuna siku niliuza mechi na pia kuna siku katikati ya shughuli condom ilipasuka na goli la pili nikajikuta nimemwaga nyavuni iyo siku nakumbuka huyo msichana alikuwa na presha na wasiwasi sana maana mienendo yangu na tabia yangu ya uasherati alikuwa anaijua huyo mwingine nilikuwa nikitumia kinga daily sema kuna siku nilipiga kavu kimoja ila ni miaka imepita na nimepima mara kibao nimekuta hollaah.
Ni maajabu ila sometimes kuna miracle labda walipata baada ya kuachana na mimi uwezi tambua.
Kisa hiki nimekikumbuka baada ya kumuona binamu yangu anavyotaabika na UKIMWI yupo kitandani hoi bin taabani analia kama mtoto mdogo wajameni kuweni makini UKIMWI ni hatari.
(Wapumzike kwa amani mahali pema peponi)
NB.
Msichana mmoja kati ya hao wawili alikuwa anasoma ustawi alifariki mwaka juzi nilijua baada ya kuona watu wameposti picha za R.I.P katika social network. Mwingine nilimuona amepostiwa R.I.P kwenye profile picture ya demu mmoja nilikuwa natoka naye kipindi hiko lakini yeye alikuwa ajui. Anyway nafikiria huu ni wakati wa kuachana na michepuko.
Hii ni true story ni ndefu ila huo ndio ufupisho wake